jk akielekea kazini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. hii gari inacost kaa milioni mia mbili za kitanzania.
    kaa ile anayopanda chancellor angela markol.
    tutanataka raisi ajae atapande NYUMBU ,gari alisi ya kitanzania.

    ReplyDelete
  2. bwana anony umeongea jambo la msingi sana,yaani pato lenyewe la taifa kwa mwezi halizidi bilioni 200 kwa mwezi halafu rais anatumia gari kama ya cancelor wa ujerumani ambaye pato la nchi yake ni mara 200 yahili la kwetu,
    let be seriously kwanini asitumie landrover au zile mikonge ya wajapani ambayo inadumu kwa miaka 10,
    na hizo pesa nyingine tunanze kujenga chuokikuu kingine.

    ReplyDelete
  3. Naungana mkono na wachangiaji wa hapo juu kuhusu matumizi ya Taifa letu kwa ujumla.

    Lakini tukiangalia bwana JMK ni Rais wa nchi ambapo anatakiwa usafiri wake uwe wa kuaminika (Anga, Majini na ata barabarani).

    Cha Msingi hapa ni matumizi ya Serikali yaweze kudhibitiwa vizuri maana ule mtindo wa kuongeza zero mwisho wa namba upo mwingi ktk Afrika. Utakuta mfano kitu kinagharimu million moja basi itaongezwa sifuri na kuwa million Kumi. Sisemi kana kwamba hii ndio ilivyokuwa bali huo ndio ukweli ktk baadhi ya mambo.

    Kwa hivyo kama haya matumizi ya Serikali yakifuatiliwa kwa undani, rushwa kudhibitiwa, Kila Kiongozi na Raia akiweza kufanya kazi kwa bidii 365/24/7 na kuwa na uchungu na hili Taifa basi maendeleo yatakuwapo tu, na hivyo vyuo vikuu vitakuwepo vingi sana nchini Tanzania.

    Kwa mfano Pesa inayotokana na ushuru wa kodi (Pato la Taifa) na ile michango (Misaada) inayo toka nje ya nchi ingekuwa inatumika kwa sahihi kama vile ilivyo pangwa (Kutokana na Project husika) basi tungefika mbali siku nyingi lakini Utakuta kuna rushwa na uzembe kila kona ya Sekta iwe ya Serikali ama Binafsi hivyo pesa inatumika bila kufika yale malengo yaliyo pangwa na hii inajulikana lakini utakuta kuna Systems kubwa ambazo mtu mmoja hauwezi kuzisambaratisha na ata ukijitokeza utawakuta kila kona na kukusimamisha tu (wanalindana).

    Maendeleo ya Taifa hili yatakuja pale kila mwananchi akijiwekea mtindo wa kuamini rushwa ni mbaya iwe kutoa ama kupokea, pia kila raia kujua kila afanyalo matunda yake yatakuwa kwa wananchi na Taifa letu hivyo inabidi tufanye kazi kwa bidii kwa manufaa ya wote na kizazi kijacho, Pia kila raia aweze kupeleka watoto wetu mashuleni kupata elimu maana maendeleo ya Taifa yanakuja kwa kuwekeza kwa watoto wetu (If we ensure that Tanzanian children succeed in life, they will ensure that Tanzania succeeds in the world).

    Mwisho kuhusu gari la Rais naona ni sawa na muhimu maana ni imara na lina Bullet-proof na linamlinda Rais wa nchi.
    Marais wengi wana magari kama haya kwa usalama wa Viongozi wa nchi mfano bwana George Walker Bush ana hili gari Cadillac DTS soma kiundani hapa.

    Kwa ufupi tu ni muhimu kupunguza matumizi yale yasiyo ya lazima pia
    ni vizuri kwa Viongozi, Wananchi wote kufanya kazi kwa bidii ili tuweze kuongeza GDP na GNP kwa manufaa ya Raia na hili Taifa maana hivyo vitu viwili vikiongezeka basi na uchumi wetu utazidi kukua na wananchi wataona maendeleo na unafuu wa maisha.

    Kama Mataifa Mengine yameweza kufanya yale ambayo nimeyasema hapo juu na kupata maendeleo makubwa, basi na Sisi Tanzania tunaweza kufanya na Taifa letu kuwa na nguvu na lenye maendeleo.Yaani tupo nyuma kimaendeleo ata na South Africa!! Kweli wana-blog tunabidi wote tufanye kazi kwa bidii 365/24/7 na tuitokomeze rushwa na ata ikiwezekana kuwafundisha watoto ama jamii zetu kana ni mbaya.

    Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

    Nashukuru.
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  4. ukweli umebaki ukweli kaa jamaa alivyosema, Rais anatumia gari ya bei mbaya.
    hata Dubya naye anatembelea gari ya bei mbaya.

    ReplyDelete
  5. tusilaani huu ndio utamaduni.hamjui 'wabenzi'?

    ReplyDelete
  6. Samahani jamani, haya magari hajanunua Kikwete naomba nitoe bmaelezo kidogo kuhusu matukio makubwa kabisa aliyofanya Mkapa kabla ya kuondoka ofisini.
    1. Kununua Rada
    2. Kununua dege
    3. Kukarabati Ikulu
    4. Kununua mabenzi ambayo yalisemwa yatawezwa kukodishwa.
    5.Kubinafsisha kila ambacho hakujenga.
    6.nk nk nk

    ReplyDelete
  7. nyinyi watu hebu acheni ujinga wenu hamna hata aibu wakubwa wazima kuandika vitu visivyo na maana hivi mnataka Raisi wenu apande gari gani? hiyo gari mnaiona ya maana sana? eti raisi apande nyumbu wewe unaijua nyumbu wewe? kama hamna hoja hebu msiandike kitu au andikeni vitu vinavyosomeka!!.

    ReplyDelete
  8. Anonymous acha jaziba, hapa ni kubadilishana mawazo na siku zote watu hatupo perfect.

    Kuna wengine watatoa ushauri mzuri na wengine mbaya sasa usiwajumuishe wote kingine na waho wana haki ya kusema lolote lile maana this is free world.

    Waache waseme waliyo nayo moyoni.Kingine kutukanana sio ustaharabu.Naona utaona umekosea kuwatukana wapuuzi na waombe radhi.

    This is free world.

    Bujiku aka the pretender

    ReplyDelete
  9. hii inaonyesha jinsi rais mstaafu asivyokuwa mbinafsi.rada ni kitu muhimu sana, ndege nayo muhimu sana, na hata kukarabati ikulu.
    aliweka mazingira mazuri kwa JK.
    hata tumeona JK kawaalika totoz (mamisi) mle kutembea.
    ndege yenyewe hata yeye ajaitumia ipasavyo kama rais, anaitumia JK sasa.
    kama nyumbu inegekuwa gari madhubuti na zipo saluni nyumbu, ingekuwa vizuri sana rais angetumia gari la kitanzania.
    Mkapa amejitahidi sana, hilo mtalikubali baada ya miaka 10 kupita kama ilivyo desturi yetu.
    hata wakati mwalimu anastaafu ni wachache sana walikuwa wanampenda, ila baada ya miaka 5 kupita,, kila mtu akamuita Baba wa taifa kwa heshima zote.jamjuah

    ReplyDelete
  10. sasa rada inakusaidia nini wewe,
    hivi watanzania mmelogwa na nani?
    yaani mtu unaona kabisha kwa mcho yako ubadhirifu wa pesa,halafu bado mijitu bado inasifia tu,alaa!
    huu ni ubadhirifu wa pesa,kuna magari ya bei nafuu na yanadumu,ndio tunategemea rais na viongozi wake wawe mfano kwa kutumia magari ya bei nafuu, na kuweka kipaumbele kwenye elimu,afya,maji nishati ya umeme nk
    sasa hebu fikiria rais awe na hili na makamu wa rais naye,na rais wa zanzibar na waziri mkuu,halafu uje mashangingi ya mawaziri,makatibu wa wizara,wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,loh!
    hizo gharama za service ya haya magari + mafuta + allowances ,
    unategemea yule mwananchi wa ilolanguru tabora atapata barabara lini?

    ReplyDelete
  11. mie narudi kwa huyu bwana JK... sioni cha ajabu sana kusafiria hako kagari...maana ni benzi kama nyengine tu kama walizo nazo kina sir nature sana sana kama ni gharama zilizoongezeka ni hizo ficha za kiulinzi e.g. bullet proof, jambo ambalo kimsingi lipo chini ya mamlaka za ulinzi katika taasisi ya uraisi...

    ni vizuri mjadala wa bw. Michuzi umeanzisha mjadala wa matumizi mbadala wa resources za serekali, ambao ni wa msingi sana sana....lakini pia labda ni vema akasafiria hako kamkweche ili asishindwe kutenda majukumu yake kisa mgongo unamuuma - maana kama kawaida wabongo hatutaacha kupiga kelele na kuzusha kuwa sababu ya kujirusha na totoz kwa sana...wakenya wana wasiwasi kuwa Kibaki tangu alipata ile ajali wakati wa kampeni ndio akaanza kufanana na raisi zezeta...akawa sio Kibaki waliyemzoea kabla...tumwonee huruma JK naye kazaliwa na mwanamke kama sisi!

