nilivutiwa na usanii huu kwenye ukutua wa nyumba moja nyu yok nadhani barabara ya 50 hivi, karibu na redio site. ingekuwa bongo sijui ingepokelewaje...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hivi michuzi, hizi safari "mnazomsindikiza" mheshimiwa majuu huwa hamuoni kuwa zinapoteza fedha ambazo zingeweza kuwasaidia wananchi? Kwa mfano hiyo safari yenu ya marekani, ukiachia wafanyabiashara waliojilipia wenyewe, na sijui kama walijilipia wenyewe maana wengi wao walitokea mashirika ya umma, kwa hiyo ni fedha za serikali. hivi hamuoni kama hizo hela zingetumiwa kwa manufaa zaidi hapa bongo? tunaambiwa kuwa kila mmoja wenu tiketi yake tu ni millioni nne, hoteli ni laki nne kwa siku na mlikaa siku ngapi vile? Kama ni kumi ukichukulia nauli, malazi na chakula bado hapo hamjalipwa posho zenu, hivi ni dola ngapi kwa siku? hivi sikosei kama kila mmoja wenu alitumia millioni kumi kwa kuja kusindikiza Mhe, raisi akiongea UN, hivi kweli tanzania tupo matajiri kiasi hicho? tunaambiwa kuwa raisi anasafiri na ofisi yake nzima waandishi, wapiga picha, washauri kibao? hivi hao maofisa waliopo ubalozini ambao tunawalipia mamilioni ya hela kuwepo wanakuwa na kazi gani? sisi ni nchi maskini duniani, ingawa tunataka kuishi kama vile tupo sawa na rais wa marekani yenye utajiri mkubwa. hivi millioni kumi uliyotumia wewe, na nasikia mlikuwa karibia na watu hamsini hapo ni billioni tano hizo bado matumizi mengine, hivyo hizo hela tungewapa mikopo wanafunzi wangapi wa chuo? kwa wewe tu ni wanafunzi kumi wangepata mikopo, waliopo sekondari na msingi je? tumshauri Rais hizi safari zake pamoja ni kuwa ni za msingi aangalie msafara wake anaokuwa nao. SISI NI NCHI MASIKINI, TUWAKUMBUKE WANYONGE NA SIO KUPENDA MATANUZI YASIYO NA MSINGI

    ReplyDelete
  2. mjomba inaonekana uko ughaibuni muda mrefu sana. siku hizi bongo ukikosoa jambo unatakiwa utoe na njia mbadala. katika hili ungesema rais atembee na watu wangapi na bajeti iweje, ama asitembee kabisa. vile vile tambua kwamba kila senti imo kwenye bajeti ya ofisi yake, na mtu kama jk ambaye amekuwa waziri wa mambo ya nje kwa takriban miaka 10 hafanyi hivyo kwa hamu, bali budi. hivi tunavyoongea anajiandaa kutembelea nchi kadhaa za asia mwezi ujao. sijui asiende huko ambako pamoja na mambo mengine anapata dili kibao za uwekezaji na biashara, vile vile anatangaza nchi. wabongo hebu acheni kujifanya kujua/kukosoa kila kitu. hamna jema? kila jambo mkosoo, kila jambo sio sawa. sasa mnataka nini? ah, haya basi jk anazulula kila siku, sasa we unasemaje? jinyonge basi tujue moja. Lohhh! mnaboa sasa...

    ReplyDelete
  3. Naona hukunielewa, mimi sikatai Rais yeye kwenda nje, lakinu huo ujumbe mkubwa ni wa nini? anahitaji kwenda na watu si zaidi ya kumi, watu arubaini au hamsini wanaenda kufanya nini? Hivi mmeweza kuchambua kuwa hizo safari zake zimezaa matunda kiasi gani? Mnazungumzia ameleta wawekezaji, kumbukeni kuwa huku biashara si ubabaishaji, watu wakizungumza inabidi kufuatilia na proposals nk. watu huku wanataka vitu tangibles. Sasa sisi ni usanii tu ndio umetujaa, tukirudi tunadanganya wananchi eti safari imekuwa na mafanikio na tumepata wawekezaji. Hebu tuleteeni takwimu na matokeo ya misafa yote iliyotumia fedha za serikali halafu mtuambie kuwa muwekezaji huyu alipatikana kutokana na safari ya rais au waziri mkuu na bila kuwepo huo msafara basi huyo muwekezaji asingepatikana. Hivi nchi zote zilizopiga maendeleo kuoka katika umasikini zilipata wawekezaji kww kupitia misafara ya Raisi. Hebu tujifunze kutumia technology katika utendaji kazi wetu. Hatupati fedha kwa rais kwenda nje, Musevereni hajaenda nchi mara nyingi kama JK na Uganda ni nchi inayopata misaada per capita mikubwa kuliko sisi. Usituambmie kuwa kuja General Assembly kutoa speech alihitaji kuja na wabunge na wasindikizaji wengine arubaini au hamsini vile na hiyo ni idadi ukiachia wafanya biashara hao mnaosema wanaleta wawekezaji, tuende na wakati. siku hizi kuna video conference, kuna webcast nk. deals siku hizi zinafanyika kupitia mitandao. Mimi sina sababu ya kujinyonga, maana wivu sina, ninachohofia ni pesa zetu kutumika vibaya at the expense ya walala hoi kukosa mahitaji muhimu.

