hizi ni habari za reo reo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. kaka michuzi tunakubali kuwa vyombo vya habari vimeufanyia kazi huu mkasa wa dito.lakini kuna mashaka kwamba hayo yamefanyika kwa kujinufaisha wao/vyenyewe.

    sidhani kama vimeifanyia kazi katika misingi ya kuwajibika, ni kwasababu magazeti yanauzika bega kwa bega na ad space, vile vile kwenye tv na radio "ad time" inanunulika kama peremende.

    kisheria dito hana hatia mpaka kesi imalizike.ingawa kesi bado iko mahakamani, pia hassan mbonde hakufa kifo cha asili, au siyo? lakini je vyombo vya habari vimejaribu kuchambua kwa makini yaliyotokea, au ndiyo hizo headline za "dito karogwa"?

    ReplyDelete
  2. michuzi watu wanauliza mbona viongozi hawajaudhulia mazishi na ule msiba wa vanetha na woltea viongozi waliudhulia au kwasababu ulikuja kutoka usa na huu umekuja kutoka sijui mabibo,watu hawana zile changamoto kama za wakina vaetha na wolter au hakuna pilau na misosi na bia nini,lakini michuzi mwanajeshi unajigawa kila mahali,tunakuitaji finland hili upate tuzo za uandisi na kupiga picha,chelsea mambo poa

    ReplyDelete
  3. Michuzi hivyo si vidole vyako vimeshika hayo magazeti?? kumbe na wewe una mpiga picha wako??? ama kweli mganga hajigangi..lakini kazi yako naiaminia m2 wangu..

    ReplyDelete
  4. Jamani vyama vya upinzani Tanzania vimekufa au vimelala au vimetiwa mfukoni na serikali ya CCM. Akina Lipumba. Mrema. Maalim Seif. Sengondo Mvungi wana msimamo gani kuhusu suala hili la Ditopile. Ingekuwa ni mtu wa Blair, Waingereza wangeishapata changamoto toka conservative party kuing'oa Labour madarakani, na inge-apply hivyo hivyo Japan, USA, Australia, France etc. Tuifuate misingi ya kidemokrasia moja kwa moja na wala si nusu nusu, kufuata vile vitu vinavyoshibisha eti tumbo langu tu, nikisema hivi au vile serikali ya CCM itaninyima ruzuku.

    ReplyDelete
  5. Jamani msiba siyo kwa kina Mbonde tu. Waathirika wengine wapo pia. Mademu uliowaacha huku nje wanapanga kuandamana hadi gerezani uchi ili kushinikiza kuachiwa kwako.

    Wapo ambao wanateseka kwa kumkosa jamaa, hawajali kuwa ni muuaji na hawajutii kupotea uhai wa mtu. Kwao pia kuendelea kumsotesha lupango ni kuwatia kitanzi. Ndiyo maana kuna divided opinions katika suala hili.

    Ya kushangaza wegine ni wake za watu lakini hawafichi expressions zao namna walivyoguswa na tukio hili. Hapa hapendwi mtu bali.............

    Nawaonea huruma kwani mambo ndiyo yameaanza. Tusubiri Pilato atakapotoa hukumu yake. Tutaomboleza zaidi wakati familia ya Mbonde itakapokuwa inafurahia kuona muuaji wa mpendwa wao anapata malipo yake hapa duniani wakati akisubiri hukumu nyingine kama tunavyoamini ipo siku ya mwisho.

    Damu ya mtu hailingani na mtu kupatiwa ajira,watoto wenu kusomeshwa, kupangishiwa nyumba, kununuliwa mchele,sembe, mafuta n.k.Hizi zote ni kuni za kuchochea moto wa jehenamu kwani kumbukeni ni uzinzi mliokuwa mnafanya. Mbaya zaidi wengine mkiwa ndani ya ndoa zenu.

    ReplyDelete
  6. Ditiopile amelogwa,

    Inasemekana alikuwa anakwenda Mbuyuni Bagamoyo kisirisiri baada ya kiza kuingia kwa ajili ya "shughuli" kujiongezea 'nguvu ya mvuto' baada ya kuukosa ukatibu mkuu wa CCM. Ngoma nzito hiyo!!

    ReplyDelete
  7. Michuzi sio reo reo ni Leo leo, Mwandishi mkubwa mwenye sifa zake lakini hawezi kutunza kiswahili ni aibu kubwa kwa taifa.

    ReplyDelete
  8. jamani wana blogg naomba kuuliza,hivi kuna watu wengine wanakuwa hawana kazi ya kufanya wao na michuiz blog?

    Kama huyu sijue ANONYMOUS yaani mpka anatia kichefu chefu maana sehemu zote ameandika yeye hata wengine tunakosa mahala pa kutoa maoni,au wewe kula kulala nini huna cha kufanya zaidi ya kuandika,maana sitie akilini muda wote huo unapata wapi kuandika kila picha tena msg zaidi ya 5.

    Jirekebishe bwana na sisi tupate sehemu ya kuandika.

    sorry kama nimekukosea.

    ReplyDelete
  9. asante sana michuzi kwa kutupatia habari kila siku zinazotokea huko nyumbani kiasi tunaweza kujua kila kinachojili kila siku ,kiasi tunafurahi sana endelea hivyo hivyo michuzi lkn humetokea mbali kaka mmm nakukumbuka toka enzi za msasani beach

    ReplyDelete
  10. mazishi ya Bwana Mbonde(Mungu amlaze mahali pema peponi)yamekwepwa na 'wanasiasa' kwa kuwa yamevaa sura ya kisiasa. Yaani kila mtu analichukulia kwa namna anavyoweza.

