Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. sheria ichukue mkono wake

    ReplyDelete
  2. Saa Monday, November 06, 2006 10:28:59 AM, Mtoa Maoni: mwita chacha

    Kwa miaka mingi Serikali imekuwa inawabeba Vigogo wanapojihusisha na uvunjaji wa sheria SASA MUHESHIMIWA DITOPILE AMEUWA KWA MAKUSUDI DEREVA WA DALADALA KISA AMEMGONGEA GARI? NATUMAINI KIKWETE KAMA ALIVYOSEMA SERIKALI YA AWAMU YA NNE HAITA MWONEA HURUMA YEYOTE ATAKAYE VUNJA SHERIA SASA TUTATHIBITISHA HATUA ATAKAZOMCHUKULIA SHEHE WA MZUZURI. INAKUWAJE UMWONYESHEE BASTOLA MTU ALIYE KUGONGA HATA KAMA HATAKI KU COMPLY? NAMBA ZA ILE GARI SIZILIKUWEPO NA DITOPILE SI NI KIBOSILE MKUBWA TU KWANI YULE DREVA ANGEKIMBILIA WAPI? SIONI SABABU YA KUTOA BASTOLA, KWANZA ANGEKUWA NI MLALAHOI KAFANYA HIVYO ANGEOZEA JELA LAKINI KWA SABABU NI DITOPILE ANAHOJIWA TU NA POLICE NA KURUDI NYUMBANI...? HALAFU TUNASEMA TANZANIA KUNA AMANI KULIKO KENYA? AIBU GANI HII? SAMAHANI NDUGU ZANGU KWA KU POST HABARI ZISIZO FANANA NA PICHA, HII HABARI YA MAUAJI ALIYO FANYA DITOPILE YANASIKITISHA SAANA, HASA UKIZINGATIA KUWA MUUAJI AMEMFANYIA MNYONGE KWA SABABU NDOGO SANA AMBAYO ANGEWEZA KUITATUA KWA AMANI!!

    ReplyDelete
  3. Saa Monday, November 06, 2006 11:24:08 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

    be fair michuzi


    Saa Monday, November 06, 2006 11:37:18 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

    MICHUZI: HUYO MUUAJI DITOPILE MBONA HUJA MLETA KARIBU TUKAMWONA VIZURI?


    Saa Monday, November 06, 2006 12:27:02 PM, Mtoa Maoni: Revd. EVM

    Michuzi kaka yangu, hivi kweli hii ni NGUVU MPYA na KASI MPYA ndo inataka viongozi wetu wawe wababe hivyo? Mara hawa wamepiga watu makofi, mara huyu anaua kwa BASTOLA, sasa huyu muuaji LAZIMA ahukumiwe kama muuaji, lazima akae rumande hadi hapo sheria itakapochukua mkondo wake!Lazima Rais amuwajibishe kwa kumtengua kuwa mkuu wa mkoa, kabla hajaua mkoa MZIMA. Inabidi Rais akawawajibisha viongozi wengine wenye tabia ya kupiga watu makofi kama ile iliyotokea kule Mbarali na Songea. Viongozi wajue kuwa cheo ni dhamana na wala wao sio miungu watu. Mungu AILAZE PEMA PEPONI ROHO ya MAREHEMU MBONDE. Amin


    Saa Monday, November 06, 2006 12:35:56 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Michuzi tupatie habari za Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw. Ukiwaona Ditopile Mzuzuri aliyemtwanga risasi Dereva wa Daladala kule Dar cku ya Jumamosi...nimemsikitikia sana Bro.Dito
    alishawahi kutolewa humu...
    http://issamichuzi.blogspot.com/2006/05/kigoma.html


    Saa Monday, November 06, 2006 3:44:02 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    mlio ughaibuni, mlizungumzia sana mauaji ya watz yaliyotokea marekani miezi michache iliyopita. mbona kimya kuhusu mkuu wa mkoa aliyempiga risasi ya kichwa dereva la daladala na kumuua? au kwavile ni mlalahoi basi hana haki manake tayari hadithi imeanza kuchezeshwa kwamba bastola ilifyatuka kwa bahatui mbaya. swali, ilifyatukia mfukoni kwa mwenye nayo? dereva alifanya purukushani gani hadi bastola ikatolewa? je, kiongozi wa serikali ni vipi alisahau usalama wa raia (abiria) waliokuwa ndani ya chombo cha usafiri? kama kweli tuna moyo wa dhati, familia ya dereva wa daladala ndiyo ya kuchangiwa!


