nimeingia leo bongo na moja kwa moja nimeenda neshno kutesti kamera yangu aina ya nikon d70s na kukuta yanga anacheza na timu ya all stars ya burundi. msindi alikuwa yanga kwa bao 2-1. hapa ni ivo mapunda akipangua krosi hatari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2006

    Michuzi,
    Kamera nzuri hiyo.Picha kama hizi huwa ni ngumu kuzipiga bila utaalamu kama wa kwako ukisaidiwa na tekinolojia ya kamera kama hiyo ya Nikon.Nadhani mwaka jana Nikon ilikuwa ndio kamera ya mwaka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2006

    Michuzi, vipi tena, nilidhani 350D ni bora kuliko Nikon D70S maana tuliona wakati fulani umejitwika mkanda wa Canon EOS 350D.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2006

    Bora ungeupgrade na Canon kama ipo

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2006

    Bwana Michuzi tunaomba kusoma deli nyuzi humu

    ReplyDelete
  5. canon yangu ni eos 300D. na nikon bora ni D1 ambayo bei ni dola kama 4,000, nami ubavu huo sikuwa nao. nimechagua hii sababu ya lenzi yake ya 70-300mm ambayo canon hatoi pamoja na kamera, na peke yake bei mbaya. deli nyuzi ntaiweka MK akinifunza namna ya kufanza hivo..

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2006

    Deli nyuzi inapatikana kwa anuani hii http://dailynews-tsn.com/.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2006

    LAKINI MICHUZI MIE MBONA NAONA PICHA ZA MWANZONI NI BOMBA KULIKO ZA HIYO KAMERA MPYA?NINI TATIZO?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 19, 2006

    Michuzi hiyo nikon d70s, migiro kailipia nini,inakaribia milioni mbili thamani yake.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2006

    Nikon D70S unaweza kuipata hata kwa Dola 800-900. Siyo ghali tena kwani ina mwaka tangu itoke na haikuuzwa kwa wingi kama walivyotazamia.

    Ila ina performance nzuri kuliko Rebel I(300D), easier to handle, better picture quality, wider flash angle and photo stability especially when taken with external flash. Only minus thing I can think of ni lack of vertical grip, unlike most Cannons.

    Nadhani ni compromise nzuri kati ya bei na performance ukilinganisha na better quality EOS cameras.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 20, 2006

    Hao walioko kwenye neshino stedium mpya wamelipa kiingilio lakini au wanafaudu bure?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 20, 2006

    huyo beki wa yanga aliye mlingotini kama willy martin kimaumbile.

    ReplyDelete
  12. rj, ingawa inglishi iz noti richebo, nashukuru kwa maoni kuhusu kamera. umenikuna kweli. unajua nikon rebel 300d lenzi yake haikawii kudata. ingawa kweli nikon 70d ni bomba zaidi, si uwongo kukamata kwake, hasa ukiwa umezoea eos, kidogo matata. umahiri wake wa flashi nimeuona usiku wa jana kwenye miss upanga (ona picha baadae kidogo). asante kwa utaalamu na kubadilishana mawazo. je unanishauri nikitoka hapa nikon 70d nipande wapi. je wewe watumia nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...