    ila ni kweli ukiachilia mbali usafiri wa raisi (kama ndiye chaguo letu) baada ya hapo kuna haja ya kudhibiti matumizi mengine na hasa usafiri huku chini...kuna kuongelea suala alilolipua ulimwengu kuwa waziri akienda safari idara zooote chini yake zinampa bahasha ya mshiko kama allowance(rushwa)...kuna kuongelea suala la PCB walionyimwa meno siku nyingi sasa hivi hakuna kulala kupekua mafaili - meno yameota...na mengine mengi...kuna rushwa mathalani kule ardhi ambazo ukizijumlisha zooote kitaifa kwa siku moja labda zinafanana value na hako kamkweche ka JK..ambazo zilikuwa zinatoka kwa walalahoi kwenda kwa watu muhimu wa wizara...ni vema tukatanua mjadala huu wa matumizi mbadala wa rasilimali zetu....aksante michuzi!

    kaka MK Tanzania ilipo sasa hivi si ya kulinganishwa na Afrika Kusini (siku nyengine sema taratibu watu wasikusikie)....hawa jamaa wametuacha mbali saaaaaana.......Sauzi ni ulaya ndani ya Afrika....sana sana bongo tunaweza kupambanishwa na Uganda, Malawi, Msumbiji na maeneo kama hayo...kama uko kiwanja siku ukiweza tua SA nakuhakikishia utatoa machozi utapogundua jinsi tumetofautia nao...

    ReplyDelete
  12. Mark Msaki ni kwamba nimefika South Africa.Pia sababu zangu za kusema tupo nyuma zinatokana ya kwamba hao ndugu zetu ni juzi juzi wametoka ktk matatizo ya nchi kwa ubaguzi wa rangi na machafuko mbali mbali sasa ata kama wangekuwa wamerithi utajiri gani toka kwa hao wazungu (Serikali iliyopita) ni kitu cha kuiga kuona ya kwamba watu wamesahau na kufanya kazi kwa bidii na kuweza kukaribisha wawekezaji walio serious wenye Capital za maana toka dunia nzima kuwekeza ktk nchi yao.

    Maana kama wananchi hawafanyi kazi unadhani uchumi wa nchi utakua? Pato la Taifa litatoka wapi? Au utabaki kukopa kukopa? Mwisho nchi inabaki na madeni makubwa tunayo shindwa kuyalipa? Au ndio uta-over spending na mwisho utabaki na budget deficit? Ni hali mbaya ki-uchumi kubaki na Budget deficit!

    Sisemi watanzania hawafanyi kazi bali speed ya kufanya kazi nchini ni ndogo sana ambapo bado tunategemea kilimo tu ktk uchumi wetu! Wenzetu wanategemea viwanda,Utalii, Kilimo, Uvuvi, Uuuzaji wa wine, na vyanzo vingi vingine wanategemea!

    Tanzania ina idadi kubwa ya watu wasio fanya kazi sasa hii nguvu kwanini tunaipoteza? Wengine wana ujuzi wao! Kwanini tunapoteza pesa kumsomesha kijana na mwisho hana kazi? Kingine kuna idadi kubwa ya watu hawana ujuzi wowote ule! Kwanini tunapoteza hii nguvu ambayo ingetumika kuongeza uchumi wa Taifa!!

    Nchi inapimwa kwa vitu vingi, Jinsi gani idadi ya watu kujua kusoma na kuandika (wanapeleka watoto wao kusoma na sio kuishia darasa la saba au form four au six bali wanafika mbali) na ata kama familia hazina pesa lakini kuna vyanzo vingi vinavyotoa mikopo kuwezesha familia kupeleka watoto kusoma.Na hapo utakuta nchi wame-inverst wasomi wengi wenye elimu ya hali ya juu.

    Kipimo kingine ni Idadi ya watu kufa wakiwa watoto ktk kuzaliwa, ata wakiwa wakubwa. Magonjwa madogo madogo kuwa mengi, n.k

    Mfano mwingine Jiulize ni kwanini Nurse au mtahalamu yoyote toka Tanzania akifika UK au nchi nyingi za Ulaya ni lazima afanye adoption ili haweze kufanya kazi na kwanini wa-South Africa hawafanyi adoption? Ni kwasababu nyingi tu kwa elimu yao kuwa ya hali ya juu na kingine ni lugha!!

