Na Ashura Mohamed -Arusha 

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imepongeza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ukiongozwa na Mkurugenzi wa Jiji, Ndugu John L. Kayombo, pamoja na timu ya Menejimenti kwa usimamizi madhubuti wa miradi ya maendeleo na ushirikishwaji mzuri wa wananchi katika utekelezaji wake.

Pongezi hizo zimetolewa leo, Juni 6, 2026, wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Soko la Mrombo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ndani ya Jiji la Arusha.

Kamati hiyo imeeleza kuridhishwa na hatua za utekelezaji wa mradi huo pamoja na namna Halmashauri ilivyozingatia uwazi, usimamizi wa rasilimali za umma na ushirikishwaji wa wananchi, mambo ambayo yameendelea kuimarisha thamani na tija ya miradi ya maendeleo kwa jamii.

Aidha, wananchi waliofika katika eneo la mradi wakati wa ziara hiyo walitoa shukrani zao kwa Serikali kwa kutekeleza mradi huo mkubwa, wakieleza kuwa utakuwa chachu ya kukuza shughuli za biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Jiji la Arusha na maeneo jirani.

Pamoja na pongezi hizo, wananchi hao waliomba kuboreshwa kwa miundombinu ya barabara zinazozunguka soko hilo mara baada ya kukamilika kwake. Akijibu ombi hilo, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Ndugu John L. Kayombo, aliwahakikishia kuwa eneo lote linalozunguka Soko la Mrombo litaboreshwa kwa kujengwa barabara za lami ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa.

Ziara ya Kamati ya LAAC ni sehemu ya jukumu lake la kusimamia matumizi sahihi ya fedha za umma na kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa inakidhi malengo yaliyokusudiwa na kutoa manufaa kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...