Home
Unlabelled
jk
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
baba baba ongeza mwendo kasi hivyo hivyo. handsome boy.
ReplyDeletekweli rais wetu handsome,utazani yu 28yrs old.anavutia.
ReplyDeleteMawanzo yangu kwa huyu bwana ni pale anapo amua kufufua upya elimu. jamani hata mliyo ugaibuni mnajua dunia hii bila elimu ufiki popote. Bahati mbaya awamu zote zilizo pita hazikujua kwamba msingi mkubwa wa maendeleo ni elimu. Leo hii china, japani, Korea na nyingine zilizo endelea zilikaa chini kwanza zikaakikisha watu wake wanapata elimu ambao ndio msingi mkubwa wa maendeleo. Hizi awamu zilifikiria kwa ujanja ujanja tunaweza kufika mbali. Zilisahau kuwa bila elimu leo hii unaweza kuwa tajiri kesho maskini. Kwa hiyo kitu kikubwa ambacho watanzania wataweza kuongea na kusikika katita hizi karne za sayanz si na technologia ni Elimu tu. Vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu. Huyu jamaa kwa mtaji huo wa kufikiri kufufua elimu kuanzia msingi namfagilia. Wawawwaa!!!!!!!!!!!!!!.
ReplyDeleteMungu amuongezee nguvu apambane na majangili na mafisadi wa tanzania.
hana kitu huyu!
ReplyDeletewewe anony wa 10:27 am ni elimu gani aliyofufua huyu? Acheni kufanya maskhara. Hebu tushushie elimu aliyofufua kama siyokuangukia kwenye mkumbo wa kumsifia tu. Huko Mlimani si ndiyo matatizo tupu pamoja na bodi ya mikopo kuundwa. Pesa yote wamemalizia kwenye kampeni. Kitakachomponza huyu jamaa ni sifa nyiiiiiingi kumbe hakuna anachofanya
ReplyDeletesomeni hii..
ReplyDeletehttp://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2006/05/20/66786.html
Leo nimesoma hii habari kwenye majira..
http://www.majira.co.tz/kurasa.html?soma=tanzania&habariNamba=701
What do you think? Kuna njama kweli au ni usanii wa kisiasa? Kwa upande wangu naona hizi ni porojo tu. Sijaona link yoyote ya uchumi kushuka na njama.
Siku moja nilikuwa naongea na African-American mmoja akaniambia anataka sana kwenda Africa ila gharama ya usafiri ni kubwa sana akaniambia sababu kubwa ni kwamba wazungu wataki wao waende Afrika ndiyo maana wanaweka bei kubwa. Ni kweli gharama ya kwenda Afrika ni kubwa kuliko sehemu yoyote duniani lakini sababu alizozitoa si za kweli ingawa kwa juu juu unaweza ukakubaliana naye. Kama ungekuwa ni uamuzi wa wazungu basi wangewarudisha wote kwao Afrika. Bei ya mafuta haijaongezeka Tanzania tu, ni karibu dunia nzima ingawa rate ya kuongezeka inategemea na uchumi wa nchi.
Kuna mahali niliandika kwamba iliwachukua wabongo miaka zaidi ya kumi kugundua kwamba Mrema hana lolote nashukuru Mungu sijawahi kumuunga mkono Mrema. Leo hii watu wote waliokuwa wanamuunga mkono wanajutia muda wao. Kwa jinsi JK alivyo mashuhuri labda 30 years who knows. You guys just be happy that you are blessed and poor. Life goes on.
