dakata martin mhando akimtembeza rais wa benki ya dunia paul wolfowitz ngome kongwe kule zenji majuzi. mbali ya kuwa afisa mtendaji (CEO? - ndesanjo nsaidie) wa tamasha lakimataifa la filamu la zanzibar (ziff) pia ni mhadhiri mkuu wa programu ya masomo ya media kule perth, australia, na pia ni muongozaji/mtunzi/mchezaji/mwandishi wa filamu mahiri aliyepata kutokea bongo.

baadhi ya filamu aliizotengeneza na kumpa heshima kubwa ni pamoja na

1. maangamizi : the ancient one (1998)

2. positive living (documentary mwaka 1991)

3.sadc : the first decade documentary (1990)

4. mama tumaini documentary drama (1987)

5. africa in Sweden (1985)

6. yombayomba (1985)


mbali na kuwa ni mtengenezaji filamu wa kitanzania anayefahamika katika uwanja wa kimataifa wa shughuli za filamu na televisheni, Dk martin mhando pia ni muigizaji mahiri wa michezo ya tamthiliya. ni mmoja kati ya waliokuwa waigizaji wa kikundi cha amthiliya aukwa kilichokuwa kinawajumuisha waigizaji wengine kama kina marehemu chambulikazi, profesa penina muhando/mlama, profesa amandina aihamba, mzee godwin kaduma, mwanfishi mchekeshaji adam lusekelo na mh. mathias chikawe ambaye sasa ni waziri mdogo wa sheria na ambaye ndie mume wa profesa lihamba.

kama ulipata kufurahia sauti ya kaka yake danstan tido mhando katika vipindi mbali mbali vya rtd wakati ule hususani Michezo, basi unaambiwa ukimuona dk. mhando jukwaani utaburudika maradufu ya sauti ya kaka yake, ambaye ndiye mtu wa kwanza asiye mtishi aliyepata kuchaguliwa kuwa mkuu wa idara ya kiswahili wa shirika la utangazaji la uingereza, bbc.

Baadhi ya tamthiliya alizopata kushiriki dk. martin ni :
. ayubu
. mafuta
. lina Ubani

mwenye data zaidi (damija, ndesanjo, mtimkubwa, makene n.k.) naomba. dk. mhando alizoza sana na rais wa benki ya dunia ila hakuna anaejua waliongea nini, hasa baada ya kualikwa chakula cha mchana na kupeleka kazi zake kwa paul.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2006

    Michuzi asante kwa blog. Tafadhali
    unapoandika majina ya watu tumia herufi kubwa...i.e amandina!!
    Jina lake ni Amandina Lihamba. Kama tatizo ni muda, unakuwa na haraka katika ku-post, weka picha katika blog unapokuwa na nafasi ya kutosha kuandika majina ya watu kikamilifu na yanavyotakiwa yaandikwe.
    Otherwise, Keep it up you are doing a good job.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2006

    Ahh WEWE anonymous hapo juu inakuwaje mwanangu hebu mwache michuzi ajimwae mwae kidogo...Hii ni shughuli baada ya kazi...au nakosea bwa' michuzi, sasa kama shughuli baada ya kazi bado umevaa suti kubwa na tai si utakuwa dipresdi. maisha yenyewe mafupi haya, Michuzi mtu wa watu na kitaaluma amebobea. Kama wewe unakasirika kusoma HERUFI NDOGO ZA MAJINA basi usisome, hujawekewa bastola. Michuzi, uko talentedi na niuz unaijuia, achana na warombo wenye negativu koments, lete mapicha hayo watu turikol Bongo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2006

    Nadhani kuna dhana kuwa mtu akitoa maoni yenye kukosoa Blogu ya Michuzi hathamini au kukubaliana na kiwango cha kazi ya Michuzi.

    Ndiyo maana wote wenye kutoa maoni yenye kukosoa wanarukiwa chapu chapu na maneno ya kebehi na kukatisha tamaa.

    Nadhani tukubaliane mtu unaweza ukathamini kazi ya mtu bila kuwa shabiki(ushabiki ni kuunga mkono kwa kila hali hata pale panapohitaji kukosoa). Tukikubaliana na hilo basi tutaweza kusoma maoni ya wanaokosoa kwa mwanga zaidi.

    Busara za Michuzi zinaonekana pale anapokwepa kuingia kwenye malumbano na wanaomkosoa (nadhani anachopinga ni kashfa na matusi aidha kwake au kwa wanaoongelewa kweye Blogu hii).

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 19, 2006

    Good point anony, very very good! again point nzuri saaaana! Jamani think twice.....ok?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 20, 2006

    Jamani nyie mnajibizana nini wakati tumeambiwa kina damija ndesanjo mtimkubwa na makene ndio wana data zaidi nyie kaeni kimya au hamja mwelewa michuzi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2006

    Uzuri wa teknolojia ya blogu ni jinsi inavyoturuhusu wasomaji kushirikiana na wenye blogu katika mijadala. Wenye blogu wanaandika, sisi tunasoma lakini pia tunakuwa na uwezo wa kuandika na kutoa mawazo yetu. Sidhani kama kuna watu wenye haki zaidi ya wengine kutoa mawazo. Jambo ambalo wengi hawatapinga ni kuwa hakuna sababu ya kutukana. Kukosoa ni sawa kabisa. Lakini kwa misingi ya utu.

    Kuhusu Michuzi kuandika majina ya watu bila kuanza na herufi kubwa, mimi sijui michuzi atasemaje. Lakini mimi binafsi sioni ubaya wowote. Mara nyingi mimi, kwa mfano huwa naandika neno mungu bila herufi kubwa na wala sioni ubaya wowote. Niliposoma aliyoandika nilielewa ingawa hakutumia herufi kubwa. Kwa watu wenye shughuli nyingi wakati mwingine unaandika mara moja na kutuma bila kuwa na muda wa kupitia tena. Iwapo wasomaji watasoma na kuelewa, basi mwandishi wa blogu atakuwa ametimiza wajibu wake. Mambo mengine ya sheria na kanuni za lugha ambazo wakati mwingine hazina maana sana yasituumize kichwa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2006

    Kuonyesha msisitizo kuhusu kutokuwepo na umuhimu wa hizi takatataka za herufi kubwa/ndogo au spelling naomba niwasilishe kipande hichi ambacho kuna mtu alinitumia....Cha muhimu ni kupata maana tu!


    Olny srmat poelpe can raed tihs.


    cdnuolt blveiee taht I cluod aulaclty uesdnatnrd waht I was rdanieg. The
    phaonmneal pweor of the hmuan mnid, aoccdrnig to a rscheearch at Cmabrigde Uinervtisy,

    it deosn't mttaer in waht oredr the ltteers in a wrod are, the olny iprmoatnt tihng is taht the frist and lsat ltteer be in the rghit pclae. The rset can be a taotl mses and you can sitll raed it wouthit a porbelm.

    Tihs is bcuseae the huamn mnid deos not raed ervey lteter by istlef, but the wrod as a wlohe. Amzanig huh? yaeh and I awlyas tghuhot slpeling was ipmorantt!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2006

    Magologozi...nimependa point yako with evidence...it is the ability to understand that matters...maana blog sio formal site ni someone's own interest and he doesn't need to be formal if he does not wish!!So...kama mnataka kukosoa how mtu anaexpress interests zake hapo mnakosea!!You want formal writings, read Ipp media etc...that's where the news is. You can give message of making things better but it depends where!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...