wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao wamefanya kazi kubwa kuhakikisha bongo inakalika kwa amani na utulivu. kutoka shoto ni mkurugenzi wa usalama wa taifa cornel Apson, mkuu wa jeshi la polisi omar mahita na mkuu wa jeshi la wananchi generali george marwa waitara. hii ni kwa faida ya msiowafahamu watu hawa muhimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Nashukuru Michuzi yaani umetukumbuka kujua sura za hawa wanaochangia ujambazi na mauaji ya raia wasio nahatia Bongo kwa kile wanachosema kutunza amani na utulivu. Sura za wananchi wasio na nafasi zimelia na machozi hayatoki tena. Wakumbuke siku si nyingi nao watageukiwa maana malipo ya udhalimu ya hapa hapa duniani.

    ReplyDelete
  2. Michuzi, sina uhakika una maanisha nini unaposema "watu hawa muhimu". Umuhimu wa mtu unapimwa na mwelekeo wake kimaisha na utendaji wake mzuri wa kazi. na sio umaridadi wa mavazi. Watu hao uliotuonesha sisi walala hoi hatuuoni bado "umuhimu" wao wakati uuaji na ujambazi unaendelea mbele ya pua zao. Mbali na tuhuma mbali mbali wanazotupiwa jeshi la polisi sijaona mikakati yoyote ya maana iliyotolewa na hawa wakuu wa vyombo vya usalama kulikabili wimbi la uvunjaji mkali wa sheria (seriuos lawlessness). Ingelikuwa ni uwezo wangu ningewafukuzia mbali kazi hawa wote na kuanza na sahani safi. Ni mara mia bora kuliko kutokufanya chochote.

    ReplyDelete
  3. Huu mjadala mwingine ameuzua Michuzi. Sioni faida ya kuwakumbatia hao maana hakuna msafi katika hilo genge linaloonekana katika picha hii. Huyo wa Usalama wa Taifa sasa ndio anajipendekeza baada ya kujifanya Mungu kuwa yeye ndiye anaopanga nani awe Rais. Yuko wapi baada ya ambao hakuwataka kushika nchi na anafanya nini kujioondoa au anasubiri kuondolewa. Haya huyu mwingine aliyeshindwa kuhimili jeshi la polisi hadi kulifanya lishirikiane na wezi na manyang'anyi wauaji wala rushwa na wengineo naye aseme nini. Si muda wake wa kustaafu umeshakamilika anasubiri nini maana jitihada zake za kutaka ubunge ziligonga mwamba aende vakajaribu tena kugawa rushwa huko. Tumecho kuwa na wazungumzaji tunahitaji akina Lyatonga Mrema wasafishe nchi. Kama huyu Mrema aliweza kutoa ulinzi kwa raia hilo genge linashindwa nini. Siwafagilii kabisa ningeomba tu waondoshwe maana sioni na sitaonamchango wao kabisa na hili nitalisimamia. Kumbuka huyo mwingine wa jeshi la JWTZ sijamsema. Hivi kuwa na bajeti kubwa katika Ulinzi kulijko Elimu na Afya kunamaanisha kuwa na yeye anaongoza idara ya ulinzi kama wafanyavyo Marekani? Atwambie bajeti kubwa ya Ulinzi inatumikaje na Tanzania inapigana vita na nani au kule Zanzibar. Kuna mambo ningeongeza hapa lakini huu mwanzo nimechoka kusoma habari za watanzania wasio na hatia kufa na hayo majamaa kunenepeana tu bila kujua wanaopaswa kuwalinda ni maskini na wanahangaika. Kuna haja gani ya Polisi na mwanajeshi naye kulindwa? Au ni kuonyesha wasivyofuzu kujilinda wenyewe. Hao hili genge weote wana walinzi makwao kwa nini wasijilinde wao wenyewe au hao wanaowalinda hulinda mabinti na wake zao?

    Hizi ni hasira za moyoni na sizimalizi sasa.

    ReplyDelete
  4. Michuzi, mimi ni mpenzi mkubwa wa insha zako za taswira. Kwa kusifia kwa maneno ya kiingereza "Its ablotulety Genius". Na nahisia unafanya masihara (sarcasm), ulipoandika kwenye picha hii maneno yafuatayo.."wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao wamefanya kazi kubwa kuhakikisha bongo inakalika kwa amani na utulivu.". Aidha umevaa miwani ile ya upeo wa handaki (tunnel vision) au unafanywa kile ambacho muandishi yoyote mzuri anatakiwa akifanye...kustimulate discussions. Kwa vyoyote vile wananchi wengi maoni yao kuhusu utendaji kazi wa hawa jamaa ni kwamba UMEOZA. Maoni yangu mimi na wafanya biashara walalahoi wenzangu wote tunaovuja jasho kila siku hapa nyuma ya mitaa ya Msimbazi ni kwamba Fukuza kazi, weka ndani au shusha madaraka hawa watu. Haswa huyu mkuu wa polisi. Huwezi kumtuhumu mkuu wa polisi kwamba anashirikiana na majambazi halafu yeye akae tu asijitetee chochote.

