Mamboz?

Naandika nikiwa nina masaa machache kabla ya kupaa kurudi bongo 11/09/05 ambapo naambiwa niamke saa 11 alfajiri (urgh!) kuwahi pipa. Hata hivyo nafurahi kusema kwamba nimepata faraja kukutana na wabongo kibao waishio helsinki, ambao wote si wabangaizaji kama nilivyodhani, wote wanafanya kazi za maana na heshima. Bravo 2 u guys! Shukrani za pekee ziende kwa fide tungaraza, dennis londo, stephen lyabandi, kisa kisa (?) kiwala, eric kilala, beni kakengi, magonela malima, ray mtafungwa na tiko mwalukasa waliotupa taff pale chelsea club, helsinki. mie niliingia mitini wakati fulani kutokana na mwaliko mwingine sehemu ingine (unajua tena ukiwa supastaa - hahahaaaa!) na kushindwa kurudi mahali pale ambapo nilifurahi ila tu sema ningefurahi hiyo klabu ingekuwa liverpool kwani mie ni "neva wok aloni" damu.

Vinginevyo, alamsiki ya kuonana. nasema tena mtu akitaka kuona snepu yoyote ya bongo anibonyeze tu!

Chaaaaooo!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ndiyo mzee,
    Ilikuwa vizuri sana kukutana tena baada ya miaka mitano. Mara ya mwisho nilivyokuja 2003 hatukutana kutokana na shughuli iliyonileta na muda kuwa mdogo.
    Basi ile ni sehemu tu ya vijana wa Kitanzania ambao uliwakuta Sports Pub Chelsea. Ungelikuta kundi zima la wana Helsinki ungefurahi na roho yako maana kuna mchanganyiko maalum wa machizi maarifa ambao huwa ni burudani sana kuwa nao. Rais Mkapa ilibidi aongeze saa nzima na nusu ya kikao kwa jinsi walivyokuwa wanamchengua na hoja, maswali, na mijadala ya Kitaifa na Kimataifa.

    Bwana Michuzi, pole na hongera kwa utalaam wako wa kuongoza 'kiti moto' vinginevyo mambo yangekuwa mengine! Ndugu yangu, yule jamaa ni mfano wa wengine wengi ambao huwa tunawapokea na kufanya majadiliano nao. Ninaweza kusema kuwa wa namna ile ni asilimia tisini na tisa 99% ya viongozi na watendaji serikali ambao tumepata kukutana na kuongea nao! Kwa kweli inasikitisha sana. Hata hivyo haikatishi tama isipokuwa inapandisha mori wa kutaka mageuzi ya kiakili, kisiasa, kiuchumi, na kijamii kwa Watanzania na Taifa lao.
    Muda na shughuli zilitunyima nafasi ya kukaa na kuongea na kufanya mengi ambayo tulikuwa tumetarajia kuongea na kuyafanya.
    Sasa naomba niongee kama wanasiasa wa Tanzania " Mwisho ningependa kutoa shukurani zangu za dhati kwa zawadi za magazeti, kaseti, na cd ulizoniletea. Yaani kwa kweli umenikonga moyo vibaya sana. Kwenye disko langu la mwezi ujao wasikilizaji na wachezaji watapata burudani ya hali ya juu sana. Pili napenda kukupa pongezi za dhati kwa kufungua hii blog. Kwa jinsi ninavyokufahamu najua utakuja na mavitu ya hali ya juu. Tatu ningependa kukumbusha kwamba hii blog itaetembelewa na wengi kwa hiyo zile picha zetu tunazozipenda tafadhali ziwe za praiveti, humu uweke zile tu zenye manufaa kwa taifa kwa ujumla. Kwa hayo machache naomba niishie hapa. Kidumu chama cha wanablog? -kidumuuu!!!! Zidumu fikra za wanablog? Zidumuu!!! Asante sana, na safiri salama.
    Fidelis Tungaraza. Helsinki, Finland.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana brother Michizi kwa kuingia katika ulimwengu wa blogu. Nikiwa kama mwanablogu mmoja wapo nakukaribisha rasmi katika safari hii ndefu uliyoianza. Mara ya mwisho tulikutana pale Idara ya habari-Maelezo kule Tanzania kipindi hicho nikiwa kama mwandishi wa habari wa kujitegemea ambapo habari zangu zilikuwa zikitumiwa na kituo cha radio cha masafa ya kati 88.4 Clouds FM.kwa sasa naishi Cape Town, Afrika Kusini nikiwa katika safari ya kujikomboa katika dimbwi dhalimu la umaskini. Unaweza kutembea blogu yangu ya furahia.blogspot.com
    Namba yangu ni +27724696433

    Dennis Mponji

    ReplyDelete
  3. Muhidin,

    Ujumbe huu ndiyo niliyokutumia ulipotihimu mdau wa elfu tano. Nimenukuu aya ya mwisho ya ujumbe ambayo natumaini ilikuwa na bado ina mantiki hadi leo.

    "Tatu, ningependa kukumbusha kwamba hii blog itatembelewa na wengi kwa hiyo zile picha zetu tunazozipenda tafadhali ziwe za praiveti, humu uweke zile tu zenye manufaa kwa taifa kwa ujumla. Kwa hayo machache naomba niishie hapa. Kidumu chama cha wanablog? -kidumuuu!!!! Zidumu fikra za wanablog? Zidumuu!!! Asante sana, na safiri salama.
    Fidelis Tungaraza. Helsinki, Finland.."

    Ni miye maridhiya,

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...