    Saa Monday, November 06, 2006 4:03:11 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    WEWE CHUJA MAONI YANAPOGUSA VIGOGO ILA WENGINE WATAYATOA. YANA MWISHO.


    Saa Monday, November 06, 2006 4:30:20 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    NIMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA HABARI ZA KIONGOZI WA SERIKALI MKUU WA MKOA WA TABORA MHESHIMIWA DITOPILE MZUZURI KUMTWANGA RISASI DEREVA WA DALADALA NA KUMWUA. TAFADHALI TULETEE PICHA ZA HILI TUKIO.

    ReplyDelete
  4. kwa mara ya kwanza michuzi, angalau umeonyesha ubinadamu dhidi ya vigogo.

    ReplyDelete
  5. Kama hajafungwa maisha huyu, kikwete hitabidi amtoe babu Seya. Kwanini asining'ing'inizwe kama mwenzake Saddam. Muuaji mkubwa huyo

    ReplyDelete
  6. Ama kweli mamboyamebadilika Tanzania. Zamani magazeti yangepigwa marufuku kuandikia hizi habari.

    ReplyDelete
  7. naona michuzi umenogewa hadi unaweka picha dabo-dabo. tuachilie tutambe kwenye blog kupunguza majakamoyo.
    NYERERE AMKA UTUONE WANAO.

    ReplyDelete
  8. HII NI AIBU YA MWAKA.. HIVI NDIO TUTEGEMEE VIONGOZI WA NCHI YETU WASIOKUWA NA BUSARA KATIKA KUTATUA MATATATIZO MADOGO KAMA HAYA YALIYOMKUTA HUYU NDIO WATAWEZA KUTATUA MATATIZO YETU MAKUBW YA KIMAISHA? PIA INABIDI UTARATIBU MZIMA WA UTOAJI SIRAHA UANGALIWE UPYA. WASIOWEZA DHIBITI HASIRA ZAO AU WANAOHAMISHA HASIRA ZAO KWA WENGINE WASIPEWE KABISA.

    ReplyDelete
  9. kwakweli huyu wamtundike tu.

    ReplyDelete
  10. Bado Kinjekitile sasa kuonja segerea hiko vipi. Na yeye pia siana mtindo wa kutembea na pisto kutishia watu

    ReplyDelete
  11. Wakili mtetezi wa mshitakiwa kazi yake kubwa ni ku-confound ushahidi wa upande wa mshitaki. Mara nyingine wakili mtetezi hufanikiwa on legal technicality tu, licha ya ushahidi wa kweli! Yangu macho!

    Isije kesi ikapelekwa mbele ya korti ya maoni (injuction) kutafuta ukweli kama Athumani Ukiwaona Ditopile Mzuzuri ana hatia, kama kesi ya Hamza Aziz ilivyokuwa baada ya kumkanyaga mwananchi mmoja na kusababisha kifo chake, na Hamza Aziz kukimbia the crime scene.

    Hamza Aziz alinusurika kutokana na legal technicality eti kwa sababu Injunction Korti (chini ya Hakimu Mkazi Mkate) ilivuka its legal scope kwa kutamka kuwa Hamza Aziz aliua! Injuction Korti haikuwa Jaji mhukumu! Yangu macho!

    ReplyDelete
  12. Sijui sheria hila hili suala siyo la kufungwa maisha dito anatakiwa kunyongwwa kabisa hii wala haitaji ushaidi mkubwa nashangaa mawakili eti wannne wakati amefanya kitendo kweupe kabisa.

