Home
Unlabelled
maalim
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Maskini self, uso umeanza kukunjamana kwa matamaa ya kwenda IKULU. umeanza kufanana na Osama!!
ReplyDeleteWanaume family-TMK walikuwa wapiga kampeni wazuri wa CCM katika uchaguzi uliopita.naona seif kapiga kofia ya wanaumeeeee sijui ujumbe anaotupa.hii ni sawa na kumuona Mbowe kavaa fulana ya TOT!!!
ReplyDeleteIkiwa kuna maana yeyote ya kuleta ushirikiano mpya baina ya Kenya, Tanzania na Uganda, ikiwa ni pamoja na kuzikaribisha Burundi na Rwanda, tatizo la kumaliza mgogoro wa Zanzibar ni kuwaacha Wazanzibari waende wanakotaka (kupitia kura za maoni)yaani wawe na nchi yao huru! Muungano wetu haukuumbika mbinguni. Tulitoa uzorotaji wa chama kimoja. Tunaendelea kuuzika ujamaa polepole. Tuzike Muungano basi, na Wazanzibari wakaribishwe kujiunga na Afrika Mashariki ili kumaliza tatizo kama la Urusi-Cheychena au Tibet-China nchini kwetu!
ReplyDeleteHuyu ni mpigania haki za kubuni za Wapemba. Wapemba hawawezi ongoza Taifa tena sababu siku zote wao agenda kuu ni kupigania haki wapemba.Nchi ya Zanzibar haiwezi ongozwa na mtu ambaye kila akilala na kuamka anaota pemba tu.Hata Tanzania hatuwezi mpa mtu ambaye mawazo yake na fikra na moyo wake uko pemba na siyo Tanzania nzima.
ReplyDeleteKarume una tabia mbaya na wewe uwe na huruma kwa mwezio.Mpe wembe akanyoe hizo ndevu zilizogaa kama mkutano wa inzi na mwambie akapige mswaki HAYO meno machafu kama ya muuza ugoro.Hiyo ndio huruma pekee unayoweza kumsaidia Karume.
Maoni Tu! kwa hiyo unataka kutwambia kuwa wazanzibar waruhusiwe either kuungana na china, au india, au komoro au kenya na nchi yeyote?
ReplyDeleteMimi nakubaliana sana na KIDUME unajua sasa hivi hatuwezi kuendelea kuwa na siasa zile za kizamani, siasa za sasa hivi ni siasa za kiuchumi. Kwa hiyo wale wazee ambao wamekuwa katika systems miaka ya siasa za ukeleketwa hawana budi wang'atuke kizazi kingine chenye mawazo ya kiuchumi kielekeze wazanzibar katika direction nyingine.
Hii pia inajionyesha wazio enzi hizi mweshimiwa rais wa zanzibar badala ya kushugulikia matatizo ya wazanzibar sasa amekuwa mswahili tu anaongea tu mambo bila kuyafanyia kazi. Mshauri kama ameshindwa kuendeleza zanzibar kichumi anyamaze ale kama ndege muda wake wa miaka minne ukiisha angatuke kama kamando siyo kuleta choko choko.
Maswala kama haya anayofanya angelikuwepo Mwalimu JK muhasisi mwenyewe angelimuonyesha jinsi ya kutawala zanzibar.
Hivi tutaendelea kuwakumbatia hawa WAZANZIBAR mpaka lini ???? Kwanza ni watu wa dhiki sana na wanafiki na ndio maana wanakimbilia huku kwetu kufanya biashara. Jambo moja ambalo ningeshauri ni kuwafukuza huku bara na warudi kwao kama haujaona wanakufa huko kwao. Kwanza ni wavivu halafu ni wachafu !!!! WARUDI KWAO HATUWATAKI HUKU BARA (TANZANIA) WARUDI KWAO
ReplyDeleteHapa pichani Seif anatafakari kwa kina sana kuhusu hatima ya Pemba na Wapemba wakati Karume kule Ikulu anatafakari Kuhusu hatima ya Zanzibar nzima kama taifa na Raisi Kikwete anatafakari hatima ya Tanzania nzima.Katika hao watatu unadhani ni nani Kenge MWITU hapo asiyejua siasa?
ReplyDeleteWapemba weupe ndio tatizo.Wanajifanya wakereketwa wa Pemba Wakati biashara na Makazi yao ya kifahari yako Unguja na Tanzania Bara.Wanatumia walala hoi na maskini wasiojua kusoma wala kuandika waishio pemba kama daraja lao la madai hewa yao na kupatia ruzuku na fursa za kisiasa.Watu wa haki za Binadamu wasaidieni watu wa Pemba dhidi ya wanafiki wanaojifanya wakereketwa wa Pemba lakini wanaishi miji mikubwa ya London,Uholanzi,Unguja,Dar es salaam n.k wakila kuku kwa mrija wakati wakazi wenyewe wa Pemba Wanaumia na wako hoi.
