NA FARIDA MANGUBE , MOROGORO

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, mamlaka ya mapatao Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro imetumia maadhimisho hayo kutoka elimu ya masuala ya kodi pamoja na huduma ya usajili wa namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN).

Maadhimisho hayo kimkoa yameyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ambapo yamewakutanisha wanawake kutoka sehemu mbalimbali walioungana kwa pamoja kusherehekea siku hiyo huku wakipata huduma na elimu kutoka kwa taasisi za serikali ikiwemo TRA

Katika banda la TRA, wananchi walipatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa pamoja na kufahamu taratibu za usajili wa namba ya TIN, hususani kwa wafanyabiashara wanawake ambao wengi wao wanajishughulisha na shughuli ndogo ndogo za kiuchumi.

Afsa Mwandamizi wa Huduma na Elimu Mawasiliano Bi Immaculate Chagguaakitoa elimu katika maadhimisho hayo amesema kuwa namba ya TIN ni hatua muhimu kwa mfanyabiashara kwani humwezesha kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria pamoja na kupata fursa mbalimbali za kiuchumi.

Mbali na kutoa elimu, mamlaka hiyo pia ilitoa huduma ya usajili wa namba za TIN papo kwa papo kwa wananchi waliojitokeza katika viunga vya maadhimisho hayo.

Huduma hiyo imepokelewa kwa furaha na wanawake pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Mwajuma Omary mkazi wa Kijiji cha Fulwa, ambapo amesema kuwa hatua ya TRA kusogeza huduma karibu na wananchi imewasaidia kuokoa muda na gharama ambazo wangetumia kufuata huduma hiyo ofisini.

Nae Mwajabu Othuman kutoka Malinyi amesema kuwa upatikanaji wa huduma hiyo katika maadhimisho hayo umewapa hamasa zaidi ya kujiunga katika mfumo rasmi wa ulipaji kodi na kuendesha biashara zao kwa kufuata taratibu za kisheria.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hufanyika kila mwaka Machi 8 duniani kote yakilenga kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii pamoja na kuhamasisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika nyanja mbalimbali za maisha.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...