    Dito anajua vizuri sheria za nchi kuliko mtu yeyeto hiyo nafikiri sheria inatakiwa kumtembelea sawa sawa.

    ReplyDelete
  13. Michuzi, hivi Sekretariety ya Maadili ya Viongozi wa Umma bado ipo hai?Bi Hawa Ngulume(DC) alimchapa kibao Mwanakijiji na mpaka leo yupo kazini,wakati mwanakijiji anaugulia maumivu. Ditopile naye kaamua kumalizia kabisa kwa kuua mwananchi mlalahoi. Na kadri mahakama zetu zilivyo na utawala wa sheria uliolala,DITO kesi atashinda kwa kishindo. Hii ndio kasi mpya ambayo wanamtandao walituahidi wananchi?

    ReplyDelete
  14. Hili jambo ni la KUSIKITISHA na ni la AIBU KUBWA sana kwa nchi yetu. Rambirambi nyingi za dhati ziwaendee Ndugu na marafiki wa marehemu, MUNGU amuweke pema peponi.
    Haya yote yanasababishwa na kuwa na viongozi si wateuliwa na hata wakuchaguliwa wasiokuwa na elimu! Kwa muda mrefu sisi vijana tumekuwa tunashuhudia jinsi waliotutangulia (Ditopile type) wakipeana au kurithishiana madaraka kama vile ni UFALME. Eti wanaita Democracy!?!?
    Muda ni huu Mr. JK, waswahili walisema "Nyota Njema Huonekana Asubuhi" fanya hayo mabadiliko, una choice kubwa saana ya wazalendo ambao (Qualified)na ni watendaji fika wa kazi.
    Do the MATH MR.PRESIDENT.

    ReplyDelete
  15. ISIJE AKAPEWA HUKUMU YA KWENDA JERA LAKINI AKAWEKWA KATIKA SAFE HOUSE KWA KIPINDI CHOTE CHA HUKUMU YAKE HII INAWEZEKANA KWA KULINDANA TU. AKIPELEKWA JELA WATUONESHE AMEFIKA JELA. HIVI NA KESI YA ZOMBE IMEFIKIA WAPI? HATUJA SAHAHU MICHUZI TUPE HABARI KAMILI ZA KESI ZOTE MBILI. ILI KUONESHA KUNA DEMOKRASIA MICHUZI TOA MAONI YANGU YAWE WAZI PIA ONDOA COMMENT MODERATION.

    ReplyDelete
  16. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  17. hili tukio nashindwa kulielewa!Ditopile inabidi kwanza apelekwe kwenye general psychiatric examination,anaweza kuwa mgonjwa huyu pia kuna uwezekano mheshimiwa anatumia madawa ya kulevya.

    ReplyDelete
  18. Wewe zemarcopolo unasema apelekwe wapi? ili ashinde kesi baada ya madaktari kuongwa na kuonesha vyeti feki kama ana matatizo na kuachiwa huru? aah huyu bana hasiachiwe kabisa wamezidi sana hawa watu. Kingine na ile kesi ya mauaji ya Zombe tunaomba ifuatiliwe hatujasahau kabisa watanzania na yeye ameua mtu huyo! Huyo ditopile kama watu wasinge muona kaua nina uhakika zaidi ya asilimia 200 angekuwa ana dunda mitaani. Ata kama akiachiwa huru ajue kwa MUNGU hawezi kuonga na kuachiwa huru kama ilivyo duniani hivyo hukumu ina msubiri tu.

    ReplyDelete
  19. Ditopile Ukiwaona wa Mzuzuri Mwinshehe !!! Kumbe wewe ni GAIDI namna hiyoooooooooooo ?????? Sasa nenda kabebe NDOO za vinyesi huku SEGEREA !! Hiyo yote ni LAANA ya wale uliowafanyia wake zako na baadaye kutamba eti wewe NI KIDUME CHA MBEGU !!!! Salamu kwa GAIDI mwenzio Mchizi ZOMBE !!

