
kuna mdau ambaye baada ya kunitumia picha hii kasahau kusema yuko wapi zaidi ya kwamba kiwinta kimetua ughaibuni kwa kishindo na hapa mkoko wake ulionasa kwenye theluji imebidi ausamehe awahi janta, anasema kufa hawafi ila cha moto (ama baridi?) wanakiona. kama hali yenyewe ndo hii wa-ughaibuni poleni - wenzenu twatanua tu na jua la mwaka mzima. si mrudi basi?
MDAU YEYOTE MWENYE PICHA ANAZOTAKA KUZIMWAGA KWENYE BLOGU YENU HII POPOTE ALIPO HUMU DUNIANI NA HATA AHERA IKIWEZEKANA ANAKARIBISHWA KWA MIKONO YOTE NA MIGUU...
Kaka michuzi unachekesha kweli,Turudi wapi?huko hata umeme na maji hakuna si bora baridi unaweza kujizuia joto na umeme na joto la bongo kaka michuzi si unaweza kuzimia mkuu!!!
ReplyDeleteWacha kwanza tuangalie usitarabu ikishindikana kabisa tutarudu kwa mzee KK tubanene!1
Hizo picha kaka michuzi tutazituma vipi basi tupe basi mawasiliano yako au email au vyovyote mkuu!1
ReplyDeleteMichuzi kaka, kawaida kukiwa na snow namna hiyo baridi hupungua yakhe, hadi kama itakaa na kuganda iwe barafu, lakini sio rahisi sababu mpaka hapo wapo kibao wanacheka kwa kupata tenda za kuondoa hiyo snow, basi ilimradi tu kila kitu kwa mpangilio,ughaibuni bwana!!
ReplyDelete