tumshereheshe shujaa samson ramadhani mshindi wa mbio za marathon 2006 huko melbrourne

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. wewe shujaa kweli, tunakusaluti. umepepea bendera yetu kati ya mataifa. umeitangaza nchi yetu,, hawa ndio wanasaidia kuitangaza nchi yetu, tuwape kipaumbele zaidi na zaidi, na sio kukazania mamisi, hii picha imeonekana kwenye all major TV news across the world.hongera Samson Ramadani!

    ReplyDelete
  2. Naunga mkono maoni ya anony hapo juu.Mambo ya UMISS hayatusaidii,mambo kama haya ya Ramadhan ndio role-model kwa taifa la kesho.
    Hongera sana bwana, nilifurahi sana.

    ReplyDelete
  3. wewe innocent nani kasema mambo ya mamiss hayatusaidii. Over 1 billion people watched Mamiss juzi kutokea ubungo plaza. Matunda tutaanza kuyaona mwaka huu. Zimbabwe pamoja na matatizo mwaka jana wali host haya mashindano ya miss tourism na tourism industry yao ilikuwa by 25%. Hii yote ni kwa sababu watu wanafikiri mambo ya mamiss ni ya kihuni, welcome to the new generation which is now taking over. Also hongera samson for representing.

    ReplyDelete
  4. fainali za kombe la dunia ndio wanafika watazamaji bilioni.
    hatujui hayo mashindano ya mamisi yalionyeshwa live kwenye chanel gani?
    mashindano ya mamisi sio uhuni hata kidogo, ila ni dalili za ukware.
    shujaaa samson anapeperusha bendera ndani ya OZ na dunia nzima wanamuona.

    ReplyDelete
  5. mzee anon, mimi nilikuwa sijui kama haya mashindano yalikuwepo mpaka nilivyoona hii picha.Mimi naishi seattle na nakwambia niliangalia live kutoka kwenye dish mashindano ya miss tourism bongo. tulikuwa kama watu 25, wengine wote ni wazungu. Na ikaniuma sana pale waliponiuliza kama mlima kilimanjaro na serengeti national park ziko kenya au tanzania,kwa sababu walikuwa wanajua ziko Kenya before the competition. my point ni kwamba kuna so many different ways za kupromote nchi. Hongera tena samson

    ReplyDelete
  6. Heshima na pongezi kwa huyu bwana.Kwa kipindi kirefu sana nilikuwa sijasikia jina la nchi yangu litajwe kwenye vyombo vya habari vya hapa mpaka majuzi medali ya dhahabu ilipotwaliwa na huyu bwana.Hongera sana.

    ReplyDelete
  7. Hukujua kwa sababu hukuwa na interest na mashindano yenyewe siyo kwa sababu yanazidiwa na miss tourism. Hii habari ya kusema Mlima Kilimanjaro sijui Serengeti viko Kenya ni hadithi za mwaka arobaini na saba. Leo hii katika ulimwengu wa mtandao na atashindwa kujua nini kipo wapi? Hao Wazungu wako wazushi hawana lolote. Tutaelewana kama utasema hawajawahi kusikia kuhusu hivyo vitu viwili. Lakini pia hata wasipojua nini cha ajabu? Wewe uliyeko Seattle ukiulizwa mji wa Topeka uko State gani si ajabu ukajiumauma.
    Tuache visingizio, tutengeneze Mahoteli ya kitalii, barabara n.k watalii watakuja tu, siyo kusingizia eti hawaji kwa sababu hawajui vivutio viko nchi gani. Hawa watu wana akili, kabla hawajatoka nchini mwao hufanya research babu kubwa kuhusu waendako. Mtu ambaye hajui nini kiko wapi hana cha kufanya na hicho kitu. "A person who asks the price of a yatch has no business owning one." J.P Morgan Sr.

