dar yazidi kupendeza siku hadi siku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hilo geti ni automatic au?

    ReplyDelete
  2. Bia moja shilingi 4000 hapo duh!

    ReplyDelete
  3. EEEhh bwana hii hotel hivi kikwete alikuwa aiseee hawa taifa stars dooh kumbe dar pame hapana cynthia ni mzuri nimechoka na uteuzi wa waislam kumbe bunge la sasa limejaa mimi naona hakuna haja ya kubishana tena siku hizi bongo watoto wengi tena asee hili golofa poa ingawa taifa stars wameshinda inabidi ukimwi hauta isha kabisa kama condom hazita kwanini hatujapata habari za mauaji ya detroit ya hawa michuzi tuna enjoy saa hii blog yako lakini jaribu wangetafuta watoto wengi wa sekondari ili kukuza mpira wa asanteni wote.

    ReplyDelete
  4. Njoroge Musyoka wewe ni MSANII. Hongera!!! Revd. EVM

    ReplyDelete
  5. kweli ni pazuri hapa.
    je umeme upo? au mgao mbele kwa mbele?
    Dunga

    ReplyDelete
  6. Jamani huyo Njoroge MSANII kwa kwenda mbele....unachanganya habari kwa kwenda mbele...chumvi ,sukari,kunde,chapati,kaimati....yaaani kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  7. i agree with you people, bongo looks great from that angle.but like human beings looks should be complimeneted with brains and tabia.

    good looks bila umeme wa kuendesha uchumi ni kama mwanadamu bila damu, kwa maana kwamba atakufa.nadhani mifano hii inaeleweka vyema kwa watanzania wenzangu, kuliko ningetolea mfano wa aina nyingine.umeme, umeme na umeme!!!bila umeme tunakufa kifo cha pole pole.tunashindwa kufanya installation ya capacity ndogo kiasi hicho, let's say 600 MW, je tungeambiwa 6000 MW ingekuwaje, mgao ingekuwa balaa, 30 minutes per day.that's a conservative estimate to be honest with you.

    i think the foreign investor who poured his millions in the kilimanjaro hotel project [above], is just one of the many who could be regretting at the moment.how are they going to recoup their investment funding kwa mtindo huu wa mgao wa umeme?

    this country is almost crippled, i'm telling you fellow tanzanians, we should wake up and start taking these matters more seriously.

    tuamke, tuamke usingizini.kama serikali imelala, basi nayo tuiamshe, ninachokiona mimi ni kwamba Tanzania hatuna sera thabiti ya nishati.na vyombo vya habari navyo ndiyo ovyo ovyo kuliko hata hao polisi wanaochukua rushwa ya shilingi 1000, upuuzi mtupu, you dont question the government when it errs.sifa tu hata zisipostahili, mnajipendekeza kama watoto wadogo wanaotaka kupewa lamba lamba.

    tatizo la umeme halijaanza leo jamani, tusidanganyane, kama lilivyo tatizo la maji, miaka 45 tangu uhuru Dar Es Salaam haina maji ya bomba.halafu tunapigiana domo maisha bora kwa kila mtanzania, sijui ari mpya, kasi mpya nguvu mpya, labda katika ndoto huenda ni kweli, lakini katika maisha ya kawaida that's crap, no matter ideology ya mtu iko vipi.

    muda mfupi kabla ya uchaguzi wa mwaka jana Oktoba 2005, tulianza kupewa longo longo zisizokuwa na kichwa wala mkia, ohh sijui transformer ime-crash kutokana na overload, oh sijui ifikapo mwisho wa mwezi fulani tatizo la umeme litakuwa historia.......longo longo ndefu.

    hivi huu upuuzi tutauvumilia mpaka lini?serikali inajua wazi kwamba umeme ni swala nyeti kwa watanzania, licha ya ufukara wao kwamba hawatumii cookers, microwave, na acs, lakini wanahitaji umeme kwa maisha yao ya kila siku iwe nyumbani au kibiashara.

    leo hii mwulize waziri wa nishati akupe jibu la uhakika haya matatizo yataisha lini, hawezi kukupa maelezo kamilifu.atasingizia mvua, na mtera iko almost empty,.

