
kakampuni ketu kalishinda tuzo ya kibanda bora cha elekroniki sabasaba ya mwaka juzi. mwaka jana kalikuwa ka pili, mwaka huu sijui itakwaje. ila tupo na usikose kutembelea photo point banda la pta kubwa mwisho kushoto mtaa wa kwanza. hapo napokea hiyo tuzo toka kwa makamu wa rais dkt ali mohamed shein


Michuzi kwa kweli unajua kutumia kipaji chako maana humo humo umeweza hadi kuunda kampuni, lakini mimi bado sielewi kidogo shughuli hasa kampuni yako, je ni kupiga picha tu au na shughuli zinginewe? hebu tupatie mwangaza kidogo wasomaji wako.
ReplyDeleteEh wananchi.. katika pita pita zangu nikakutana na blogu zingine kama hii ya michuzi, nikaona nisiwanyime uhondo. Mnaweza kuzitembelea http://www.blog.co.tz/athumani
ReplyDeletehttp://www.blog.co.tz/mrocky
Asante Aisha, lakini hapa nafikiri si ubao wa Matangazo. Vi blog vyenyewe vimechoka kama nini!! Upigaji wa picha zile haujanikosha roho. Waeleze akina Athumani na Mrocky wajaribu kupiga picha vizuri.
ReplyDeleteAnony wa 4:19pm acha mtimanyongo!
ReplyDeleteWe anony 4:19 mbona m-binafsi sana? kama hujakosheka roho ni wewe peke yako!
ReplyDeletemija!
ReplyDeletekukujibu ni kwamba kakampuni haka ka photo point kanashughulika na upigaji, usafishaji na uchapachi wa picha za aina zote, mkazo ukiwa kwenye digital imaging, ikiwa ni pamoja na picha za studio, harusi na hafla zingine zote. pia tunauza filamu na kamera na vifaa vya picha kama vile fremu na albamu.
dada aisha nakuunga mkono kwamba tunamabloga wa picha wengine kama ulivyotaja hapo juu, ambao ni hodari kwa kazi hii na si vibaya kuwatembelea kupanua wigo la blogu za picha.
Ama kweli Michuzi wewe uko tofauti. Ni watu wachache sana wana moyo kama wa kwako. Wangapi wanaweza kufagilia biashara za washindani wao?
ReplyDeleteWewe bila hiana unashauri watu watembelee blog pinzani.
Tunahitaji wengine wachache kama wewe ili tuendelee
Asante kwa maelezo.
ReplyDelete