ReplyDeleteWe maalim mbona umeshajifia unataka tena nini! kaa nyumbani kwako ulee wajukuu! kwani uso umeshajaa makunyazi urais wa nini?
ReplyDeleteKwako Bw. Seif Shariff Hamad, Waziri Kiongozi Mtaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
ReplyDeleteNi dhahiri kuwa wewe si kiongozi Shupavu wa Chama cha Wananchi CUF.
Nina imani chama chako kinatakiwa kuendeshwa kwa misingi ya kidemokrasi na wala siyo ki-imla. Naamini kuwa chama chako kinajitambulisha kwa kudai haki zaidi na wala si kwa upendeleo wa watu wa upande fulani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naamini kuwa wewe na Mwenyekiti wako Bw. Harun Lipumba, mmepata nafasi nyingi za kugombea urais kupitia chama chenu kuliko mwanachama mwingine yeyote. Naamini ndani ya chama chenu cha CUF wapo watu wenye uwezo mkubwa wa uongozi zaidi yenu nyinyi. Naamini kabisa Bw. Seif Shariff Hamadi sasa huna jambo jipya utakaloweza kulifanya kama Katibu Mkuu wa CUF sembuse rais wa Zanzibar. Naamini unang'ang'ania madaraka kwa manufaa ya kikundi cha watu wachache waliopo ndani ya Jamhuri hii. Naamini wewe na kundi lako la watu wachache ndani ya CUF ndiyo wenye nguvu na maamuzi ya mwisho na wala siyo Mwenyekiti na wanachama wengine. Naamini kuwa unakalazimisha hali hii ya CUF ni SEIF na SEIF ni CUF kwa manufaa binafsi. Naamini matokeo ya kwenye sanduku la kura yanatakiwa yaheshimiwe na wala si vinginevyo. Acha ujeuri, husda, dharau na kejeli, muheshimu Rais Amani Abeid Karume akiwa ni kiongozi wako halali.
Nakushauri achia ngazi ili demokrasia ichukue nafasi yake ndani ya CUF.
ruta mwalimu jk alisema dhambi ya kujitenga haiwezi kukuacha ni kama kula nyama ya binadamu nimenukuu...kwahiyo sifikiri ni jambo la busara kuwatenga hawa ndugu zetu cha msingi ni kuanzisha mjadala wa kitaifa kama ilivyo kwa jumuiya ya afrika mashariki elimu juu ya muungano nayo iwe katika muongo huo huo wa jumiya ya afrika mashariki kuna vitu vichache sana vya kurekebisha ili kwenda na hizi siasa za kiuchumi na maendeleo ambavyo vinarekebishika na kuwa na tanzania yenye amani na undugu tusije anza kufarakana na kwenda mbali
ReplyDeleteMonday, November 13, 2006 11:00:11 AM,
ReplyDeleteSikusema "kuwa wazanzibar waruhusiwe either kuungana na china, au india, au komoro au kenya na nchi yeyote."
Nilimaanisha kwanza tujadili matatizo yaliyopo, na endapo kutakuwepo na ulazima wa wa-Zanzibari kuwa as independent and sovereign State, basi kura ya maoni ipitishwe huko huko.
Maoni zaidi:
Kuna wa-Zanzibari wanaoamini kuwa Mapinduzi yaliyotokea si ya halali! Kuna minong'ono ya wa-Zanzibari kuwa uhuru wa Zanzibar ulitekwa na Wabara (akina Karume na Mwinyi Co.)! Muungano si wa halali, ndio maana wengine walitaka kuushitaki Muungano na Umoja wa Mataifa!
Watu wa namna hii wakifanikiwa, huenda wakazishitaki pia serikali za Uingereza na Kenya kwa kuunganisha Mwambao kuwa sehemu ya Kenya!
Ni wajibu wa Rais JK, Serikali ya Mapinduzi, CUF na interested parties nyingine kuanika nje wazi wazi kitovu cha uhasama na dukuduku za kuhusu uhusiano wa Tanzania Bara na Tanzanian Visiwani!
Ni lazina JK a-apply ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya katika kumaliza mgogoro huu ambao unpoteza wakati, nguvu, na ku-occupy the minds za Watanzania!
