jk kamchagua isaack mruma kuwa bosi mpya wa deliniuzi kuanzia alhamisi ilopita

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2006

    Michuzi tuwekee na mkurugenzi mpya wa redio uhuru tafadhali

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2006

    MICHUZI ,HUYU NDIYE ALIYEIDHINISHA TRIP?BANANA NAYE KISAWASAWA!USICHEZE MBALI NA CHOO!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2006

    Bado tunakumbatia Wazee mno nilitegemea vijana kama akina Michuzi wapewe nafasi kama hizi. Sijui vijana bado tunaendelea kuwa taifa la kesho.Huyu si kwenye miaka 59 hivi au 60 na kuendelea. Weka vijana wafanye vitu kwa spidi, kasi na nguvu mpya.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 22, 2006

    Mizee mizee tu bado inaendelea kupata vyeo, hapa tumeliwa hakuna jipya wala nini? sasa kwa hili naanza kuwa na wasiwasi, tunaitaji watu wenye mawazo mapya huyu mzee mikakati mipya ya kuendeleza kampuni apate wapi. Michuzi tunahitaji kuwaelimisha watanzania. JK uwaziri sawa lakini ukurugenzi siyo siasa hata kama ana elimu gani muda wake umeisha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 22, 2006

    Huyu ni kada wa chama tawala na ni mmoja kati ya Vingunge wa Itikadi ya Chairman Mao Tsetung katika kufanya vyombo vya habari kutumikia System.Hapo hata mzee Yusuf Halimoja kasingiziwa katika kujua mambo ya siasa za nchi hii. Nadhani ni ushauri wa Comrade Kingunge.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 22, 2006

    Kama Mheshimiwa KIkwete ni 55 na mnasema ni kijana sasa kuna ubaya gani akimtueua kijana mwenzake wa miaka 60?

    Lakini jamani tuwe realistiki, hawa wazee woote kweli hamuwataki wafanye kazi? Mimi naona bado wazee wanahitajika kwani busara zao na experiensi zao inabidi wawaoneshe vijana. Kwahiyo kinachotakiwa ni miksicha nzuri kati wazee wachapakazi na vijana wachapakazi wafanye kazi kwa pamoja.

    Kazi ya vijana ni kuleta aidia mpya na kazi ya wazee ni kurefaini na kuziboresha aidia hizo. sio kuzitia kapuni.

    Mimi hapa ni kijana lakini kila nikikwama huwa naongea na baba yangu ambaye ana miaka 75 na kila mara niliyooongea naye hajashindwa kunisaidia. Kwa maana hiyo basi hata serikalini wanatakiwa wazee wawepo ili wawasaidie vijana kuchapa kazi vizuri.

    Mimi sioni aibu kusema kuwa na kombinesheni ya vijana na wazee.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2006

    Anony wa 11:51 Pm tangu tupate uhuru Tz imeongozwa na wazee kibao sehemu nyingi wametufikisha wapi? Wazee wazidi kuturotisha watuachie sasa na sisi vijana waone moto wa maendeleo. Wazee tangu uhuru mpaka leo tunarudi nyuma tu nchi kama China, Japana, Korea nk tulikuwa wote sasa wapo wapi. Jamani wazee tuachieni nchi yetu vijana na sisi tujaribu maana nyie mmeshashindwa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2006

    Anony wa 11.51PM umenifurahisha sana umegusia maswala ya msingi lakini kuna kitu kimoja ambacho umesema jinsi unavyomfuata baba yako. Sasa huu siyo executive chief, umesema baba yako anakushauri(kama kingunge). Kuna vitu viwili hata mtu kukushauri na kuwa yeye ndio kila kitu, wazee ni wazuri kutushauri pale tunapokwama (wameona mengi), lakini siyo wa kututoa sehemu moja kwenda nyingine. Tembelea/au tuwaulize wenzetu walioko nchi zilizoendelea utaona aibu makampuni unayosikia yanakimbia ulimwenguni siyo wazee ni vijana sijui wewe una umri gani lakini hapa namaanisha vijana wa 30-35-40(sema wenzetu wanapandisha haraka) huwezi kuamini.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2006

    Anon 10:07 na Grill,
    Mimi anony 11:51 niko 30's lakini bado ninapenda kufanya kazi na wazee,wazee bado ni muhimu. Maoni yangu ni kwamba kuwe na balance ya wazee na vijana na kila kundi liwe openi kwa input ya kundi lingine, yaani kundi la wazee liwe lazima liwe na michango ya vijana na vijana wawe na michango ya wazee ktk kufanya maamuzi mbali mbali. Kama mukiwaweka wazee nje kabisa watakuwa hawana la kuwashauri kwa sababu watakuwa ni autisaidaz, hawatajua ni nini kiko chunguni manake na kwa maana hiyo hawatakuwa na la maana la kukushauri. Cha msingi ni kwamba wazee wanawahitaji vijana na vijana wanawahitaji wazee.

    Kuhusu Taifa kuongozwa na vijana hilo ni swala ambalo naona mna liovaluku. VIJANA WAMESHAWAHI KULIONGOZA TAIFA LETU. Nitarudia tena vijana wameshawahi kuliogoza taifa let kwa muda mrefu sana kuliko hata hao wazee mnao waita wazee. Hao unaowaita wazee walshakuwa vijana na wao na walianza kuongoza Taifa wakiwa vijana.

    Hebu piga hesabu, wakati wa miaka ya 1960's akina Nyerere, Kawawa, Chief Fundikira, Bob Makani, Sir George Kahama walikuwa na umri gani? hao walikuwa vijana na ndio walioongoza Taifa enzi hizo.