    Tanzania tumepata uhuru lini? Ni siku nyingi sana lakini tumeshindwa kuwekeza kwa muda wote huo!! Ni kwasababu ya wizi wa Viongozi na wananchi kuchukua rushwa na kujilimbikizia mali kibao na kuwa na account za mamilion ya pesa kila kona ya dunia! Kama Taifa lenye kupata huo uhuru siku nyingi na Kingine ni nchi yenye Amani sana basi tungelingana angalau na South Africa maana tuna kila vyanzo kuwezesha Taifa kulingana na hii nchi na kama Serikali na wananchi hawaweki targets unadhani ni nani atakuja kukuokoa na huu umasikini ambapo tutabaki kujilinganisha na Uganda, Malawi, Msumbiji ambazo ni nchi masikini na nyingi zilikuwa na Vita na Uganda bado wana vita na LRA. Kweli ni haibu tupu.

    Jiulize ni kwanini viwanda mali ya Serikali vimeshindwa kuendelea? Ambapo vingekuwa ndio work force wa uchumi wetu!! Lakini vinauzwa kwa bei rahisi na ya kutupa!!
    Tuna migodi mingapi Tanzania ya madini ya kila aina tunapata faida gani kuliko huyo mtu aliyenunua hii migodi kwa bei rahisi na ya kutupa? Angalia South Africa wana migodi mingi na hawataki mchezo nchi inapata pesa toka kwa wawekezaji na kupitia kodi na pia wananchi wanasikia unafuu wa maisha kutokana na hao wawekezaji!! Jiulize ndani ya Tanzania yule mwananchi aliye karibu na migodi anasikiaje unafuu wa maisha? Si ndio kila siku hana pesa ata ya kula!!

    Ebu angalia hii aibu South Africa wamepata uhuru juzi lakini GDP yao ipo juu zaidi ya Tanzania nchi iliyopata uhuru decades nyingi zilizopita.

    Sasa kufanya kazi kwa bidii 365/24/7, kuweka targets za maana, matumizi ya Serikali kuangaliwa, wananchi kupeleka watoto kusoma, Kuacha rushwa na wizi kwa Viongozi na wananchi kutasababisha nchi kuendelea na kufanikiwa.Kingine ebu jamani tuchukue advantage ya kuwa nchi yenye amani na kuweza kuita serious investors kuwekeza nchini kwetu na pia tufanye kazi kwa bidii.Tukiulizwa kwanini Tanzania wa wananchi wake ni masikini utajibu nini cha kujitetea? Utasingizia nini? Angalia mataifa mengine ya Africa watasingizia Vita!! Sasa je wewe na mimi tutasema nini? Naomba majibu!!

    Na sio kujilinganisha Tanzania na Uganda ambayo wana matatizo ya Vita vya LRA na matatizo kibao.

    Kwa Tanzania kupata uhuru siku nyingi tungekuwa mbali sana tena mbali sana zaidi ya South Africa.

    Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  13. M.K. nimekuamini kwa pointi ulizoangusha hapo juu. ni mawazo mazuri ambayo kila mtanzania angejiuliza tungeishafika mbali sana.... kama watu wanakataa kuwambiwa mana kuna haja ya kuanza kuchapa watu viboko sasa. ebu ona kuna wapumbavu wameishaanza kupigia kelele ultimatum za Lowassa....na hakuna kulegeza buti mwendo huo huo....

    ni kweli na ni aibu utakuta watu wanashinda vijiweni toka asubuhi hadi jioni wana bishana Yesu na Mohamad SAW nani zaidi, jioni wanarudisha timu nyumbani na wanakuta msosi vile vile....inabidi mazingira yabane mpaka ifike muda hata siku ukiumwa tu hakuna msosi...hapa utandawazi utatubiga viboko....

    tatizo ni kwamba kwa miaka mingi watu wenye mawazo kama yako walikuwa hawaruhusiwi kuwa na sauti (kutilia vitumbua mchanga).. ni Mungu alitukumbuka watanzania akamcholopoa Jk huko alikokuwa amefichwa... Jambo la kwanza la muhimu kabisa ni kushikishana adabu, kazi wameianza vizuri...tuongeze nguvu , I am optimistic kuwa tutafika...halafu tusikubali kurudi nyuma kuwa na maraisi wanaoendekeza libeneke...tunatakiwa tuanze kuwapanga sasa...bada ya Jk , Ngoyai, halafu Joni Pombe, labda baada ya hapo hata wewe bwana M.K unaweza ukafuatia....

    viva Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...