Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
MAHAKAMA Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imeitupilia mbali kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali kati ya Tanzania Bara na Zanzibar iliyokuwa ikiikabili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kuridhika kuwa hati ya madai ilikuwa na kasoro za kisheria.
Uamuzi huo umetolewa leo Mei 28, 2026 na Jaji David Ngunyale aliyekubaliana na pingamizi la awali lililowasilishwa na Chadema kuwa wadai walishindwa kubainisha muda rasmi ambao madai yao yalitokea kama inavyotakiwa kisheria.
Katika uamuzi wake, Jaji Ngunyale alisema baada ya kupitia hati ya madai alibaini kuwa baadhi ya matukio yalitajwa kwa ujumla kwa miaka ya 2014 na 2019 bila kuonesha tarehe rasmi ambazo mgogoro huo ulianza.
Alisema Amri ya VII kanuni ya 1(e) ya Kanuni za Mwenendo wa Mashauri ya Madai (CPC) inataka mlalamikaji kubainisha muda ambao sababu ya madai ilitokea ili mahakama iweze kujiridhisha kama kesi imefunguliwa ndani ya muda unaotakiwa kisheria.
“Hivyo mahakama inashindwa kujiridhisha kama ina mamlaka ya kuisikiliza kesi hii au la. Kitendo cha mahakama kushindwa kuona mgogoro ulianza lini ni upungufu ambao mahakama inayosimamia sheria haiwezi kuuacha hivihivi,” alisema Jaji Ngunyale.
Kutokana na sababu hizo, mahakama ilitupilia mbali kesi hiyo huku ikielekeza kila upande kubeba gharama zake.
Kesi hiyo ya madai namba 8323 ya mwaka 2025 ilikuwa imefunguliwa na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chadema, Said Issa Mohamed pamoja na wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.
Waliofunguliwa kesi walikuwa ni Bodi ya Wadhamini Waliosajiliwa wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Katika madai yao, wadai walidai kuwa kumekuwa na mgawanyo usio sawa wa mali na rasilimali za kifedha za chama kati ya Tanzania Bara na Zanzibar kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa pamoja na Katiba ya Chadema.
Pia walidai kuwepo kwa ubaguzi wa kidini na kijinsia pamoja na matamko yenye nia ya kuvuruga Muungano wa Tanzania.
Mbali na madai hayo, waliomba mahakama kusitisha shughuli zote za kisiasa za chama hicho pamoja na matumizi ya mali na fedha zake hadi maagizo ya mahakama yatakapotekelezwa.
Awali, upande wa wadaiwa uliwasilisha pingamizi la awali ukidai kesi hiyo ilikuwa na kasoro za kisheria pamoja na kufunguliwa nje ya muda uliowekwa na sheria.
Kiongozi wa jopo la mawakili wa wadaiwa, Mpale Mpoki, alidai kuwa hati ya madai haikuonesha ni lini sababu ya madai ilitokea jambo lililoifanya mahakama ishindwe kutambua kama kesi imefunguliwa ndani ya muda au la.
Alisema matakwa ya Amri ya VII kanuni ya 1(e) ya CPC yanahitaji mlalamikaji kueleza wazi muda wa kutokea kwa madai hayo.
Upande wa wadai ukiongozwa na wakili Shabani Marijani ulidai kuwa hati ya madai ilikuwa imeeleza matukio mbalimbali katika aya ya saba hadi ya 16 na kwamba baadhi yake yalikuwa yanaendelea hadi sasa.
Hata hivyo, mawakili wa Chadema walisisitiza kuwa maelezo hayo hayakubainisha tarehe rasmi ya kuanza kwa mgogoro huo.
Kabla ya uamuzi huo, Mahakama ya Rufani Aprili 15, 2026 ilibatilisha sehemu ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliokuwa umekizuia chama hicho kufanya shughuli za kisiasa na kutumia mali zake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.
Mahakama ya Rufani pia ilielekeza kesi hiyo isikilizwe na jaji mwingine tofauti na Jaji Hamidu Mwanga aliyekuwa akiisikiliza awali na kuagiza pingamizi kuhusu ukomo wa muda lisikilizwe kwanza.
Kutokana na uamuzi wa leo, shauri la maombi lililokuwa limewasilishwa na Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, nalo limekoma kwa kuwa lilitegemea uwepo wa kesi hiyo ya msingi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...