Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, imesema itaendelea kuimarisha mifumo ya huduma za afya kupitia tafiti mbalimbali ili kuhakikisha wagonjwa wenye magonjwa adimu wanapata huduma stahiki na kwa wakati.
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema hayo leo Machi 4, 2026 wakati akifungua Kongamano la 16 la kusambaza matokeo ya tafiti za magonjwa adimu lililoanfaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kushirikiana na AKRDF foundation jijini Dar es Salaam.
Pia Dkt.Magembe, amesema serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za chuo hicho kuwa kitovu cha ubora, ubunifu na utafiti kwa maendeleo ya taifa na ukanda wa Afrika Mashariki.
Amesema Serikali inayapa uzito stahiki magonjwa haya adimu, ili yaweze kushughulikiwa kwa kina na upana wake, kwa kushirikiana na Taasisi kama Ali Kimara, mashirika na sekta binafsi hivyo kuùwafikia watoto wengi zaidi," amesema Dkt. Magembe.
Ameeleza kuwa MUHAS ina wajibu wa kuongoza tafiti na kuzalisha wataalamu mahiri katika sekta ya afya. Aidha, amebainisha kuwa serikali itaendelea kuboresha huduma za rufaa na kuimarisha mifumo ya matunzo inayounganisha huduma za msingi na za kibingwa.
Kwa mujibu wa Dkt. Magembe, duniani kuna zaidi ya magonjwa adimu 7,000 yanayoathiri takribani watu milioni 400. Asilimia 80 ya magonjwa hayo husababishwa na vinasaba, na wastani wa mtu mmoja kati ya 2,000 huathirika.
Amesema kuwa nchini Tanzania, inakadiriwa kuwa asilimia sita ya wananchi wanaweza kuwa na aina fulani ya ugonjwa adimu.
"Miongoni mwa magonjwa adimu yanayoonekana zaidi ni selimundu, hemofilia, tawahudi, lupus erythematosus na Gaucher.
Aidha, Dkt. Magembe amesema hadi kufikia Desemba mwaka 2025 zaidi ya wataalamu wa afya 200 katika vituo 14 walikuwa wamepatiwa mafunzo ya kuanzisha vitengo vya tiba ya magonjwa adimu ikiwemo 'hemofilia' kuanzia ngazi ya msingi.
"Serikali imeshachukua hatua za kujenga uwezo wa maabara yetu ya Taifa, mafunzo kwa wataalamu wa Afya na kuanzisha vitengo maalum vya matibabu ya magonjwa adimu kuanzia ngazi ya msingi (Zahanati, kituo cha afya na hospitali za wilaya), tulianza na Seli mundu (Sickle cell) na sasa Hemofilia ambapo tayari wagonjwa 500 wamegundulika na wanaendelea na tiba,” amesema Dkt. Magembe.
Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS , Profesa Emmanuel Balandya, amesema MUHAS inatambua jukumu lake katika utoaji wa elimu, utafiti na huduma zinazohusu magonjwa adimu.
Ametaja changamoto zilizopo kuwa ni pamoja na uhaba wa vipimo vya vinasaba, gharama kubwa za uchunguzi na utegemezi wa maabara za nje ya nchi.
Ameongeza kuwa kupitia tafiti, ubunifu na ushirikiano na wadau, chuo kinaendelea kutafuta suluhisho endelevu yatakayotekelezwa ndani ya mfumo wa afya nchini.
“Kongamano hili, limeandaliwa kama jukwaa la kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kuibua mapendekezo yatakayobooresha utambuzi, matibabu na ubora wa maisha ya wagonjwa. Pia litatumika kusikiliza maoni ya wagonjwa na familia zao na kujadili namna bora ya kuimarisha rufaa kuanzia ngazi ya msingi hadi huduma za juu’ amesema Profesa Balandya.
Naye Mwenyekiti wa AKRDF, Sharifa Mbaraka, amesema matokeo ya tafiti yanatarajiwa kuleta maboresho chanya kwa watoto na jamii kwa ujumla, hasa yatakapoingizwa katika sera za afya.
Ameeleza kuwa makubaliano na MUHAS yanalenga kuanzisha tafiti mahususi, akibainisha kuwa kwa sasa watoto wenye magonjwa adimu hawatambuliwi ipasavyo katika mifumo ya bima ya afya, hivyo wanahitaji msaada zaidi.
Kaulimbiu ya mwaka huu, “Magonjwa Adimu: Ni Zaidi ya Tunavyoweza Kufikiria,” inalenga kuhamasisha jamii kutambua suala hilo kama ajenda ya kijamii, kielimu, kiutafiti na kisera inayohitaji ushirikiano wa wadau wote.

Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe akizungumza leo Machi 4, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa akifungua Kongamano la Magonjwa Adimu 2026 lililoandaliwa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa Kushirikiana na Taasisi ya Ali Kimara Rare Disease Foundation (AKRDF)

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS , Profesa Emmanuel Balandya, akizungumza leo Machi 4, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Magonjwa Adimu 2026 lililoandaliwa na MUHAS kwa Kushirikiana na AKRDF.
Mwenyekiti wa AKRDF, Sharifa Mbaraka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa Kongamano la Magonjwa Adimu 2026.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS , Profesa Emmanuel Balandya (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa AKRDF, Sharifa Mbaraka wakisaini mkataba wa makubaliano kwa ajili ya kufanya tafiti kuhusu magonjwa adimu leo Machi 4, 2026 jijini Dar es Salaam

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...