    ReplyDelete
  5. Kumbuka kuwa kulinda watu ni tofauti na kulinda mbuzi.Basi tuwashukuru hata kwa hilo dogo walilofanya maana kama hujui amani basi uliza congo ya manyema na sudan na somalia ambayo hata sasa haina kiongozi na umeona wasomali wanavyo iba hata pasi za wabongo na kukamatwa nazo malawi.

    ReplyDelete
  6. Ndugu anonymous tunachozungumzia ni RESPONSIBILITIES. Huwezi ukakaa na kusema tu pointi hio kwamba "tuwashukuru hata kwa hilo dogo walofanya". Tunahitaji kuwajibika, Its only a matter of time Mandhari ya mitaa ya Dar itakuwa kama Mogadishu, watu watakuwa wanabeba magobole kwa kujilinda. Hawa wasomali unaowasema kwamba wamekutwa na pasi za Bongo ni mfano ambao nilikuwa nikupe wewe nikuonyeshe level of corruption ambayo viongozi hao wamezifungia macho. AMKA!

    ReplyDelete
  7. subuuuuuutuuuu kumshukuru nani? mbuzi? mimi nani ananishukuru? ZAMA HIZO SASA ZIMEKWISHA!!! wote tunajenga taifa kila mtu kwa nafasi yake.... ni nini maana ya hilo dogo wamefanya?? tumewaweka wafanya madogo au makubwa / ya kuridhisaha??? mbona mrema aliweza??? kauli hizi za kusema japo kidogo na kuwasemelea wenzio ndio zimelelea kansa ambayo ndio inataka kuanza kumyima JK usingizi!! mbona mimi / watanzania wengine wanafanya makubwa hawajapewa asante? lazima ifike mahali tutambue kuwa cheo ni dhamana unayopewa kwa niaba ya wengine (kwamba wote hatuwezi kuwa ma IGP na sio kuwa hatustahili) michuzi nani anampa asante kuibua mijadala humu ndani? hawa na watanzania wengine wanaofikiri kwa mrengo huo ndio wanadhani wana haki ya kula matunda ya uhuru bila kufanya kazi na kuwanyima au kuwaonea hata masikini / watanzania wenzao haki zao za msingi za kuishi wachilia mbali kujiendeleza...

    kwa ufupi hao vingunge wanahusika sana kudumaza maendeleo ya nchi yetu. wameanza hasa kwa kudumaza upinzani. wewe kama polisi ukienda ukakuta kuna ugomvi unashughulikia nini si chanzo cha ugomvi? polisi wanaenda unguja, wakakuta janjaweed / vijana wa kukodi wanapiga kura vituo si vyao unguja, wananchi wanakazana kulalamika janjaweed waondolewe wao wanaenda na kupiga wananchi...pumbafu kabisa wanamlinda nani???? kwanza kama kuua walianza siku nyingi si walimtandika masikini Kombe nyingi tu mbele ya familia wakidai ni mwizi wa magari??? - HILI HALIISHI LEO KWENYE HISTORIA YA tANZANIA. SHAME!! gharama yake ndio hiyo sasa zanzibar hakukaliki na maendeleo itakuwa ndoto!!! kwa kweli IGP wetu kuacha kufanya kazi zake na kuingilia mikondo ya siasa mie sina msamaha nae!!

    huko usalama ndio kabisaaaaaa wao adui wao mkubwa ni mwanasiasa wa upinzani..wao walitakiwa kuwa mbele kutoa ushauri unaojenga inchi na umoja sio kujenga chama fulani....hawa usalama wametufikisha mahali tunaficha kadi za vyama vyetu ili tusihusishwe na dhambi za chama chetu kutesa watanzania wenzetu??!! wanafanya nini wanakaa tu kuangalia chuki zinakua ndani ya nchi yetu siku hadi siku??? - ni kwanini mpaka ifike mahali JK aseme mtu akitaka kuenda CHADEMA mwache aende...kwa ujumla hawa ndio wanamfanyisha raisi wetu kazi za kiwaziri!!!

    kwa kweli tukirudi kwa jeshi siwezi kusema sana kwa sasa, lakini ni ukweli kuwa majeshi kwa nchi za wenzetu ni uwekezaji...labda sasa abadili jeshi lake liwe la wataalamu ambao watafanya kazi kama za ujenzi wa mahospitali kila kata.....lakini na kingine kwani Waitara si ni mkuu kwa Mahita au wako tofauti kabisa?

