Home
Unlabelled
vipaji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Michuzi embu tuwekee picha ya sheikh huyo ambaye kamtukana mengi na ambaye anataka asomewe fatwah.Huyu sheikh mbona analeta mambo ya kidini sasa,tutaogopa kurudi tanzania sasa, kama mambo yenyewe yakiwa ukristo na uislamu.
ReplyDeleteKauli ya Sheikh dhidi ya Mengi yapingwa
ReplyDeleteHabari Zinazoshabihiana
• Mengi abana vigogo wamwombe radhi 26.05.2006 [Soma]
• Masheikh kuchunguza mgogoro wa Waislamu na 'Quality Group' 09.03.2006 [Soma]
• Osama Bin Laden aibuka kwa vitisho 25.04.2006 [Soma]
*Manji awaandikia barua viongozi Msikiti wa Idrissa
*Awataka wasitishe azma ya kusoma dua ya albadiri
Na Gladness Mboma
WADHAMINI na Waasisi wa Msikiti wa Idrissa, Kariakoo, Dar es Salaam, wamesema kauli ya Sheikh Ali Bassaleh ya kudai kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya IPP Limited, Bw. Reginald Mengi, anaupiga vita Uislamu ni ya uchochezi.
Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Katibu wa Familia ya Sheikh Idrissa bin Saad, Alhaj Saidi Rubeya, wakati akizungumzia kauli ya Sheikh Bassaleh kuhusiana na Bw. Mengi ya kuhusisha kutumia vyombo vya habari kupiga vita Uislamu na Waislamu.
"Kwa mantiki hiyo, sisi wadhamini na waasisi wa Msikiti wa Idrissa, tunatoa msimamo wetu kwamba kauli ya Sheikh Bassaleh haina uzito wowote kuthibitisha kuwa Bw. Mengi anaupiga vita Uislamu kwa maana yoyote," alisema.
"Tukiwa kama familia ya Sheikh Idrissa na wadhamini wa Msikiti wa Idrissa, hatukubaliani na kauli ya Sheikh Bassaleh, tunapinga yeye kuutumia Msikiti kuendesha uchochezi wa kisiasa na kidini. Uislamu hautaki dhana, unataka ushahidi wa kweli, ndipo Waislamu waamini kuwa dini yao inapigwa vita," alisema Alhaji Rubeya
Alisema viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) hawateuliwi kwa Uislamu wao, bali kwa sifa ya elimu, uadilifu, uaminifu na uwezo wao wa kuongoza na suala la kuhoji mapato na matumizi ya NSSF, liko ndani ya wadau wake, ambao ni jamii ya Watanzania ambao ndani yake wamo Waislamu na Wakristo na dini nyingine.
Alhaji Rubeya alisema kwa sababu hizo, suala la vyombo vya habari kuandika habari za NSSF, halina sababu za kutosheleza Waislamu kuona kuwa vyombo vya habari vya Bw. Mengi pamoja na ukristo wake, kuwa anapiga vita Uislamu.
Alisema kauli za uchochezi wa kidini ni suala la hatari kubwa katika jamii, ambalo athari yake ni kubwa inayosababisha jamii kusambaratika na kukosekana amani na umoja katika jamii.
Alhaji Rubeya alisema bado jamii ya Watanzania kwa muda mrefu, haijawa na chuki za kidini na wanashirikiana katika mazishi, harusi, sherehe, kazi na elimu, ni dhambi kubwa kwa Mwenyenzi Mungu kutaka kutumia dini ili kulisambaratisha Taifa lenye amani, umoja na upendo.
Aliwataka Waislamu kupima mambo kabla ya kufikia uamuzi na wakazanie watoto wao kwa nguvu zote, ili wapate elimu dunia na kushikamana.
Alisema Bw. Mengi amekuwa akitoa misaada mingi kwa Waislamu bila kubagua, hivyo anashangazwa na kauli ya Sheikh Bassaleh ya kudai kuwa Bw. Mengi anaikashifu dini hiyo.
Jana katika Msikiti wa Idrissa, Sheikh Bassaleh alisema hatakuwa tayari kumwomba radhi Bw.Mengi kutokana na kauli yake, kuwa Mwenyekiti huyo wa IPP anatumia vyombo vyake vya habari kuupiga vita Uislamu.
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group, Bw. Yusufu Manji, amewaandikia barua viongozi wa Msikiti wa Idrisa, akiwataka kusitisha alichokiita ni azma yao ya kumsomea albadiri Bw. Mengi.
Katika barua yake ya jana kwa Sheikh Kondo Bungo, Sheikh Idris Mtambani na Sheikh Bassaleh, Bw. Manji, alisema alipokea kwa masikitiko habari zilizoandikwa katika gazeti moja la Mei 25-31 mwaka huu, kuhusiana na azma hiyo.
"Machozi yamenilenga niliposoma habari hiyo, maana mimi ni mwelevu wa kutosha kujua uzito na athari za dua kama hiyo...wale ambao wanaelewa mambo haya, wanafahamu kuwa dua maalumu ya albadiri haina kinga na inawateketeza masikini na wafalme, bila kubagua," ilisema sehemu ya barua hiyo.
Alisema katika barua hiyo kuwa yeye ni mtoto mchanga katika masuala ya dini yake na anakubali kwa moyo mmoja kuongozwa na maimamu wake hao, lakini nafsi yake imemsuta na kumtaka ajitahidi kumwokoa binadamu mwenzake katika janga lililoko mbele yake.
Bw. Manji alidai kuingiwa na moyo wa huruma kwa watakaoathirika endapo dua hiyo itasomwa, hasa familia ya Bw. Mengi.
source:majira
AKIIWEKA HIYO PICHA NA YEYE YUMO NDANI YA HIYO ALBADILI!LAKINI UKWELI HUYO SHEKH ANABOHA!
ReplyDeleteWewe anony unayeposti habari za vyombo vingine vya habari acha uchuro. Kama unataka watu ambao hawajasoma habari hizo wazipate yatosha tu kutoa link ya mahali inakopatikana siyo kutuhamishia gazeti lote la majira kwenye blogu hii. Nimekuvumilia lakini sasa naona tabia yako hiii inaota mizizi. chondechonde kama hujui kupost link sema usaidiwe.
ReplyDeleteISSA MICHUZI !Kwa wengine watalalamika, kwangu mimi najua kuwa kila mtua ajaye kwenye blogu hiii anajua kuwa huyu bwana anasema kwa picha. Anawagusa watu kwa picha , Wengine wataguna, wapo amabao watazoza na kuguna. Mwisho wasiku wote wamekuja Kwa ISSA MICHUZI kwa sababu wanajua Issa Michuzi Ni Babu Kubwa. Au Mna bisha?Na hii picha haikua na ubishani wa dini yoyote
ReplyDeletejamani kuweni wasomi picha na comment mbona tofauti sielewi issa fafanua.
ReplyDelete