kijana hashim ana urefu wa futi 7 na inchi 3 na akiwa na umri mdogo wa miaka 17 anaendelea kwenda juu. hivi sasa anasoma mombasa alikopewa skolaship na shule fulani baada ya kuonekana na timu yake ya basketbol ya vijana 'city bull' ilipoenda cheza mwaka juzi. hapa alitembelea ofisi zetu za daily news mtaa wa samora. nyuma yake ni masembe tambwe ambaye ni futi 6 inchi 4.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Huyu jamaa nilikutana nae huko Houston Texas. Anasoma huko na anatarijiwa kuwa future NBA star.

    ReplyDelete
  2. Tuko naye Houston sasa hivi, He's doin Big. High school yake ilikuwa Champion na alikuwa MVP (Kno what I'm talkin 'bout).

    ReplyDelete
  3. man huyu dogo ni big time! dogo anapiga kikapu kimuona unaweza ukasema ni mmarekani! kuanzia mavazi, tembea yake, alafu dogo anapiga kikapu(basketball) mimi nilienda kuangalia nilikua sijui dogo ni MTZ baada ya game akawa anasign outographs nikaenda pale nikamuuliza wewe ni mmareknani akasema MTZ nilifurahi kinoma! dogo unaambiwa hadi wamarekani wenyewe wanamuheshimu! wameshinda texas chamiponship alafu dogo mvp! hebu jamani niambieni uwe MVP wa basketball marekani! dogo ni big time! alafu ukiongea naye hana hata maringo nahamu waTZ maarufu mngeiga mfano wake! alafu yuko single! ukimuuliza maswali kuhusiana na nje ya Basketball anajibu so smart eh bwana michuzi fanya mpango uwasiliane na huyu dogo! e mail yake ni hasheemthabeet@hotmail.com! au mtumie namba yako ya simu atakupigia yaani dogo haringi mimi ndicho ninachompendea! eh bwana watanzania wote respect kwa Hasheem Thabeet dogo ataitangaza nchi yetu baada ya miaka miwili! mtumieni e mail mmsupport jamani e mail yake ndio hiyo hapo juu! hasheemthabeet@hotmail.com

    ReplyDelete
  4. duh huyu dogo namuonaga Houston, kabadilika ile mbaya utasema sio huyo hapo wa kwenye picha unaaambiwa watu wanamuheshimu kama bosi, ila haringi, jamani hivi masupa staa wa kibongo tungekuwa kama hyu dogo sijui Tz ingekuwa wapi! nashangaa eti watanzania wanaoishi naye hata hawamjali, yaani huku wamarekani wanampigia saluti ile mbaya, unaambiwa kila atakapoenda wamarekani wanamuweka VIP hata nilienda kwenye NBA game Houston Rockets ikiwa chini ya mtu mrefu kuliko wote NBA Yao ming walikuwa wanacheza dhidi ya Cleveland Cavaliers ikiongozwa na Kijana LeBron James nikamuona Hasheem kakaaa siti ya mbele kabisa na mastaa wa marekani akiwemo Vince Young mchezaji wa mwaka jana wa University of Texas nikaona duh huyu dogo akiamua kuringa itakuwaje? lakini cha kushangaza anaongea n waTZ kama kawaida, ni kweli kama alivyosema huyo jamaa hapo juu dogo anahitaji support!

    ReplyDelete
  5. duh michuzi si umtafute dogo akupe picha zake mpya hiyo picha nahisi mwenyewe akija kuiona na sehemu aliyopo sasa hivi hatojisikia vizuri! dogo mtu maarufu kiwanja mbadilishie hiyo picha kaka duh!

    ReplyDelete
  6. duh michuzi wewe unamsaidia vp huyu dogo na hiyo picha kama yupo mwanza kwa bibi yake!

    ReplyDelete
  7. million dollar kid! hasheem aka duh hata sijui nimfagilie vp huyu dogo! ni kipaji kipya! inabidi watanzania wote tufumbue macho kumpa ushauri na kumsaidia nini la kufanya ili dogo aipeperushe bendera yetu! jamani nani anammjua vizuri huyu dogo? kama unamjua hautakataliana na mimi kusikia nasmea kwamba dogo ni nyota inayokaribia kung'ara gizani! hebu jamani tuwe wakweli tu mmeshawahi kusikia Mtanzania anacheza mpira wa kikapu(basketball) marekani na ana dominate huo mchezo huko Marekani? duh huyu dogo ni kipaji! hasheem Big up sana! sisi mashabiki wako toka sauzi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...