    ReplyDelete
  8. michuzi, nilisahau kukupa asante kwa kuzua mjadala. keep it up bwashe!

    ReplyDelete
  9. Mara ya kwanza wakati MICHUZI anabisha hodo kwenye blog,Ndesanjo alishindwa kufahamu mtazamo na mwelekeo wake katika huu uwanja.

    Mimi binafsi napenda picha zake sana ila maneno yanayoambatana nazo nathubutu kusema yananipa wasiwasi.

    Usalama gani anaozungumzia michuzi wakati watu wanakatishwa uhai kila siku kama kuku tena mchana kweupe na police wamejitosa katika kulitekeleza hilo!!!!!

    Mna habari kua police wanasema kiasi cha pesa walichokutwa nacho washukiwa ni Ml 5 wakati ndugu wa marehemu wanasema ni kiasi kikubwa cha pesa!!!!!Sasa zimekwenda wapi???

    Amri na tangazo alilotoa Waziri wa Usalama wa raia la kuwataka Police waue majambazi linapaswa kutekelezwa kwa umakini na hata ikibidi kutazamwa upya>

    ReplyDelete
  10. Duuh kuna Anti-CCM kibao amani na utulivu sio kazi ya polisi pekee yao basi hata raia wema na ndo maana huyo Mrema aliweza kufanya hayo yote kwa ushirikiano wa karibu na wananchi na hii ni PR ya mtu kuna wengine wanakaa ofisi kusubiri majibu wengine wanaingia uwanja wa vita kujua matokeo,sasa huwezi kuanza kutupa shutma tuu kwa akina Apson,Mahita na Waitara ila tuzipeleke kwa Ma OCD wanachapa usingizi wakati wananchi wanataabika.

    ReplyDelete
  11. Narudia tena mchango wangu hapo juu. Kuchapa usingizi kwa MA OCD ni kufeli kwa kuwajibika kwa wakubwa wao. Hatuwezi kusema kwamba viongozi hawa ni safi kwa sababu wanaovurunda ni watumishi wao. Viongozi wazuri ni lazima wajue kuhamasisha, wawe wawadilifu, waaminifu na wenye upeo mkubwa wa kutathmini hali halisi. Ningependa umsome mawazo ya Peter Drucker kwenye maswala ya Uongozi halafu upime viongozi hawa kama wanafaa au vipi.
    --Majaliwa
    Msimbazi Dar.

    ReplyDelete
  12. kuchapa usingizi??? nilipo pia ninafanya mengi kwa ajili ya taifa langu na labda nalala masaa manne kwa siku mbali na blanketi chapa mtu langu.....kama JK halali wewe unachapa usingizi kama nani? suala ni kupurura wote....na kuanza upya...hebu sogea pembeni kidogo labda kule ardhi...suala la kuuza kiwanja mara mbili mbili nalo utaliitaje??basi JK ni anti CCM? labda ndio maana mtandao ilibidi uwepo maana wengine waliishadhani nchi ni ya kuchapa usingizi!...HEKO WANAMTANDAO!!!

    suala lingine ambalo ni udhaifu wa utendaji wa serekali kulindwa kwa gharama zote kwa ile syndicate maarufu ya "umwenzetu" - je suala la mtu kulaumiwa kwa utendaji wake mbovu linahusiana nini na u anti CCM? je ni kweli kuwa CCM imeapa kulinda uovu? kumuwajibisha kigogo kunahusiana nini na kuwepo kwenye chama fulani? ndio maana watanzania wamejengwa kwenye dhana kuwa Seif asingeweza kufanya kazi vizuri zaidi kama raisi wa visiwa? mbona alikuwa tayari kuunda serekali ya umoja wa kitaifa angeshinda? - JE kuukumbatia upole wa mwalimu kubadilisha badala ya kufukuza walioharibu kwenye mashirika ya serekali ndio sera ya CCM kwa kuwa yeye alikuwa mwanachama namba moja? je tuendelee kuua bandari / uchumi yetu kwa kuwa utaratibu wa kizembe wa siku nyingi ulilelewa huko huko CCM??

