huyu ndiye mbaga, mwanachama wa yanga. huwa hakopeshi mtu pale mambo yanapokwenda kombo. ana uwezo wa kuzozana na uwanja mzima kufikisha ujumbe, hata kama yanga ime
shinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Je huyu jamaa ni komandoo nini?

    ReplyDelete
  2. NJaa kali tu, hamna chochote.

    ReplyDelete
  3. mbona kavaa rangi za dam ya simba?

    ReplyDelete
  4. Hivi inakuwaje katika Tanzania ya Leo ya Serikali ya awamu ya nne Mkuu wa Mkoa Ditopile Mzuzuri anamfyatulia risasi mlalahoi anayetafuta riziki (dereva wa daladala) kisa amekwaruza gari lake? Je serikali yetu ya awamu hii inatupeleka wapi watanzania?

    ReplyDelete
  5. Kwa miaka mingi Serikali imekuwa inawabeba Vigogo wanapojihusisha na uvunjaji wa sheria SASA MUHESHIMIWA DITOPILE AMEUWA KWA MAKUSUDI DEREVA WA DALADALA KISA AMEMGONGEA GARI? NATUMAINI KIKWETE KAMA ALIVYOSEMA SERIKALI YA AWAMU YA NNE HAITA MWONEA HURUMA YEYOTE ATAKAYE VUNJA SHERIA SASA TUTATHIBITISHA HATUA ATAKAZOMCHUKULIA SHEHE WA MZUZURI. INAKUWAJE UMWONYESHEE BASTOLA MTU ALIYE KUGONGA HATA KAMA HATAKI KU COMPLY? NAMBA ZA ILE GARI SIZILIKUWEPO NA DITOPILE SI NI KIBOSILE MKUBWA TU KWANI YULE DREVA ANGEKIMBILIA WAPI? SIONI SABABU YA KUTOA BASTOLA, KWANZA ANGEKUWA NI MLALAHOI KAFANYA HIVYO ANGEOZEA JELA LAKINI KWA SABABU NI DITOPILE ANAHOJIWA TU NA POLICE NA KURUDI NYUMBANI...? HALAFU TUNASEMA TANZANIA KUNA AMANI KULIKO KENYA? AIBU GANI HII? SAMAHANI NDUGU ZANGU KWA KU POST HABARI ZISIZO FANANA NA PICHA, HII HABARI YA MAUAJI ALIYO FANYA DITOPILE YANASIKITISHA SAANA, HASA UKIZINGATIA KUWA MUUAJI AMEMFANYIA MNYONGE KWA SABABU NDOGO SANA AMBAYO ANGEWEZA KUITATUA KWA AMANI!!

    ReplyDelete
  6. Kwa miaka mingi Serikali imekuwa inawabeba Vigogo wanapojihusisha na uvunjaji wa sheria SASA MUHESHIMIWA DITOPILE AMEUWA KWA MAKUSUDI DEREVA WA DALADALA KISA AMEMGONGEA GARI? NATUMAINI KIKWETE KAMA ALIVYOSEMA SERIKALI YA AWAMU YA NNE HAITA MWONEA HURUMA YEYOTE ATAKAYE VUNJA SHERIA SASA TUTATHIBITISHA HATUA ATAKAZOMCHUKULIA SHEHE WA MZUZURI. INAKUWAJE UMWONYESHEE BASTOLA MTU ALIYE KUGONGA HATA KAMA HATAKI KU COMPLY? NAMBA ZA ILE GARI SIZILIKUWEPO NA DITOPILE SI NI KIBOSILE MKUBWA TU KWANI YULE DREVA ANGEKIMBILIA WAPI? SIONI SABABU YA KUTOA BASTOLA, KWANZA ANGEKUWA NI MLALAHOI KAFANYA HIVYO ANGEOZEA JELA LAKINI KWA SABABU NI DITOPILE ANAHOJIWA TU NA POLICE NA KURUDI NYUMBANI...? HALAFU TUNASEMA TANZANIA KUNA AMANI KULIKO KENYA? AIBU GANI HII? SAMAHANI NDUGU ZANGU KWA KU POST HABARI ZISIZO FANANA NA PICHA, HII HABARI YA MAUAJI ALIYO FANYA DITOPILE YANASIKITISHA SAANA, HASA UKIZINGATIA KUWA MUUAJI AMEMFANYIA MNYONGE KWA SABABU NDOGO SANA AMBAYO ANGEWEZA KUITATUA KWA AMANI!!

    ReplyDelete
  7. Huwa anaingia mechi bila kulipa kiingilio mlangoni.Dawa ya kukata domodomo lake ni kuhakikisha analipa kiingilio.Hiyo tu inatosha kumfanya akiingia atulia kwenye kiti uwanjani kama wachovu wengine wanavyotulia.

    ReplyDelete
  8. michuzi unapoomba radhi familia ya lowassa kwa matusi yaliyoandikwa na wadau basi uwe unaomba kila siku kwanye familia nyingi.kila mtu ana uchungu anapoandikwa.inauma sana unapopendelea upande mmoja tu na sio pande zote,be fair michuzi.

    ReplyDelete
  9. be fair michuzi

    ReplyDelete
  10. be fair michuzi

    ReplyDelete
  11. MICHUZI: HUYO MUUAJI DITOPILE MBONA HUJA MLETA KARIBU TUKAMWONA VIZURI?