    sasa kama wanajua mvua ni tatizo, kwanini tusitafute vyanzo vya umeme mbadala?

    mimi naudhika sana, ingawa labda hilo halisaidii, lakini tanzania inazidi kuumia, kama tulishindwa maendeleo ya viwanda miaka ile, tulikuwa na nafasi nzuri ya kujiimarisha katika information and communications technology, tutawezaje kwa hali hii.

    huenda sisi wengine ni vihere here, baadhi yetu hatuoni kama hili ni janga la taifa.nilitegemea rais na serikali yake wangekuwa wametangaza rasmi kuwa ni janga la taifa mpaka sasa.lakini walaaa!!!

    tuwe na uchungu na nchi yetu, hii mambo ya umeme na tanesco ina historia ya rushwa mbaya sana.tena inanuka vya kutisha, tukirudi nyuma kuna miradi ya kijinga kama iptl, songas na mambo kama hayo.

    ungetarajia kwamba watu watabadilika, lakini wapi bwana, siyo watanzania hao.ulafi mbaya sana unaizingira nchi yetu, mimi ninachojua ni kwamba incompetency, corruption na ulafi ndiyo vinakwamisha maendeleo ya nchi, lakini Tanzania siyo masikini hata simu moja.

    Lakini ipo siku yenu nyinyi mnaojenga ughaibuni huku mkibomoa nchi, ipo siku mtaadhibiwa, iwe hapa duniani au huko tusikokujua.umeme, umeme na umeme.

    that's the bottom line, let's solve this problem kabla ya kuongea mambo ya ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya.slogans dont run the economy, it's about policies and committment.

    ReplyDelete
  8. sio yeye jamani, lazima kabastuka huyu!!

    ReplyDelete
  9. Ni kweli huyo anoymous (2:59 pm) hapo juu ameelezea kinagaubaga matatizo yanayolikumba taifa letu.
    watu tunashindwa kuelewa kuwa majengo mazuri bila miundo mbinu ya uhakika yanakuwa ni bure tu
    a) umeme-nashangaa ukuiongea na watu wengi wanasema tuna maendeleo sana siku hizi. Labda ya mtu mmoja mmoja lakini sio kama taifa
    b) maji-hivi kweli mpaka akina Jey Z wanakuja kuchukua ujiko na kuonekana kuwa wanatueleta maji?? Tena hapa tunaongelea Dar es salaam, huko mtwara sijui kutakuwaje
    c) elimu siku hizi hupati bila ya kuwa na pesa-elimu imezidi kuwa duni
    d) afya-vile vile bado hairidhishi, waganga hawatoshi na hao wachache waliopo halipwi vizuri-wanabakia kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa.
    e) UZURI WA MAJENGO SI MAENDELEO-hayo ni mendeleao ya kijujuu tu-tuamke jamani-huo muda wa kushangaa majengo umepitwa na wakati-tuanze kuzumgumzia maendeleo ya kweli.

    ReplyDelete
  10. HUYO anoymous (2:59 pm)KASEMA UKWELI KABISA. YAANI VIONGOZI WETU HAWANA UCHUNGU KABISA NA ILE NCHI NA WATU WAKE.VIBIASHARA VYA SALON ZA KIKE NA KIUME VYOTE VIMEKUFA,BIASHARA BARAFU NK. NATAJA HIZI KWA KUWA NI ZA MTANZANIA WA CHINI KABISA.VIONGOZI WALIKUWA WANALIJUA HILI TANGU SIKU NYINGI, WANAILA TANESCO TU, KUIINGIZA KWENYE MIKATABA GHALI NA YA KIPUMBAVU KAMA IPTL,NET GROUP NK. NA HIVI MAJUZI KAMPUNI YA KITAPELI YA MAREKANI KUSAIDIA JENERETA..... YAANI NI UWOZO MTUPU.
    NA WEWE MICHUZI SIJAWAHI KUKUONA UKIELEZEA TATIZO LA UMEME WALA MAJI KWENYE HII BLOGU YETU. WEWE NI KUWAWEKA WATU WAKILA FUTARI VITU AMBAVYO HAVITUSAIDII WALA SI VYA MAENDELEO YOYOTE, WAKATI WEWE UNAJIDAI NI MPENDA MAENDELEO.MAENDELEO NI KWA VITENDO SIO KUJISIFIA!!!ONYESHA NJIA WANA BLOGU WATAFUATA.