Inaonekana Sam unaakiri sana I can't believe. Ningelikuwa nakujua ningependa tuongee siku moja. kwa uchache Unaona mbali. Anony. wa 7.51PM omba mungu umalize shule Tanzania ni ngumu. Lakini ninachofikiria mimi JK akishindwa kazi sijui kama tutampata mtu anayeweza kuitawala vizuri sana Tanzania(mawazo yangu). Hii ni kwa sababu ya imani walioonyesha watanzania kwake. Believe me it will take century without getting somebody with acceptance like JK. Mikopo bodi mimi nilikuwa na wasiwasi na hiki kitu walikuwa wanakopesha kama vile mtu anaenda kuomba maji bahari ya hindi. najua mnajua hapa maji si ni tele hayaishi. Lakini nafikiri iliundwa kukidhi matakwa ya chama tu.
ReplyDeleteIf tanzania will not learn from outside (RSA, Kenya etc) kwa nchi ambazo zimeweza kukopesha wanafunzi/kuunda sera nzuri za elimu na zikapata mafanikio, presha za kisiasa hazitasaidia. Leo hii watanzania wangapi wamekopeshwa na wamesoma kwa mikopo. Jibu ni wengi since 1994. Ni wangapi wako tayari kulipa zero why? sababu ni nyingi mojawapo ni ya anony wa 7.51PM. Wakati Beni akiwa waziri elimu ya juu na Birari, wakati watu wanaenda kufatilia mikopo wanapigwa mabomu kwanza wakati huo peasa zinakimbizwa chuo kikuu. Unapata peasa na maumivu juu yake. nani aende kulipa pesa wakati alipigwa ngwala na ffu ndo akapewa.
Niliona mkenya mmoja yuko nchi za nje anaenda kulipa mkopo aliyosomea nikamuuliza kwa nini. Akasema nini kibanda nilichojenga wakati nasomeshwa na serikari. Na wako tayari kulipa. Tanzania hata ilikopesha na wanyarwanda kipindi hicho. Sijui watawafata Rwanda.Ninavyojua kwa sasa nivigumu serikali kuwasomesha wanafunzi wote tanzania let us have education policy whereby industries will contribute like South Africa. Kwanini wao wameweza?
Samahani kwa kuwachosha.
Sam 9:25 PM, ni kweli unachosema. Mimi lakini binafsi sidhani kama wazungu wangependa kuwarudisha african americans wote africa, kumbuka ingeleta patashika kubwa once wakishafika na bado wanaitegemea africa sana kwa market na malighafi. Kuna ambao walikuwa advocates wa kurudi africa, naamini unawajua kina marcus garvey wakajikuta wao ndiyo wanakuwa deported. Kuna watu kama africa bambataa walianza kampeni za kulink AA na waafrika wakajikuta wanasakamwa hadi wakaacha. Huwa najiuliza sana nasema blacks duniani tukiunda some kind of network ya kushirikiana, not necessarily wote kurudi afrika tutakuwa na nguvu kuliko race nyingine yoyote.
ReplyDeleteKuhusu Mrema, mimi nilimpigia kura uchaguzi wa 95 najuta. Nadhani wapinzani wengi, hata hao wasomi kina mbatia na mbowe ni CCM. Usije kushangaa hata mtikila ni ccm. Kama walikuwa haraka kumhorace kolimba wamekuwa wanasubiri nini kwa watu kama kina mtikila ambao wanataka tanganyika? Anyway, siasa nimeachana nazo mimi, hii ni moja ya rare situations naongelea siasa.
Anon 7:22
ReplyDeleteHivi wamrekani unafikiri wanakuoneeni huruma sana ninyi waafrica? Kuna soko gani wamarekani wanalitegemea huku Africa? Labda silaha (Sina uhakika) na kam ani silaha basi hawakupendeni kwani hizo silaha ndio zinaendesha mauaji ya kinyama ktk hizo vita zinazoendelea Africa.
Na hizo vita zilizo africa zingalikuwa bara lingine sio ajabu zingeitwa World War XYZ.
Kwa kweli zaidi ya silaha mie sijawahi ona bizaa za kimarekani nyingi hapa africa. kama kuna mtu ana data tafazali zitoeni
Ni kweli ulichosema, lakini sikumaanisha kwamba wanatupenda weusi. Kuna mtu alisema marekani wanaspend zaidi kulinda walichoinvest kuliko thamani ya investment yao (mfano singapore nafikiri wanaspend kwenye base yao kama bil 8 wakati investment ni 3, around those #s).
