hekalu lilopigwa nyundo na site lililopo masaki barabara ya toure kuelekea hoteli ya sea klifu, kona ya kwenda ubalozi wa afrika kusini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2006

    MICHUZI,UNAMANISHA NINI?UNAPOSEMA KUPIGWA NYUNDO?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2006

    Linategemewa kupigwa nyundo,kama manispaa ya kinondon watashinda kesi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2006

    mbona kama wameshalivunja vunja si wamalizie tuu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2006

    Mnalionaje hili swala la kuvunja nyumba Jamani! Kusema kweli mimi sijaliunga mkono kutokana na sababu zifuatazo.

    Kama alipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili au nne akajenga nane alifanya kosa kwa upande mmoja. Ila kama alipewa kibali cha gorofa mbili akajenga nane ni mtu aliyejitahidi kuchangia katika maendeleo ya taifa letu endapo kama jengo limejengwa katika taratibu za kufaa za kihandisi na kama halihatarishi maisha ya watu watakao ishi au kutumia jengo hilo. Sasa endapo alikiuka na amejenga hili jengo kwa ujenzi wakufuata utaalamu wa kuihandisi na wakuaminika sioni haja ya kubomoa hili jengo. Kwa nini? Ni kwa sababu kama likiuka taratibu alitakiwa asimamishwe kuendelea kujenga kabla hajafikia hatu a za mwisho za jengo hilo. Pili kwa hali ya Watanzania tulivyo na umaskini wetu, ni kwamba kutumia vihela tulivyo navyo nakubomoa nyumba ambayo wnegi wetu tunakosa pakufanyia kazi au kuishi ni makosa hata mbele ya mungu. Kwanza kubomoa ni gharama, unatumia mali za wananchi kubomoa mali za wananchi ambazo ndio hazina za taifa. Kwa nini asipewe adhabu au likataifishwa likawa mali wa umma, kwa nini asitozwe fidia kwa ajili ya kukiuka taratibu hiyo fidia ikawalisha wenye njaa na hiyo hela ya kubomolea ikanunua dawa hospitali? Walikuwa wapi hadi jengo likafikia hatua hiyo? Hilo jengo kwaninia hata serikali isilitaifishe na kulifanya kuwa hospitali ya wilaya kulikoni kulibomoa kama liko kwenye ubora? Hawa wafanyakazi wa sekata mbali mbali walio sababisha yote haya wamesha chukuliwa hatua gani ya kuwawajibisha? tusaidiane mawazo kwa hilo huenda niko njia panda wazee!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2006

    hata mimi sijaliunga mkono labda kama hiyo hela kaiiba. Lakini hivi hivi ni kutiana umasikini jamani. Ardhi tanzania tunazo kibao majumba yaliyojengwa kiolela ni mengi huyu tena kajenga bichi. Mimi sioni haja ya kumfanya masikini. Ingelikuwa mimi ningesema imeisha tokea na uwe mwisho,. Halafu unashughulikia waliohusika. katika kutoa vibari.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2006

    Hata mimi imeniuma sana kwani licha ya kuvunjavunja hilo ghorofa wameiba vitu vingi tuu kama TV,Ma-Sink,Makochi,A/C... Ndimi PM K'nyama...

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2006

    Masikini kasi mpya haiwezi kumsaidia huyu mtanzania?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2006

    Mimi tatizo langu ni kwa huyu jaji ambaye ametoa amri ya jengwa kuvunjwa bila kusikiliza defence ya jamaa. Alafu sasa hivi eti wasilivunje wanasubiria kwenda maakamani. Jamaa akishinda kesi kama kweli alikuwa na kibali lazima serikali imlipe ma billion ya pesa kwajili watu wameiba sana kwenye hili jengo mpaka tiles yani aibu. Bongo sio siri kuna nyumba nyingi zimejengwa bila mpangilio eti kwenye ripoti ya hao majamaa wanacheki kama zimeingiliana na waya sijui mabomba ya maji. Hizo waya ziko wapi wakati umeme hatuna, ebu waende uswazi waangalie nyumba na nyanya kama fence vile, wakitaka kuendeleza ujengaji wangeaza sehemu kama manzese ambapo korido ya nyumba ndio barabara. Au PM analeta mfu wa kuwakomesha wa juu ndio wachini wataiga?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2006