    Piga hesabu tena, wakati Nyerere anakuwa waziri mkuu mwaka 1960/61 alikuwa na umri wa miaka 38 tu, Kijana sana! kana kwamba hiyo haitoshi, wakati Kawawa anachukua uwaziri mkuu January 2, 1962 alikuwa na umri wa miaka 36 tu.

    Edward Moringe Sokoine alikuwa waziri mkuu kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1977 akiwa na umri wa miaka 39 tu. Na Jakaya Kikwete naye alisha wahi kuwa mmoja kati ya mawaziri walio na umri mdogo sana kwene baraza la mawaziri na fikrii wakati alikuwa na miaka 36 (not sure though) lakini he was in his 30's.

    Kumbe basi Taifa limekuwa likiongozwa na vijana kwa muda mrefu sana. Kama wewe ulikuwa mtoto haina maana wao hawakuwa vijana wakati huo, walikuwa vijana kama wewe ulivyo kijana leo hii.

    Haya hebu tuje sasa ivi, angalia manaibu mawaziri wangapi ni vijana chini ya miaka 40. Nitawataja ninao wajua Deodatus Kamara(36), Lawrence Masha (36), Emanuel Nchimbi (34). Haya angalia wabunge wangapi ambao ni chini ya miaka 40.

    Vijana wapo nafikiri kwenye miksi, vijana tunachotakiuwa kufanya ni kujishughulisha na politiko process ili na sisi tujichanganye na "wazee" na hatimaye kuchukua madaraka eiza tutakapo kuwa na umri mkubwa kidogo au tukingali vijana.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2006

    Mimi ndio niliye andika 10.07AM nafikiri kama sikosei kwa mnyambulisho huo nakubali unaijua tanzania barabara kwa sababu nafikiri hujakosea kwa sababu kuna watu wengine umewataja na miaka yao. Na nimegundua kuwa uko sawa kwa mara nyingine tena nakupongeza kwa kutoa mnyambulisho huo. Kwa mtaji huo umenishinda kwamba wazee twende nao taratibu. Narudia kwa mawazo uliyoyatoa nataka kurudi nyuma na kusema inawezekana vijana wetu na vijana tunaowajua wako tofauti.

    Sijui kama nitakosea nikimaanisha nashindwa kutofautisha kuongoza kampuni na kuwa mwanasiasa naomba watu wengine wazidi kunielimisha kuhusu tofauti za vitu hivi viwili. Nini maana ya kuwa mkurugenzi wa kampuni(chief execative) na kuwa Mbunge, Waziri na mtu mwanasiasa mwingine.

    Mwenye mawazo, au chief exacutive yeyote anipe tofauti zake. Nitashukuru. make nilisha msikia JK akisema Uwaziri hausomewi????????

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 23, 2006

    Nashukuru sana anony hapo juu kwa jinsi tulivobadilishana mawazo. Nashukuru kwani umenifanya niikumbuke historia ya TZ ambayo niliisoma shule ya msingiiiii. hata hivyo ilinibidi niende kwenye vitabu vya kumbu kumbu ili niwe na data za kukukonvinsi.

    Kuhusu swali lako la Chief Executive na cheo cha kisiasa mimi kwa maoni yangu naona tofauti iko moja CEO anajiteua kama kampuni ni ya kwako au anateuliwa na mwenye kampuni wakati kwenye siasa inapaswa uchaguliwe na wananchi.

    Zaidi ya hapo mimi noana waote ni sawa tu, woote wanatakiwa kuwa na lidaship skills nzuri, wanatakiwa kuwarizisha waliowachagua, wanatakliwa kuwaletea maendeleo wananchi wao.

    Ni kweli kabisa JK alivosem ahuwezi kusomea uwaziri wala U CEO. Lakini kuna masomo unayoweza kusoma ili kukusaidia ktk ufanisi wa kazi yako. kwa mfani somo la critical thinking, manejimenti, bajeting n.k haya ni masomo ambayo sio lazima uyasome kuwa CEOau waziri lakini ukiyasoma yatakusaidia kuwa waziri au CEO mzuri.

    ReplyDelete
  12. Source:: Daily News Saturday
    Story by: DAILY NEWS Reporter
    Date: 20.05.2006


    PRESIDENT Jakaya Kikwete has appointed Mr Issac Mruma (51), the Managing Editor of Tanzania Standard Newspapers (TSN), publishers of 'Daily' and 'Sunday News'.

    A statement issued yesterday by the Director of Information Services (Maelezo), Mr Kassim Mpenda, said Mr Mruma's appointment became effective last Thursday.

    Mr Mruma, a former Daily News member of staff, is currently Assistant Director of Public Consumer Affairs with the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA).

    He rose through the ranks to become News Editor at TSN and later joined Bunge as Education and Information Officer.

    He was then seconded to the Office of Chama Cha Mapinduzi Secretary-General as Assistant Press Secretary before he was appointed Press Secretary to the Prime Minister.

    Before the formation of TCRA following the merger between Tanzania Communications Commission (TCC) and Tanzania Broadcasting Commission (TBC), Mr Mruma worked as the Public Relations Officer (PRO) for TCC.

    The new Managing Editor, who is married with three children, is an MBA holder, having obtained his Bachelor of Arts degree in International Studies from Belgrade University in Yugoslavia and diplomas in journalism from Dar es Salaam and London schools of journalism.

    Early this year he received certificates in website and multimedia designing, production and video editing from Mumbai, India.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 24, 2006

    Tunategemea uongozi bora na uzoefu alionao Mr Issac Mruma(51) katika kuiendelea TSN. Tunamtakia mafanikio mema katika kazi yake na kuibadisha kwa Hari mpya, nguvu mpya na kasi mpya kama alivyosema Rais na kuboresha TSN kuwa mojawapo ya makampuni bora Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...