    ReplyDelete
  20. Kuna mtu amekumbushia kesi ya Marehemu Hamza Aziz, ambaye pamoja na yaliyotokea alishinda kesi, na zawadi yake alihamishiwa marekani, kikazi! JK hakuwa rais wakati huo,hamna haja ya kusema ni nani, haya mambo yalianza zamani jamani, tusianze kumlaumu JK wakati bado ni mapema kabisa, na hata kama hiyo ndio itakuwa outcome tukumbuke mambo ya kubebana yalianza from day one!

    ReplyDelete
  21. Hii ni noma,
    Ni kweli Mheshimiwa Ditopile angeweza kupandwa na mahasira kama ingekuwa ajali ya kufa mtu.Upo uwezekano Kepteni Mzuzuri angeweza kutoa mguu wa kuku kama dereva husika angeleta ubabe au matusi baada kufanya ajali ya kufa mtu.Bro Dito angeweza kuchukua sheria mkononi kama waliogonga gari lake walikuwa ni majambazi wenye silaha..
    Ni wazi tukio lenyewe halikuwa la "kufa mtu"...na wazi ile kutaka kuonesha ubabe ndio imepelekea mtu kufa...huu ubaunsa kautoa wapi ukiniuliza??inawezekana ni ktk ile kujiona sisi ndio wenye nchi yetu...busara japo kidogo tu ingetumika maafa kama haya yasingetokea...watoto wangapi wamebaki yatima,watoto wangapi watashindwa kwenda shule inabidi bro dito itabidi atupe taarifa...

    kwa upande mwingine aliyoyafanya mzee Ditopile(58) inatusaidia kutukumbusha jinsi gani wabongo hatupendani.hatuna mapenzi ya dhati miongoni mwetu...mimi sikupendi wewe na wewe hunipendi mimi kama mbongo mwenzako Kunidhulumu,kuniibia,kuninyanyasa,kunionea,
    kunidharau,kutonionea huruma,kunisaliti na mambo kama hayo ukinifanyia ndio unajiona mjanja..hata ukija kuwa mkuu wa mkoa huwezi kubadilika mwendo unakuwa ule ule hata uwe waziri mnene...wengi ktk viongozi hawana upendo wowote kwa raia.ni wazi kama kuna nchi ambazo viongozi wake wanatakiwa wawaenzi wananchi wao kama wana familia zao basi Tanzania ipo.nchi maskini kupita kiwango watu tumechoka hatuna matumaini...Njaa,dhiki,ujinga,ukimwi na maradhi mengine yanatusakama...kama mkubwa wa nchi yenye hali hii inabidi upendo wa hali ya juu uwe nao kwa raia wako.Ikifikia mpaka kiongozi unaua mtu ktk nchi kama hii kuna haja ya kwenda semina kujifundisha upya nini maana ya UONGOZI.

    Mi sio mahakama niweze kumuhukumu mtu,kisha sina ufundi ktk masuala ya sheria na kesi. Ningekuwa naweza kuongea na Mzee Ditopile ningemwambia asijifanye mbabe kwa mara ya pili au alete ununda mbele ya wabongo 37,000,000. Aongee na nafsi yake amuombe msamaha mwenyezi mungu,awaombe msamaha watanzania wote,awaombe msamaha wanafamilia Hassan MBONDE kwa “ukatuni” alioufanya.
    Mwenyezi mungu amrehemu ndugu yetu.

    ReplyDelete
  22. unajua hawa akina Dito ndio wanaona hii nchi kama vile wameikatia viza na sisi ni wakimbizi.sasa naona wakati umefika kila tone la damu ya mmlala hoi imwagikayo ,imwage pia damu ya hawa wanaojifanya MAGAIDI.Mimi nashangaa vibaka tunawachoma moto ,hivi Ditople imeshindikana nini siku hiyo ya tukio kumchoma moto,au ndio hivyo wabongo tunaogopa mlio wa bunduki?
    Lakini bado tuna uchungu sana na roho ya MBONDE wasirogwe Dito wamwachie maana patakuwa hapatoshi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...