    ReplyDelete
  11. NASAPOTI MTOA MAONI WA PILI HUKO JUU, BWANA HAPA MLALAHOI KAMA MIE NAINGIA KUCHEKI TU. AU IKITOKEA KAMA KUALIKWA KWENYE SHEREHE HIVI KAMA NILIVYOBAHATIKA KUALIKWA KATIKA ARUSI YA SYLVESTER CHEYO HAPO NDIO NILIJIPIGA BIA ZA DEZO TANI YANGU. MAANA KWELI BIA MOJA ELFU NNE. WAKATI NIKIENDA USWAZI KWA KIASI HIKI NAPATA BIA KAMA TATU HIVI NA CHENJI YA KUNUNUA UNGA NA MCHICHA WA KUPELEKA NYUMBANI INABAKIA VILE VILE.
    HAPO KEMPISNSKI BWANA TUWAACHIE WENYEWE KAMA LIUMBA, ALBAT MARWA, PETER RUPIA NDIO KWAO HAPO WAZEE WAZIMA NA MARA KWA MARA WANAONEKANA HAPA HASA PETER NA TOTOS WAKE YULE WA SHOMBE HIVI IRENE, NIMEMWONA SANA HAPA. NA KWENYE ARUSI YA SYLVESTER CHEYO PETER NA IRENE WALIMWAGA RAZI KWELI, TOBAAAAAAA WALIPENDEZA SANA, HONGERENI SANA, WENYE WIVU WAJICHONGE TU. MHESHIMIWA MICHUZI TUNGEFURAHI SANA TENA SANA KAMA UNGETULETEA HAPA BULOGUNI SASA PICHA YA PETER NA IRENE. AHSANTE MHESHIMIWA.

    ReplyDelete
  12. kawaida taratibu za mahoteli kama haya ni kwamba zipo kwa ajili ya business communities, wageni,wawekezaji,watu wenye company accounts za kikweli kweli, hazijatengenezwa kwa ajili ya mtu yeyote tu kwenda kutanua na ndio maana wanaweka bei za namna hiyo ili kuchuja, na tukumbuke wao wenyewe hawaoni hasara sababu wana uhakika na wale walengwa wao hata kama wachache.
    sehemu nyingi za ughaibuni huwezi kukuta mtu kaamua tu akapozi sheraton, au kempinski kunywa bia hata awe ana pesa kiasi gani, labda tu kama ana miadi au shughuli maalumu inayompeleka pale, kuna sehemu nyingi tu za kufanya hivyo kulingana na mazingira, kama vile ilivyo bongo, hivyo basi kabla ya kuanza kulalamikia bei zao inabidi tuelewe mambo kama haya.

    ReplyDelete
  13. Anonymous 2:59:27 PM Kwa kweli umeongea point sana, lakini ndio ujue sisi watanzania tuko nyuma kiasi gani, kwani kuna mtu aliona kwamba ulichoongea hakina maana na akakipinga, sijui hii nchi itafika wapi na watu kama hao. Wewe jinsi hii nchi inavyoendeshwa inakuuma kama inavyoniuma mimi na kwamba waandishi wa habari ambao ndio wangekua mstaru wa mbele kushikia bango swala hili, lakini wao wanamuuliza maswali rais anayotaka kuulizwa wakati hali ya nchi hairidhishi kabisa. Longolongo imezidi na hakuna jambo la maana linalofanywa. Naweza kusema jambo la maana ni ile tume ya kuchunguza wale polisi na ujambazi kupungua kidogo, lakini ukija kwenye maswala yanayohitaji vichwa, ubunifu, na kujituma kwa hali ya juu, nafikri viongozi na waandishi wa habari wanatuangusha sana. my email address is concomitant13@yahoo.com, twaweza wasiliana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...