    ReplyDelete
  11. MIJITU INAONGEA PUMBA SANA KWA KWELI.
    KUNA NDUGU MMOJA ANASEMA VIONGOZI WAKO WAPI KWENYE MSIBA , KWANI UMESIKIA KUWA HUU MSIBA WA TAIFA. ACHA UJINGA WEWE. VIONGOZI WANA MENGI YA KUFANYA. ALILOLIFANYA DITO ALIHUSIANI NA SIASA NI SULA LA KWAKE MWENYWE.

    NA SUALA LA KUHUSU VONETHA NA WALTER UNABIDI UANGALIA NI KWA NINI WAKUBWA WALIKWENDA PALE. SABABU KUBWA LABDA NIKUAMBIE NI KWAMBA WATU WALIKWENDA KWA SABABU YA BABA YAKE WALTER. WATU WANAMFAHAMU KWA KUWA NI MZEE WA SIKU NYINGI KATIKA SYSTEM NA IKUMBUKWE NI MMOJA WA WATRANZANIA WACHACHE WA MWANZO KUENDESHA NDEGE NCHINI NA PIA ANAJICHANGANYA SANA NA WAKUU MJINI. ACHA USHAMBA.

    NA HUYU BWAGE ANAYETAKA LIPUMBA AZUNGUMZE ASITUCHAFUE KABISA. TUACHIE LIPUMBA MSOMI WETU. KWANI KUNA MAMBO KIBAO YA KUZUNGUMZIA.MTU AKIMPIGA KIBAO MKEWE NALO NI LA KUZUNGUMZIWA KWENYE VIKAO. NOOOOOOOOOOOOO! SIDHANI KAMA NDIYO SIASA. UMEPOTOKA NA NAFIKIRI KATAFUTE MUDA WA KUPIKA,WACHA SISI TUSIKILIZIE MOTO UNAOMUENDEA BWANA DITTOTOKA MAHAKAMANI.

    NAITWA MPENDA HAKI....

    ReplyDelete
  12. Wewe Anony wa Thursday, November 09, 2006 5:19:56 PM a.k.a MPENDA HAKI bado uko kwenye ulimwengu wa giza la totoro. Inaonyesha una damu ya CCM mwenye damu ya kijani na mavi ya njano. Hili suala la Dito kuua ni la kitaifa na hao akina Lipumba na Mvungi kama kweli wana akili timamu wanaweza wakalilinganisha suala hili na lile la Rosa Parker au Sharpeville vilivyokuwa vyanzo vya kuwakomboa weusi USA na Suid Afrika, sambamba na hapa kwetu kuwakomboa walala hoi na wanyanyaswaji na baadhi ya viongozi wachafu wanaojifanya Wahangira na kufikiria kuwa they are above the law.

    ReplyDelete
  13. GeGeDu.....Tafuta maana ya Anonymous

    ReplyDelete
  14. Jamani mbona kwenye msiba Mrema mzee wa kiraracha alikuwepo au nyinyi hamkumuona, Michuzi pia alikuwepo na Mkuu wa polisi mkoa wa kinondoni pia au mna watu wenu maalum mpaka wawepo ndio mnaridhika

    ReplyDelete
  15. RHY ACHANA NAO WALEVI HAO. WANAKUWA HAWANA LA KUANDIKA . KWANI NI LAZIMA RAISI HAWEPO KWENYE MSIBA.

    WANASHINDWA JIULIZA WATU WANGAPI WANAKUFA HADI HUYU AWE SPECIAL.....SIMAANISHI KWAMBA BWANA MBONDE HAFAI. ILA NINALOTAKA SEMA NI KWAMBA PALE MUHIMBILI KUNATOKA MAITI SI CHINI YA ISHIRINI. YAANI WANATAKA RAISI AENDE TOA UBANI NA KUSHIRIKI MAZISHI YA WATU WOTE. HUYU RAISI HANA KAZI YA KUFANYA AU IMEKUWAJE.

    MIE NAOMBA KUSISITIZA TENA , KWAMBA TENDO ALILOFANYA DITTO NI LA KWAKE DITTO. ALINA UHUSIANO NA ILANI YA UCHAGUZI, WALA KAZI ZAKE KAMA MKUU WA MKOA NA HILO PIA HALINA UHUSIANO NA MARAFIKI ZAKE AKIWEMO MH.RAISI.

    KITENDO ALICHOKIFANYA NI CHAKE MWENYEWE. KWA HIYO TUACHE SHERTIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

    ReplyDelete
  16. To be honest, alitakiwa angalau mkuu wa mkoa wa Dar awepo kwenye msiba kwa heshima ya familia maana aliyehusika/anayekisiwa ni mmoja wa watu wa serikali. For the sake of all Tanzanians either rich or poor. Hii ni moja ya kazi yao kubwa, to look after people na kuhakikisha vitu kama hivi havitokei. Sio swala la kuwa busy, busy, busy.

    ReplyDelete
  17. wewe gegedu umepinda au ulikimbia umande ?jamani hebu mchekeeni gegedu huyu ni bwege hadi kiama,hebu tafuta mtu aliyesoma akuelekeze maana ya anonymous bwegee mtozeeeen iiiiiiiii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...