Hakuna mgogoro.Mgogoro ni wapemba tu.Ukiwaondoa wapemba nchi hii muungano utakuwa shwari na bila kelele wala tatizo lolote.
ReplyDeleteWapemba hawapendi mswahili akitawala,walimsumbua Mzee Karume,Aboud Jumbe,Mwinyi na Salmin Amour .
Kwa wapemba kiongozi mzuri ni mwarabu au Mpemba.Hata sheikh mzuri kwa wapemba lazima awe mwarabu au mpemba.Ndio maana wapemba hawaipendi kabisa BAKWATA sababu ni baraza la kiislamu linaloongozwa na waswahili ngozi nyeusi.Masheih wazuri kwao ni wale wenye uarabu arabu na upemba.
Hata wakifunga mwezi wanaoamini umeandama ni ule unaoonekana uarabuni.Huu unaoandama Afrika sio mwezi ni koroboi tu!
Kavaa tu kofia ya wanaume lakini ninavyojua CUF hakuna wanaume wa nguvu maana Profesa Lipumba ambaye ni mwenyekiti wao wa chama Taifa hata mke hana. Hivi ana tatizo gani? hadi akose mwanamke kama hicho chama ni kweli cha wanaume kama hilo kofia alilovaa linasema ukweli.
ReplyDeleteSitaki kabisa kusikia habari za wapemba. Huku mtaani mtu akifa nyumba ya pili karibu na Mpemba,Mpemba hafungi duka anaendelea kuuza tu hata kama maiti iko ndani.Lakini akisikia mpemba mwezie kafa hata kama kafa Maili 1000 lazima afunge duka.
ReplyDeleteIkifikia uchaguzi utawakuta misikitini wanapita kufanya kampeni wachaguliwe .Wanafiki wakubwa.Mtu kama huna uhusiano siku za kawaida ndio unataka siku ya uchaguzi akuchague.Ndio maana CUF ilikosa kura nyingi isipokuwa Pemba peke yake.Hata wana CUF wasio wapemba waliona ujinga wakaamua kupigia vyama vingine.Wapemba msipobadilika mitizamo,fikra zenu na namna mnavyoona na kuwachukulia watu wengine wasio wapemba hakuna mtu atakuja kuwapa kura nchi hii mtakuwa mkishinda huko huko kwenu Pemba.
Sasa hivi Zanzibar ndio wanauhitaji muungano kuliko Tanzania bara.Zamani tulikuwa Bara tunauhitaji muungano kwa sababu tulikuwa tumechoka kiuchumi ikabidi tuwe tunakimbilia Zanzibar kununua chupi na sidiria.Sasa hivi tunaweza enda au agiza hata ulaya tukanunua.Hatuna shida tena na Zanzibar.Wao ndio wana shida kuanzia chakula na Biashara zao wanahitaji bara ili watajirike.Sasa hivi ni wakati muafaka wa kuwatimua kwenye muungano kama wanajifanya kunatanata.
ReplyDeleteMheshimiwa Kikwete wakileta mambo ya urembo na kulegeza macho waambie waanze na watu wao walioko bara warudi Zanzibar upesi.Wasikupe presha Raisi wetu uache kufikiria mambo yao yasiyo na kichwa wala miguu.Wawepo au wasiwepo kwenye muungano hawana wanachotuongezea wala kutupunguzia sana sana wanatupaka matope tu mbele ya jumuiya za kimataifa.
CUF inasema haki sawa kwa wote lakini nenda Pemba ujaribu kuanzisha chama cha siasa au uwe mwanachama wa chama kingine zaidi ya CUF utanyanyaswa hadi ukome na wana CUF.Hii ndiyo haki sawa kwa wote? Watu wa haki za binadamu tembeleeni Pemba muone uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na CUF kwa watu wa vyama vingine.Pia kuna unyanyasaji wa hali juu kwa watu wa dini zingine hasa Wakristo.Hakuna uhuru wa kuabudu kule.Na tunashukuru jumuiya za kiraia kwa kupeleka taarifa kwa jumuiya za kimataifa kuhusu uvunjaji demokrasia Pemba na tunashukuru baada ya wengi wao kujionea hali halisi ilivyo Pemba wameanza kuwaelewa Wapemba na wameanza Kushawishi serikali zao kujitoa kuendelea kuwaunga mkono CUF.Ndiyo maana sasa hivi hawaipigii kelele Serikali ya Tanzania kama zamani walipokuwa hawajawajua vizuri CUF.
ReplyDeleteHaki sawa mzifanyie kazi Pemba pia siyo kwenye kutaka uraisi tu.