    ReplyDelete
  4. For your information alikuwa na watu 90 toka Bongo acha waliotoka ubalozini kama 10 na ushehe.
    Wengine eti kupiga picha kama hizo ambazo naamini kilichomvutia michuzi kama alivyosema ni ngono si jingine. Alngalia bwana weka picha zenye kusaidia jamii siyo kujifunza manufaa si kila ukionacho basi ukitoe. Basi mbona hujaweka picha za wale akinadada wanaoonyesha nyeti zao ni kujiingizia vidole wenyewe kwenye mabaa maalum?? Naamini huko nako ulifika kama siyo basi siku ukija tena Amerika nitakupeleka ili uwapelekee wajomba zako na familia yako tu.

    ReplyDelete
  5. michuzi wee mhuni wewe!!!

    ReplyDelete
  6. Huyo anon wa kwanza ameongea mambo ya msingi sana. Halafu huyu anon wa pili bure kabisa, yaani ana-crash point za mwenzake kwakutoa point pumba kabisa, maan au na wewe ni mmoja wapo wa waliotumia mabillioni ya serikali katika hizi safari nini?

    Umefika wakati sasa watanzania waanze kuhoji ufujaji wa fedha wa namna hii. Kwanza returns za hizi safari za kutafuta wawekezaji ni kubwa kiasi gani? Wawekezaji wenyewe wakija wanapata Tax holiday ya miaka mitano then baada ya hiyo miaka mitano wanabadili jina tena na wanapata another 5 - year Tax holiday! (Sheraton- Royal palm- Movenpick!).

    PRIORITIES! Priorities ndugu zangu, nadhani kuna vitu vingine vya muhimu zaidi ambavyo vingeweza kufanyika kwa manufaa ya umma na hayo mabillioni yalitumiwa na watu wachache katika hizi safari (Elimu, afya, umeme etc). Viongozi wetu tunaomba mtuonyeshe uzalendo kidogo jamani. Hivi Mwalimu katika urais wake alikuwa anasafiri na watu wangapi?

    ReplyDelete
  7. michuzi acha uhuni, mambo gani sasa haya

    ReplyDelete
  8. Wale wale walioshiriki kuuza vya umma ndio wale wale akina Bukuku wa Ikulu!

    ReplyDelete
  9. anon wa 5:56 mwambie ukweli huyo anon aliyesema kuwa ujijonge inaelekea yeye ndo kibaraka wa kikwete maana anavyomtetea utafikiri analipwa hela( inaelekea maana mi sijui) ukweli unabaki kwamba hela zetu za sisi watanzania zinatumiwa vibaya, halafu asante ndugu kimasomaso kwa kutupa hizo figures za watu waliokwenda, hivi jamani sisi kweli tuna hela ya kupeleka watu 90 nje ya nchi. Hivi huyu kikwete anafikiri Tanzania ina hela au anawajali kweli hawa wananchi wake,? maana haya mamilioni yaliyotumika kwenye safari mi nakwambia yangesaidia hata asilimia kidogo uchumi wetu na watu wake. hawa viongozi ni wa kutimuliwa kabisa

    ReplyDelete
  10. Ninashukuru kuwa watu mmeona hoja ya msingi kuwa fedha za Tanzania zinatumiwa vibaya kwenye hizi safari za Raisi. Cha kusikitisha zaidi ni kuwa kama alivyosema ananymoius wa 12.24.40 ni kweli kuwa JK anasafarinyingine kwenda majuu, basi nakuomba ndugu Michuzi hebu umuonyesha haya mawazo ya sisi wananchi. Aende hizo safari zake lakini apunguze ujumbe. Hivi akiambatana na watu kumi tatizo ni nini? yeye ni raisi tu tena ataheshimika zaidi kuwa anajali nchi yake kama atakuwa na ujumbe mdogo. fadhila za yeye kulipa ni kwa sisi wananchi sio hao wabunge wake. Unajua wafadhili wanatushangaa. Leo tunashindwa kufadhili wanafunzi chuo kikuu eti hatuna hela, lakini Rais anabebeshana na watu kedekede ambao wanaenda tu kutalii. Hivi priorities zetu zipo wapi? JK hebu uwe na huruma na hii nchi. Michuzi nasisitiza tena hebu tafuta njia ya kumuonesha JK kuwa anachofanya ni kutuvunja moyo watu tuliomchagua kwa kura nyingi. Anatufanya tuanze kujiuliza kama kweli alistahili kura zetu. Asije akawa Raisi wa kwanza kutopewa term ya pili. Maana sasa hivi miradi mikubwa yote inayotekelezwa ni ya enzi ya mkapa, yeye hana jipya. atulize boli hapo nyumbani afanye kazi za maendeleo, ziara za nje amuachie waziri wake wa mambo ya ndani. yeye hawezi kuwa Raisi na waziri wa nje kwa pamoja.

