kakampuni ketu kalishinda tuzo ya kibanda bora cha elekroniki sabasaba ya mwaka juzi. mwaka jana kalikuwa ka pili, mwaka huu sijui itakwaje. ila tupo na usikose kutembelea photo point banda la pta kubwa mwisho kushoto mtaa wa kwanza. hapo napokea hiyo tuzo toka kwa makamu wa rais dkt ali mohamed shein

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Michuzi kwa kweli unajua kutumia kipaji chako maana humo humo umeweza hadi kuunda kampuni, lakini mimi bado sielewi kidogo shughuli hasa kampuni yako, je ni kupiga picha tu au na shughuli zinginewe? hebu tupatie mwangaza kidogo wasomaji wako.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2006

    Eh wananchi.. katika pita pita zangu nikakutana na blogu zingine kama hii ya michuzi, nikaona nisiwanyime uhondo. Mnaweza kuzitembelea http://www.blog.co.tz/athumani
    http://www.blog.co.tz/mrocky

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2006

    Asante Aisha, lakini hapa nafikiri si ubao wa Matangazo. Vi blog vyenyewe vimechoka kama nini!! Upigaji wa picha zile haujanikosha roho. Waeleze akina Athumani na Mrocky wajaribu kupiga picha vizuri.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2006

    Anony wa 4:19pm acha mtimanyongo!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2006

    We anony 4:19 mbona m-binafsi sana? kama hujakosheka roho ni wewe peke yako!

    ReplyDelete
  6. mija!

    kukujibu ni kwamba kakampuni haka ka photo point kanashughulika na upigaji, usafishaji na uchapachi wa picha za aina zote, mkazo ukiwa kwenye digital imaging, ikiwa ni pamoja na picha za studio, harusi na hafla zingine zote. pia tunauza filamu na kamera na vifaa vya picha kama vile fremu na albamu.

    dada aisha nakuunga mkono kwamba tunamabloga wa picha wengine kama ulivyotaja hapo juu, ambao ni hodari kwa kazi hii na si vibaya kuwatembelea kupanua wigo la blogu za picha.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2006

    Ama kweli Michuzi wewe uko tofauti. Ni watu wachache sana wana moyo kama wa kwako. Wangapi wanaweza kufagilia biashara za washindani wao?

    Wewe bila hiana unashauri watu watembelee blog pinzani.

    Tunahitaji wengine wachache kama wewe ili tuendelee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...