
katika miaka yangu takriban 20 kwenye fani ya kupiga picha, hakika nimepiga picha nyingi na kila mojawapo naipenda kama mtu umpendavyo mtoto wako, hivyo hata wawe mia, penzi lako kwao huwa sawa. lakini pamoja na hayo, mmoja wa watoto hao anakuwa kipenzi, kama ilivyo picha hii ya sanamu ya bismini mtaa wa azikiwe


aahhh hii picha ni ya zamani sana jamani hivi michuzi nani alibuni na kutengeneza picha hii..??
ReplyDeleteUshaambiwa hili ni sanamu la bismin (askari monument) we unadai ni picha na unaulizia nani katengeneza picha hii,siku ukija dar toka huko kwenu kijijini ulizia mtaa wa samora na azikiwe kwenye makutano ndio kuna hili sanamu, na wala usiliogope maana wengi wakija wananyoosha mikono juu wakihofia bunduki yake
ReplyDeleteAnony wa 10:00 hebu soma vizuri malelezo ya michuzi hapo juu ndio utajua kama aliandika sanamu au picha...
ReplyDeletekumbukumbu zenu wote tisa kumi yangu pale alivyoigiza bambo mhh nilicheka sanaaaaaaa sijui michuzi uliwahi kumwangalia bambo akiigiza pia? hivi yupo siku hizi na je bado anaigiza? maana sijamsikia siku nyingi nimesikia ametoa wimbo wake mzuri.
ReplyDeleteSanamu lenyewe jeusi aswaaaa, lakini mimi nimefurahishwa na picha yenyewe, ulivyoipiga 'against light' na ilivyotoka. Umenikumbusha mbali katika somo la picha, kwa mwalimu Bob mcDonald pale SAUT kuwa inaitwa 'Silhouette'
ReplyDeleteWatu wa zamani wa Dar hawakusema "sanamu ya Bismini" bali "picha ya bismini". Kabla ya picha ya Michuzi. Kumsema mtu anayeiita hii "picha ya bismini" kwamba ni mshamba ni kutojua jina na lugha halisi.
ReplyDelete