    ReplyDelete
  8. mzee anon, you will be suprised watu wanakwambia wanaenda kupanda mlima kilimajaro kenya. hata kuna wa africa amboa nasoma nao majuzi tu ndiyo wamekuja kugundua kwamba mlima kilimanjaro upo tz. You'll be suprised man

    ReplyDelete
  9. mpanda/mpenda milima yetote anajua geografia na historia za milima.
    swala ni kwamba kuna watu wengi duniani hawajui hata kilimanjaro ni kitu gani.
    ila samson kuzunguka ule uwanja na bendera yetu,wengi walikumbuka hee! "Tanzania" hee!,wengi kwenye tv majumbani walikumbuka atlasi zao.
    hata yule commonteta alizungumza mengi sana kuhusu Tanzania wakati jamaa alipokuwa anafukuzana na yule mkenya.nilisikia mengi kuhusu nchi yangu hata mimi(MTZ)mwenyewe sikuwa na yajua, kwahiyo hii yote ni credit kwetu. jamjuah

    ReplyDelete
  10. Vipaji vya namna hii vinabidi viendelezwe nchini kwetu. Jamaa ametutoa aibu na kufanikiwa kupata gold ktk haya mashindano ktk muda wa 2:11:29 soma hapa.

    Serikali na wadau wengine wengeliona hili swala na kuweza ku-support vijana wa namna hii basi tungekuwa mstari wa mbele ktk michezo, Wenzetu unaona wamefanikiwa na kupata medal nyingi ni kutokana wanaandaa vijana wao ktk haya mashindano na mengine zaidi ktk muda mrefu toka wakiwa vijana (wadogo).

    Hii ni moja ya ajira maana wengi wanatajilika kutokana na huu mchezo maana licha ya Gold medal kuna zawadi nyingi mshindi upata na mashindano mengine utoa pesa.
    Sasa tukiwapatia Vijana wengi mafunzo na kuweza kuwa-sponsor basi tutaweza kuondoa idadi ya watu wasiokuwa na ajira.

    Kwa ujumla michezo yote ya aina yoyote ni ajira kwa Vijana ktk hii dunia.Tuweze kuwasaidia watanzania wengi tokea wadogo.

    Ongera Samson Nyonyi Ramadhani kwa ushindi uliopata na uzidi kushiriki mashindano mengi kuwakilisha Taifa na wananchi wa hili Taifa.Pia itazidi kukupatia kipato hasa hasa yale mashindano ya Manchester yanatoa pesa nzuri sana.

    Picha zaidi za Samson Nyonyi Ramadhani bonyeza hapa.

    Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  11. Well said MK

    ReplyDelete
  12. Mimi binafsi maadili ya kupitisha wanawake na vichupi mbele ya kadamnasi ili waamuzi waseme nani mzuri zaidi sikubaliani nayo. Haya ni mawazo yangu binafsi. Pia kitendo cha uzuri huo kuwa unatokana na vigezo vya utamaduni wa upande mmoja wakati dunia yetu ina vigezo tofauti vya uzuri kutokana na tamaduni mbalimbali sikiungi mkono. Pia mantiki ya kufanya mwili wa mwanamke kama chombo cha maonyesho na biashara sikubaliana nayo. Hii ni kinyume na falsafa na mtazamo wangu.

    Kingine ni tabia ya nchi kuamini kuwa nchi inaweza kutangazwa vyema kwa mashindano ya siku moja na kutumia muda mwingi na fedha nyingi katika mashindano hayo. Ukiacha nchi zinazojulikana kwa vita, tafuta nchi zinazojulikana na kuheshimika duniani zimefikia hapo zilipo kwasababu ipi. Ukikutana na nchi ambayo inaheshimika, inafahamika, inasikilizwa katika vikao vya kidunia,n.k. kwakuwa eti inazalisha "ma-miss world" na "ma-miss universe" niambieni. Nielimisheni hapo.

    Nielimisheni kama kuna nchi iliyopiga hatua kijamii na kiuchumi ambayo kati ya sababu za nchi hiyo kupiga hatua ni kuwa imewahi kutoa "ma-miss" hiki au kile.

