mwalimu julius kambarage nyerere. naomba nitoe hoja binafsi kuwa kumtaja mwalimu kama 'hayati' ama 'marehemu' ni kupunguza utukufu wa jina lake kama ilivyo kwa watu wengine maarufu duniani. wazo ni kwamba tumtaje tu kama yu hai - naomba kuwakilisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. sasa naona michuzi, unakwenda mbali katika mtazamo wa mambo. hebu niambie kwamba unataka watu tujaze hili folder tukiangalia maisha ya mtu ambaye hayupo.

    bwana michuzi mimi ninapenda kukuambia kwamba , maneno hayo hayakuwepo kwa bahati mbaya.yaliwekwa makusudi kwa wale watu ambao kwa mikono au kwa kitendo kilichoonekana na umati wa watu kwamba walikufa na baada ya kufa walizikwa, na hii inawajumuisha pia wale waliopotea lakini ambao hakuna utata kwamba walikuwapo eneo fulani kwa shughuli fulani hapa nazungumzia watu kama mashujaa wa vita. hatuna hakika kama aliyeandikwa kwenye kiegezo cha kaburi ndiye aliyelala ndani. lakini tumethibitisha kwamba alikufa,

    turudi kwa alomaarufu marehemu au hayati mwl.nyerere. suala lake ni rahisi kama nikiangalia utangulizi wangu hapo juu. mwalimu alikufa na kwa kweli sio suala la siri au lisilojulikana hasa kwa wale ambao tulikuwapo duniani siku ake za uhai tunasema kwamba tuliona kweli kafa na watu walimuaga.ninachotaka sema hapa ni kwamba hadi kufikia hatua hiyo basi anatosha katika heshima hiyo ya uhayati na si vyenginevyo.

    ukitaka turudi kwenye suala la kumtambua kama vile yupo hai,labda ungeshika kalamu na kutuambia kwamba ulikuwa unamaanisha nini kusema hivyo au unataka kutupeleka kanisani ambapo hadi sasa hawajatoa jibu juu ya lile wazo la binadamu kutukuzana. kwa kweli tusifike huku,mungu alitoa na ametwaa.katika jina lake tumsifu............amin.

    ReplyDelete
  2. Kati ya picha za Mwalimu ninazozipenda hii ni mojawapo. REST IN PEACE MWALIMU.

    ReplyDelete
  3. brother michuzi samahani kwa kutokukubaliana na wewe.
    lakini si kila mtu natakiwa kumpa heshima hayati nyerere kama unavyofikilia.
    mimi binafsi sina cha kumshukulu huyo jamaa,hivyo naona aitwe marehemu kama wengine tu.

    ReplyDelete
  4. Michuzi,

    Nadhani huu "ushabiki" wa marehemu mwalimu unataka kutufanya tuwe vipofu wa ukweli wa mambo.

    Hebu tutajie watu maarufu wengine waliofariki ambao hawaitwi marehemu ... (the late ...).

    Ukifariki ukiwa unaheshimika duniani, bado heshima yako inabaki... hata watu wakikuita marehemu, kwa sababu marehemu haina maana mbaya, inaonesha ukweli wa mambo tu kwamba haupo nasi tena kwenye dunia hii.
    Asante

    ReplyDelete
  5. Hata ukiitwa Mtume au Mtakatifu, haitabadili mtazamo wa mtu dhidi yako. Kwa mantiki hiyo, jina marehemu au hayati kama walivyosema waungwana hapo juu, halishushi wala kupandisha heshima ya Mwalimu kutegemeana na mtu mwenyewe anavyomchukulia Mwalimu tangu awali. Binafsi, ninae heshima kubwa sana kwa marehemu Mwalimu Nyerere. Mungu amlaze mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  6. sina kawaida kuingilia mjadala, lakini huu, hasa kwa vile nimeanzisha mwenyewe, naomba kujitoma.

    anony wa 7:02:30 pm umesema nikutajie watu maarufu. naomba nikupe mtunzi william shakespeare, ama julius ceaser ambaye katika kumfasiri mwalimu hakumwita hayati ama marehemu. na hapo naogopa kutaja mitume ambao tunao kiimani tu. naomba kutoa hoja

    ReplyDelete
  7. Kwa MUNGU hakuna mkubwa wote tu sawa tu. MICHUZI sio naomba kuwakilisha, kumwakilisha mtu ni wakati yeye hayupo unafanya kwa niaba, Kiswahili sahihi hapa ni naomba kuwasilisha, kuwasilisha ni kutoa kitu. Tukikuze Kiswahili chetu ili tusiwapotoshe wanaojifunza

    ReplyDelete
  8. Mi binafsi hilo neno 'MAREHEMU' au 'HAYATI' yaani siyataki kabisa. Haijalishi mtu ni wa aina gani lakini kwa vile alishakuwa MTU kwa kweli sidhani kama inapendeza kumuita HAYATI/MAREHEMU. Lakini ukweli ni kwamba hii ya NYERERE it is too too too much yaani hata kanisani kiti chake bado kipi kwanini wanamtukuza hivyo JAMANI. Ila kama unaangalia vizuri na kufuatilia vizuri - hakuna sehemu waliyosema Marehemu au Hayati Julius Nyerere - mara nyingi huwa - Hayati baba wa taifa.

    ReplyDelete
  9. Kwa mujibu wa baraza la kiswahili la taifa BAKITA maana ya neno HAYATI ni mtu ambaye hajafariki, hili neno linatokanana kusharabu neno HAI, kwa hiyo Nyerere si hayati kwa sababu ameshakufa tayari, ila tukisema Hayati Mwinyi, Hayati Mkapa au Hayati Kikwete ndio tutakuwa tunapatia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...