    Sheria msumeno. Full stop. Watanzania jifunzeni kufuata haki. Unajua uchungu wa kunyang'nywa kiwanja chako cha haki? Uozo wa maafisa wa ardhi na wanaotoa rushwa usiwe na nafasi tena.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 26, 2006

    SUALA LA MIPANGO MIJI TANZANIA LITACHUKUA MUDA NA LINAHITAJI KIONGOZI WA WIZARA MWENYE VISHENI NAUWAJIBIKAJI WA ZIADA.
    SIONI KAMA KUNA UHALALI WA KUBOMOA JENGO HILO HATA KAMA HUYO BWANA AMEVUNJA SHERIA;ANGESIKILIZWA,NA KISHA WALIOMSAIDIA KUPOTOSHA UKWELI(WANAOBOMOA JENGO)WANGESHUGHULIKIWA KWANZA.
    INAUMA!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 28, 2006

    huyu mwenye jengo ni muhindi koko hawana heshima wala adabu wanajisahau kwamba sisi ni wazawa na hii ni nchi yetu, dada zetu wana nyanyaswa sana na hawa wahindi kwenye vigogofa upanga, na watu wa NHC wamewajaza wahindi tu kwenye maghorofa kwa ajili ya rushwa wakati sisi pia tunahitaji kuishi kwenye hizi nyumba za gharama nafuu. hawa wanahela hawajengi na wakijenga ndio kama hivi hawafuati sheria. Mimi naunga mkono maghorofa yabomolewe ili iwe fundisho na bado atalipia gharama za uvunjaji, kiboko yao alikuwa Iddy Amini uganda mpaka leo wana adabu hawa wahindi,na ilala tunakagua maghorofa yote tukiona tatizo tuna bomoa na kuiba kama kawa vifaa vya ndani

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2006

    Kama ni mhindi nafikiri hata urahia kanunua tu si mtanzania akifanya fujo arudishwe kwao, tutaomba tikira aingilie kati suala hili. Hawa wezi tu

    ReplyDelete
  13. Sheria ni msumeno.
    Itakuwa ni kosa iwapo jaji kaamua jengo livunjwe kabla ya kusikiliza kesi.
    Nadhani mrorong ungekuwa:
    - Ujenzi usimame (mwenye mali aweke ulinzi)
    - Kesi ifanyike
    - Jamaa akishinda (manispaa ya kinondoni ilipe gharama za ulinzi + ucheleweshaji kumaliza ujenzi
    Jamaa akishindwa - Jengo linavunjwa (hasa kama kuwepo kwake hapo kutahatarisha maisha ya watu!

    Sioni kwa nini inakuwa rahisi sana kumuhurumia mtu ambaye kuna uwezekano kavunja sheria!
    Yes, maofisa wahusika - itabidi waonje joto ya jiwe (kufukuzwa kazi - sounds fare!)
    LAKINI na jamaa naye inabidi aonye kajoto kidogo.
    * Iwapo nitakuja nyumbani kwako - nika-paki Lexus hapo nje, nakukuachia ufunguo. Wewe ukaanza kutanua nayo (kwa kudai kuwa umepewa) bila kujua kama hiyo gari ilikuwa imeibiwa. Ukikamatwa nayo ndugu - ni Ukonga! Inaitwa kukutwa na mali ya wizi!
    Ned

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 01, 2006

    Michuzi hapa kuna wanasheria wengi...hili swala la kubomolewa hili jengo lina utata sana.Kama nimeelewa vizuri zilikuwa na apartments hizi. Hili eneo haliruhusu ghorofa zaidi ya ngapi au kosa haswa mpaka mali hii iharibiwe hivi ni nini? Nakumbuka (Sheraton Hotel) sasa ni Royal Palm watu walilazimisha iwepo eneo hilo la mjini kwa ajili ya wateja,lakini sheria ilikuwa hairuhusu ghorofa ndefu eneo hili sababu inazuia upepo(kama nipo right) walipokuwa maofisa wa Sheraton hotel walikataa ile hotel kupewa hadhi ya sheraton, sababu floor zilikuwa chache na hadhi yake haikuwa nzuri. (Mimi pengine sielewi vizuri kama kunamahali nimekosea nirekebisheni). Sasa pakibomolewa patabaki kiwanja tu, au atakuja kuchukua mkubwa wa nchi ale pesa kilaini, maana kumbukeni hata viongozi pia wanaona location inalipa??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...