    Samsoni anahitaji kupongezwa. Dakika chache kabla hajashinda niliulizwa na mtu,"hivi kwanini wakenya huwa wanashinda mbio ndefu?" Kabla sijamaliza kujibu Samsoni alikuwa akifanya vitu vyake. Mtazame hapo na bendera yetu...ananikumbusha enzi za akina Nyambui, Ikangaa, Bayi, n.k.

    ReplyDelete
  13. nakubaliana na ndesanjo mambo mengi.
    mashindano mamisi katika nchi nyingi ni kwa ajili ya wasichana wadogo. hata wanafuatilia sana ktk nchi nyingi ni wasichana wadogo.
    na hata ukimuuliza mtu hapa mitaani, miss world ni nani?,katokea wapi? watu wachache sana watajua jibu.ni kwamba kuwa miss sio kuwa supermodel,kama(naomi, imani, wek alek) kuna tofauti kubwa.
    hii biashara ya umisi sio kubwa sana nje ya Tanzania kama wengi wanavyofikiri.
    kama tunapenda sifa na kujulikana na Tanzania kiwa familia kwenye midomo ya waghaibu,njia raisi ni kukazania michezo, na kuwapa msaada, kipaumbele mashujaa kama samson.
    Tuwaone kwenye front page za magazeti na tv zetu mara kwa mara,hii itasaidia kuwahamasisha vijana wengi.jamjuah

    ReplyDelete
  14. Hivi mbona wakina Ikaanga, Bayi nk walikuwa wanashinda hizo mbio na kuitangaza nchi, lakini hali ya tanzania iko pale pale?

    ReplyDelete
  15. michezo ni ajira.ikangaa na bayi wamenufaika sana na michezo hata wao binafsi.
    hata leo watanzania tunawafurahi hao magoldi medalisti wetu.
    wana tambula na bodi kuu za michezo kama IOC,nk,nk.kumbuka wanamichezo sio wapanga mbinu za maendeleo.hiyo ni kazi wanasiasa.

    nchi nyingi za africa hasa magharibi zina wanamichzo wengi wanaolipwa mpaka 3million dolla kwa mwaka,kutokana na michezo tafauti tafauti.Tanzania hatuna hata mmoja,inasikitisha sana.
    mafano patric viera, mzaliwa wa senegal mchezaji wa mpira anajenga football academy senegal.japokuwa ni raia wa france kwa sasa.hiko mifano mingi sana, Nwako Kanu anayo hospitali kubwa ya magonjwa ya moyo kwao nigeria.

    tukiwatumia vizuri mamedalisti kama hao, tutapata wanamichezo wengi bora, kama kina maria mutola,gabriel selasie, na hata kina michael johnson wa kitanzania.
    jamani ari mpya nguvu mpya! jamjuah

    ReplyDelete
  16. nimekuelewa mheshimiwa.

    ReplyDelete
  17. Furaha kwa wantanzania, Mtanzania wa pili kupata medal ktk mashindano ya commonwealth ni ndugu JOSEPH NAASI Fabian ambaye ameshinda mbio za 10,000M leo hii 25/03/2006 na kuwa mshindi wa tatu na kupata medal ya Bronze.

    Habari kamili bonyenza hapa .

    Idadi ya watanzania kupata medal bonyenza hapa

    Ongera Samson Nyonyi Ramadhani na Fabian Joseph Naasi.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  18. suala baada ya hapo ni je, medali hizo zina msaada gani kwa taifa letu? si tunarudi pale pale kwenye kutangaza taifa? kwangu mimi sioni tafauti yoyote kati ya umiss na ukimbiaji. vyote ni muhimu na vya kuendelezwa. mimi sio shabiki sana wa mpira, lakini siko kipofu kuelewa umuhimu na nguvu ya mpira katika kujenga uchumi na kuzungusha hela. suala lengine ni je, Tanzania tumeweza kufanya michezo yetu kuwa proffession - ili isaidie kupunguza tatizo la ajira? maana pia kama hilo nalo halipo, sioni sababu kumshikia kidedea mwanangu apoteze muda wake kuwa mkimbiaji....eti anajenga afya!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...