ReplyDeleteWana investments nigeria, egypt, sasa libya na silaha kwa wingi sana. Si ajabu hata TZ tunanunua silaha kutoka us, sasa rudisha weusi wote kama hawajavunja mikataba....unaongelea billions and billions of investment. Hata hivyo, sasa ni too late, tayari weusi na wazungu wameshajimix na kuzaliana utaanzia wapi?
Nashukuru bi/bw. hapo juu kwa kutuletea hiyo link kuhusu ziara ya Rais na matarajio yake ya kuleta wawekezaji ndani ya nchi.
ReplyDeleteNingeiomba Serikali iweze kuingia mikataba na hayo makampuni na hiyo mikataba iweze kuwasaidia watanzania na sio kuwasaidia wao (makampuni na viongozi wetu) kwa kuweza kupokea 10 per cent.
Wanabidi waelewe ya kwamba watanzania tunajua kila kitu kinacho endelea na wasije wakazani sisi ni mambumbu hivyo basi kutokana na taifa letu limebalikiwa na kuwa na utajiri mkubwa ni mategemeo yetu kwamba maisha yatapunguwa ugumu kwa kila raia kutokana na uwekezaji huu utakao kuja.
Watanzania wote tungeomba tuwe na mawazo mazuri ktk kuchangia ili yatuwezeshe kufika mbali na sio kuwa na mawazo ya kutoa matusi na kusema watu ktk picha mbali mbali.
Anony 11.38AM shukrani kwa mawazo yenye busara nyingi sana nafikiri wote tukichangia mawazo kama ya kwako Tanzaia itafika mabli na ningependa kuongezea wale watu wanaosoma/kufanya kazi ugaibuni nimekuwa nikiona wanasema ndo maana hatuendelei. Mimi ningeomba watushauri kwa kutumia picha ya rais wetu hii hapa. Je Watanzania tufanye nini ili tuendelee katika nynja mbalimbali. Ukiangalia katika sehemu yako ulipo je huko wenzetu wanafanya nini na mbinu gani hili na sisi tuangalie kama zinaweza kutusaidia. Mimi ni Mtanzania tu ninayependa kuona mawazo ya wengine na mijadala mbalimbali ambopo najua watu wengi wanapitia hapa.
ReplyDeletemnaofagilia huyu mtu sijui mnafagilia kwa lipi! ni kweli kwamba ccm ilichukua pesa za epa kufanyia kampeni kama hujui hilo njoo uniulize mimi. ndio maana hadi sasa hivi swala la hizo pesa kurudishwa imekuwa kama mchezo wa kuigiza. hivi ile kampuni hewa ya kagoda mnajua ilisajiliwaje? au mnabwabwaja tu ilimradi msikike kwamba mmmesema. halafu nawe michuzi inaonekana umeweka yale maoni yanayomfagilia tu ili kuwakoga watu waone kwamba wananchi waanaridhika na utawala wa huyu jamaa wakati si kweli.
ReplyDeletehivi zile pesa zilizochotwa wasingeweza KUKOPESHWA wanafunzi badala ya watu KUJICHUKULIA halafu wanapewa deadline ya kurejesha? kama ndivyo basi wale watu walofungwa magerezani kwa kosa la kuiba KUKU wafunguliwe kisha waopewe muda wa kurudisha kuku waloiba kama hawa wezi wa epa! ndio. si sheria ni msumeno bwana?
kama rais anakaa mezani na wezi waka-negotiate namna ya kurejesha pesa walizoiba kuna kosa gani kama walofungwa kwa kuiba kuku nao wafunguliwe wakae mezani waelewane watarudisha lini kuku wa watu walowaiba?