mtimkubwa upo? mbona kimya? haya, nakuchokoza sasa!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Huyu ni baba Patrice Lumumba, mzee wa kazi ambaye majasusi wa serikali inayodai kuwa kinara wa demokrasia dunia (yaani CIA) na makacheroa wa Kibelgiji walimwogopa kama sijui nini. Na hatimaye kula njama iliyokuja kuondoa uhai wake. Alikuwa anapenda sana kuhutubia kwa kiswahili kile cha Kongo.

    ReplyDelete
  2. mabeberu walimua kwasababu ya uranium. uranium ya kutoka congo ndio ilitoa atomiki bomu la hiroshima. alikuwa na mtazamo wa kimashariki(soviet).
    na ndicho kilichomua laurent kabila.aliwapa dili north korea.na ndio hakakosa sapoti na kuchuniwa na hata bongo. jamjam

    ReplyDelete
  3. Nakumbuka moja ya kauli zake za mwisho kuwa 'Kasavubu ananila njama, najua nitauawa; iwapo nitauawa, amani haitapatikana Kongo' - Patrice Rumumba.

    Londo

    ReplyDelete
  4. Lumumba ni wale viongozi wanaojua kuwa watauawa kutokana na misimamo yao kuendana kinyume na maslahi ya mabeberu lakini hawabadili misimamo yao.

    ReplyDelete
  5. Nakumbuka mwaka jana au mwaka juzi ilitengenezwa programu maalum ya televisheni kuhusu Bw. Patrick Lumumba na ilikuwaje akauawa.

    Je kuna mtu anaweza akanielekeza niwapi naweza kuipata wapi video au DVD ya programu hiyo?

    Natanguliza shukrani za dhati.

    ReplyDelete
  6. Muhidin,

    Nipo. Lakini nipo bize kupita JK na mweziye Mbowe miezi michache iliyopita! Nimo harakatini najenga blog yangu! Siri usimwambie mtu mpaka itakapokuwa tayari, kutakuwa na migoma humo mpaka watakoma.

    Maalim, utafikiri mchawi! Jana nilikuwa natazama DWTV wakawa wameweka focus in Congo kufuatia uchaguzi mkuu wa Kongo utakaofanyika mwezi Juni mwaka huu. Tuombe kheri uchaguzi wao uende vizuri ili Kongo nayo ipumzike dhahama.

    Nimepata kutazama dokcumentaries kadhaa kuhusu mauaji ya Hayati Lumumba na ujio madarakani wa Mobutu Sese Seko. Kwa kifupi ni vifo vya Lumumba, Nkrumah, Tombalibaye, Olympio, na wengineo wa kariba yao vinatukumbusha njama za mabeberu wasiolala usiku na mchana katika kulinda masilahi yao ya kibeberu.

    Aluta continua,

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  7. nkurumah alikufa mwenyewe kwa kansa.

    ReplyDelete
  8. Tungaraza karibu kabla hujapiga hodi. Sie tunaopata mambo mengi mapya kutoka kwako huwa tunakumiss unapoteleza kinyemela. hata hivyo pole na kazi zako zinazokuweka bize kuliko JK na Mbowe.

    ReplyDelete
  9. Enzi zake naona mikorogo kwa wazaire ilikuwa bado.

    ReplyDelete
  10. anonymous said..........
    Mzee Lumumba wa Kongo tunakulia.mabeberu wamemuondoa dunianijuu ya yakugombea uhuru.Wazee Nyerere,Lumumba;Nkrumah tuna wa miss.Mungelikua uhai,kama wa Afrika hatuteswe ivi............

    ReplyDelete
  11. Mwenyezi Mungu Amulazi pahali pema!Hatuna mengi ya kusema jaami kwani makatili hao hawajaondoka, lakini sisi watu wa kiafrika ni lazima tukimuona mzungu tukumbuke kwamba ukatili wao haujaisha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...