    ReplyDelete
  12. Michuzi kaka yangu, hivi kweli hii ni NGUVU MPYA na KASI MPYA ndo inataka viongozi wetu wawe wababe hivyo? Mara hawa wamepiga watu makofi, mara huyu anaua kwa BASTOLA, sasa huyu muuaji LAZIMA ahukumiwe kama muuaji, lazima akae rumande hadi hapo sheria itakapochukua mkondo wake!Lazima Rais amuwajibishe kwa kumtengua kuwa mkuu wa mkoa, kabla hajaua mkoa MZIMA. Inabidi Rais akawawajibisha viongozi wengine wenye tabia ya kupiga watu makofi kama ile iliyotokea kule Mbarali na Songea. Viongozi wajue kuwa cheo ni dhamana na wala wao sio miungu watu. Mungu AILAZE PEMA PEPONI ROHO ya MAREHEMU MBONDE. Amin

    ReplyDelete
  13. Michuzi tupatie habari za Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw. Ukiwaona Ditopile Mzuzuri aliyemtwanga risasi Dereva wa Daladala kule Dar cku ya Jumamosi...nimemsikitikia sana Bro.Dito
    alishawahi kutolewa humu...
    http://issamichuzi.blogspot.com/2006/05/kigoma.html

    ReplyDelete
  14. Duh hawa ndio wanabishana na redio sometyms!!

    ReplyDelete
  15. sasa mbona kavaa Rangi ya simba!!! ana lolote

    ReplyDelete
  16. mlio ughaibuni, mlizungumzia sana mauaji ya watz yaliyotokea marekani miezi michache iliyopita. mbona kimya kuhusu mkuu wa mkoa aliyempiga risasi ya kichwa dereva la daladala na kumuua? au kwavile ni mlalahoi basi hana haki manake tayari hadithi imeanza kuchezeshwa kwamba bastola ilifyatuka kwa bahatui mbaya. swali, ilifyatukia mfukoni kwa mwenye nayo? dereva alifanya purukushani gani hadi bastola ikatolewa? je, kiongozi wa serikali ni vipi alisahau usalama wa raia (abiria) waliokuwa ndani ya chombo cha usafiri? kama kweli tuna moyo wa dhati, familia ya dereva wa daladala ndiyo ya kuchangiwa!

    ReplyDelete
  17. WEWE CHUJA MAONI YANAPOGUSA VIGOGO ILA WENGINE WATAYATOA. YANA MWISHO.

    ReplyDelete
  18. NIMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA HABARI ZA KIONGOZI WA SERIKALI MKUU WA MKOA WA TABORA MHESHIMIWA DITOPILE MZUZURI KUMTWANGA RISASI DEREVA WA DALADALA NA KUMWUA. TAFADHALI TULETEE PICHA ZA HILI TUKIO.

    ReplyDelete
  19. mfukoni kwa kiongozi yeyote bali ni kodi yetu na jasho letu. naomba uanzishwe mfuko wa kuaminika kwa ajili ya watoto wa marehemu. tena iwe akaunti itakayokuwa ikitoa kiasi fulani cha pesa kila mwezi. bora kuchangiwa na jambazi au malaya kuliko ditopile na mahasimu wake.
    kaka yangu mbonde, roho yako ni ushuhuda dhidi ya wakandamizaji.

    ReplyDelete
  20. ukishaonja nyama ya mtu, huachi. nae huyu katumia bastola hadharani, basi si ajabu kesho akatumia kwa jirani yake. dito baba, kesi utashinda ila picha ya marehemu akikusihi kabla hujaitoa roho yake, itakuongoza kaburini.
    nilielewa pale wanajeshi wa kiingereza walipopandishwa ndege kupitia v.i.p baada ya kumuua dada kwenye mojawapo ya hoteli za kitalii pembezoni mwa dar es salaam.
    ila sielewi pale kiongozi anapowageukia watu wake na kuwafyeka kisa taa ya gari. si ditopile peke yake aliyechukua hatua mikononi, wanajeshi nao ni tatizo wanapokuwa barabarani.

    ReplyDelete
  21. Ditpoile kazoea...sasa atakula na Zombe ugali wa yanga keko....nimechukia sana.Unaua mtu kama ni NZI

    ReplyDelete
  22. NINGEPENDA AHUKUMIWE KAMA ZOMBE, WAKUTANE BWANA WAKASINZIE PAMOJA UKONGA HII NI ARI MPYA, NGUVU MPYA NA KASI MPYA. HAKUNA KULEANA ETI KWA KUWA NI KIGOGO WA SERIKALI NAOMBA IWE MFANO KWA VIGOGO WENGINE WENYE KUONEA RAIA.

    ReplyDelete
  23. HAPO INABIDI SHERIA ICHUKUE MKONDO TU KWA MH. DITTO AHUKUMIWE KAMA ILIVYOKUWA KWA KESI YA ZOMBE. NA HII ITAKUWA MFANO KWA VIONGOZI WENGINE WA SERIKALI, KWANI MADARAKA SIO KIPIMO CHA KUWAONEA RAIA NA KUCHUKUA MAAMUZI KAMA HAYA, HII INATISHA. KAMA VP KILA MTU AMILIKISHWE SILAHA BASI ILI TUGONGANE! NAOMBA SERIKALI IMUADABISHE BRO! DITTO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...