jk akiwa na makamu wa rais na waziri mkuu na mawaziri wadogo waliobadilishwa wizara leo
mbele kushoto ni hezekiah chibulunje anayehamia wizara ya viwanda na biashara akitokea kilimo anakobadilishana na david mathayo david (mbele kulia). nyuma shoto no dk. batilda buriani anakwenda mipango, akibadilishana na salome mbatia pale wanawake na watoto. mwenye njano nyuma ya jk ni dk. emmanuel nchimbi anayetoka habari, utamaduni na michezo na kubadilishana na daniel nsanzuganko, anayemfuatia. bernard membe anakwenda nishati na madini akibadilishana na dk. lawrence masha mambo ya ndani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kazi kubwa bado ipo mbele yetu watanzania.Ndani ya miezi kama tisa tu baraza la mawaziri limeshapanguliwa?!!Kwa bahati mbaya mabadiliko kama haya huenda sambamba na gharama kubwa za kuhamishana nk.Nani analipa gharama hizi?

    ReplyDelete
  2. Usihofu Jeff gharama hizi fwedha kila mara ipo, kodi ya Wadanganyika. Tulipoamua kuacha kuwafadhili wanafunzi chuo kikuu tulijua mambo kama haya yanatokea. Serikali yetu inafanya kazi kukliko awamu tatu zilizotangulia na huu ndio moja ya mkakati wakuonyesha tuko serious.

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha sana kuona mambo kama haya yanatokea, hivi hizo fedha tunazo saana kufanya vitu kama hivi??? Jaman hivi tukumbuke hatuna umeme wala maji, kwanini tusingetekeleza hayo kwanza kwa pesa za ku train hawa mawaziri, na mabadiliko yao??? Michuzi peleka malalamiko haya kwa J.K.

    ReplyDelete
  4. masha angetakiwa aondoke manake tangu mapema alishaboronga kwenye mikataba huko nyuma,sijui kwa nini watu wanabebana hivyo yaani mpaka unachoka.jamani tanzania tunaenda wapi?????

    dr batilda buriani ameonyesha kukomaa na kwa kweli nafikiri anajitahidi ndio mana amepewa wizara ngumu kidogo.

    na salome mbatia ni kama demotion kwake anatakiwa aangalie steps zake.

    hao wengine bado sijawajua vizuri ngoja tuone kama kuna jipya.

    god bless tz

    ReplyDelete
  5. Kuna bwana hapo alikuwa embassy hapa Ottawa kashika sana mabinti za watu maziwa akiwaliwaza kuwa atakuwa PM au Foreign Minister kaka yangu Bernard Membe namwona kwa nyuma pale kwenye picha na vigogo wenzie (Kamtesa sana mdogo wetu Upendo kuwa atamwoa na nini ) katuachia garasa sasa anatesa bongo kishikaji hili baraza zima lina players kibao .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...