    watanzania imefika mahali sasa tuache kuchukulia siasa kama mpira wa simba na yanga kwamba unashabikia tu hata kama kuna uozo. tunaosema maneno haya haina maana kuwa ni wapinzani.....inaweza kuwa ni muendelezo wa wanamtandao!!...hatutaki ifike mahali tushindwe kukiri imani za vyama vyetu kwa ajili ya wapumbavu wachache...imefikia mahali siasa inakuwa vita??? lazima tubadilike!kama ndugu yangu aliyesema ni uant CCM yeye yuko teyari kuona haki za wananchi zinavunjwa ili tu chama fulani kishinde, basi bado kazi ni kubwa!!

    ReplyDelete
  13. Elimu haina mwisho, nakushukuru majaliwa naendelea kujinoa ki public management na bwana Peter Drucker..mambo ya blogu hayo!!

    ReplyDelete
  14. Elimu ni uhuru(education is freedom)wananchi wengi hawajui haki zao,wananyanyaswa kila siku lakini hawajui wafanye nini.Ni jukumu letu kuwajulisha na kuwaelimisha.Pia tatizo kubwa jingine ni la viongozi wetu waliotajwa nina uhakika hawana kisomo,Apson alipomaliza darasa la nane amlienda uingereza kusoma akadai amepata Master Degree,darasa la nane anawezaje kutunukiwa masters? Mahita sidhani kama amewahi kuona chuo kikuu chochote labda chuo kikuu cha Polisi Kurasini.Sina uhakika na Waitara simjui.lakini kwa mantiki hiyo hao viongozi hawana elimu na kwa ulimwengu wa leo viongozi wasio na elimu unategemea ufanisi wao utakuwa je?Ndo maana maamuzi yao ni ya ajabu ajabu.Ninauhakika kuwa watu kama hao kwanza wanaongoza idara zao kwa upendeleo na kujirundikia watu wasio wasomi kwa hofu ya wasomi kuwa challenge.
    Ni wakati mwafaka wa kuliona hilo, na pia kutafuta mbinu za kuondoa Vihiyo hao madarakani ambao hawawezi na hawaendi na wakati.Pia
    viongozi wetu Makatibu wakuu wakuu wa idara ,mikoa na kadhalika wachunguzeni wengi wana vyeti bandia kutoka baraza la mitihani.

    ReplyDelete
  15. sasa hapo bwana anony unanirudisha kule nyuma kwenye dhana ya kubebana kuwa kubebana ndio huwa kunaua kanuni zilizonyooka za utendaji kazi. kuna bwana mmoja alisema ili nchi zetu zifanane na nchi za ukweli, inabidi tufike mahala tuwe na taasisi zinazosimama zenyewe bila kutegemea upepo wa siasa. hata hivyo, ni kweli bwana anony kuwa hata kama kanuni zipo ukijua kuwa cheo hakikustahili, umebebwa, unakuwa huna budi ya kuegemea kwa wakubwa kwani pia huna cheti au kanuni ambacho unapigania kukitetea. maana cheti mfano cha chuo kikuu hukipati tu kwa sababu umesoma na umefaulu, bali pia kama unafanana nacho kimaadili na kikanuni. ndio maana masenate ya vyuo yana uwezo wa kufuta cheti / kutokumpa mtu cheti.

    elimu ni uhuru. ni kweli kwamba kwa mtu aliyeelimika ni ngumu kuwa mtumwa wa mshahara...hivyo ni ngumu kwa asiyeelimika kujitegemea bila mshahara....

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 24, 2006

    Jukumu kubwa la kutokomeza ujambazi liko kwa wananchi wote siyo vyombo vya dola peke yake. jeshi la polisi ndilo lenye uwezo mkubwa wa kushirikisha wanachi na vyombo vingine vya dola kumaliza tatizo hilo. napenda kuwafunua macho wanaodhani kuwa usomi pekee ndiyo unaweza kuleta mageuzi katika vita dhidi ya ujambazi. Suala siyo usomi bali ni uzalendo wa dhati. Msomi anaweza asiwe mzalendo kama kwa asiyesoma. Cha msingi ni kuweka mtu mwenye sifa za usomi, uzalendo na anayekerwa na vitendo hivyo bila kujali maslahi binafsi. Vile vile usomi wa nadharia tu hautoshi tujifunze majukumu ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ili kutokuchanganya mambo kwani usilolijua ni sawa na usiku mnene wa giza totoro. Vita hivi vitakwisha tukiwa makini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...