    ReplyDelete
  11. labda ndugu zangu mmesahau kuwa JK amezungukwa na wahuni katika maamuzi na ushauri. eti Cisco Mtiro, yule aliyewahi kugombea ubunge Temeke akaangushwa na Mrema, sasa ndiyo mkuu wa itifaki (Protocal). Eti January Makamba, na wengineo, hao tu ni matatizo tosha.
    Pili mnamwambia Michuzi wakati mnajua wazi kwamba Michuzi ni mmoja wa wahuni walioizunguka Ikulu. ukitaka kuhakikisha hilo, angalia taaluma yake anavyoitumia, kaitka 70% ya picha zake ni za kihuni. Amejaza propaganda za kuwadanganya wanannchi, na anasikia raha kuweka picha zisizo na maana ili tu wahuni watoe matusi nk. au atatoa picha za kufagilia, hata pailpo na uzembe.
    tatu mnalalamika eti JK alichaguliwa kwa kura nyingi, Nyie kuweni macho. Ni taifa gani lenye multparty, mtu akashinda kwa 80% ya kura zote? hata Nyerere hakuwahi kushinda kwa asilimia hizo, na alikuwa anapigiwa kura akishindanishwa na kivuli, tena ni mtu maarufu kuliko mtu mwingine Tanzania.
    Wananchi pia mnadiriki kudanganywa eti kuna siku 100 za utukufu wa JK!!!!!!!! ajabu sana! hata Yesu hakuwahi kupewa siku 100 za mafanikio yake, Mtume Mohammad S.A.W hakuwahi kupewa siku 100 za mafanikio yake, leo hii mtoto aliyelelewa katika makucha ya ubadhirifu, na akatulizwa sehemu bora ya kutafuta wageni ili waje wautafune uchumi wetu kwa miaka 10 mfululizo, akiwa waziri wa nje, eti leo hii awe malaika!!! Ajabu sana.
    kwanza angalia baraza lake lilivyojaa, nchi changa ina mawaziri zaidi ya 50, wote hao wanafanya nini?
    jana kabadilisha baraza, tukategemea atapunguza utitiri wa mawaziri, kumbe kwabadilishia majina tu, na ulaji ni ule ule.
    JK, mzimu wa Mwalimu utakutokea ndotoni uweweseke, shauri yako.
    Uliambiwa umri haujafika, sentesi ile ilikuwa na maana. Wewe kwa papara zako ukadhani unaambiwa umri wako wa kuishi duniani, kumbe maana ilikuwa huwezi kutuongoza kwa masifa na kuwalaghai wananchi kwa kununua vyombo vya habari na wapiga picha kama akina Michuzi.

    ReplyDelete
  12. Ingekuwa Bongo wabongo wanagejazana pale kuipigia nyeto.

    ReplyDelete
  13. NAUNGANA NA WOTE WANAOSEMA HELA YA TAIFA INATEKETEA.MBONA KUNA MAMBO MENGI TU MUHIMU JAMANI,MFANO MABASI YA WANAFUNZI,MIKOPO CHUO KIKUU,WAMACHINGA NK.MIMI NASEMA JK NI LIMBUKENI NA KAJA KUPONDA MALI NA WATANZANIA TUTAJUTIA UAMUZI WETU WA KUMUWEKA MADARAKANI SIKU SI NYINGI.
    HAKAI OFISINI KUBUNI MIKAKATI WALA NINI KIGUU NA NJIA TU YANI HUYU JAMAA NI HOPELESS KABISA.I HAVE LOST MY TRUST IN HIM TOTALLY AND COMPLETELY.KWANZA NAONA HATA BABA WA TAIFA HAKURIDHISHWA NAE NDIO MANA TOKA AMEINGIA MADARAKANI NI MIKOSI JUU YA MIKOSI.ANA NUKSI HUYU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...