Ulevi wa Kipemba
ReplyDeleteNILIZINDUKA majira ya saa nne usiku nikiwa nimelala chali. Macho yangu yalitua juu ya dari nyeupe. Baada ya muda mfupi nikagundua kwamba juu yangu kuliuwa pangaboi na taa kali ikimulika. Nilijua kwamba hapa sio nyumbani. Nipo wapi basi? Nikajaribu kujivuta kidogo ili kutaka kujua habari zaidi. Hapo ndipo nilipohisi kwamba nilikuwa taabani maumivu makali yalinipata mwilini. Ukwenzi mkali wa kuonyesha maumivu ulinitoka.
Baada ya kushindwa kujifaragua nikaamua kuangaza pembeni yangu. Kivuli cha mtu kilikuwa kimejinamia. Alipohisi kwamba ninamtizama naye alinyanyua macho yake. Macho yetu yakakutana. Dalili ya machozi haikujificha kwenye macho yake. Nilianza kumwonea huruma. Ni kaka yangu mwenyeji wangu hapa Zanzibar.
"Hadi lini tutaepukana na dhiki hii?" alinung'unika.
Sikuwa na jibu bali niendelea kumwangalia kwa muda huku machozi yakinibubujika kama mvua. Hatimaye niligeuza uso na kuangalia juu. Sikuwa nimevutiwa na chochote darini bali mawazo yangu yalikwenda mbali, mbali sana. Sio umbali wa siku nyingi bali matokeo mengi ya huzuni na sio wingi mkubwa, bali uchungu wake unaumiza sana sana. Unakata maini, unachefua moho, kichwa kinakaribia kupasuka, ulimi unakaribia kuacha kazi. Kila kitu sasa waweza kukiona kichungu kuliko.
Mara baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza kwamba wanafunzi sasa itawabidi warudi kujiandikisha kwao walikotoka, nilisema nitakwenda. Niliwakuta watu wamo katika kujiandikisha. Malalamiko kila mahala, shutuma kushutumiana, matusi kutukanana. Nikasema ah, ndio jino kwa jino". Nikajijibu mwenyewe... "Pengine ... lakini
Sikuchelewa kujua sababu yake. Au niseme sikuchelewa na mimi kuingia ngomani. Nami sikukosa wa kumtukana bila kujijua. Labda ni kweli aliyosema mhariri wa gazeti moja litolewalo kila wiki "ni ulevi wa Kipemba".
Basi siku ya pili yake nilichukua cheti changu cha kuzaliwa. Nikajisogeza kwenye foleni mara tu baada ya kuswali swala ya asubuhi. Tukasubiri saa mbili. Tulikuwa tunaongea, tulicheka na kufyonya. Hayakuwa mazungumzo ya kufurahisha. Lakini uchungu unapozidi binadamu hana budi kucheka.
Kila mtu alikuwa akizungumzia sababu ya kuitoa CCM madarakani. Aliyenyimwa nafasi ya masomo kiroho mbaya. Aliyezuliwa kufanya biashara kubwa ya kuagiza mchele... Aliyekosa ajira kwa kufukuzwa kwa vile ni Mpemba... Anavyosota kusubiri kiinua mgongo kwa kuwa hana jamaa. Maana mambo yenyewe kama huna jamaa, ujitegemee. Ndio sera ya CCM - Ujamaa na Kujitegemea. "Rasilimali yangu ni kura tu ili nijitegemee... Hata nikishinda hapo mwezi mzima...kama si vile virungu vya usiku jana. Ningelala hapa hapa... Sote tulicheka... "Ohoo, ulevi wa Kipemba huo". Nilijisemea.
Sasa saa mbili inakaribia mtu wa mbele sasa hataki tena mazungumzo. Macho mbele tu... Ghafla akalazimika kugeuza uso kwani watu walianza kuguna mm! Mm! Bismillahir! Uso kwa uso na "Mahita" (askari polisi mmoja kule Kusini Pemba huitwa "Mahita" kwa uhodari wake wa kuwafundisha CUF ngangari). Gari la KMKM likiwa na wazamiaji kibao waliteremka. Kwanza ni bambasanchi. Utadhani watuhumiwa wa wizi, mabegani, tumboni, mifukoni mat.. ni... Baadaye amri moja.
Kaa chini! Tukakaa "Mahita" na Diwani (mgombea) wa CCM wakaanza kuopoa wakereketwa wa CCM. Baada ya hapo amri nyingine. "Rudi nyuma" Tukarudi. Wakereketwa wa wakereketwa wakawekwa mbele..!! Donge zito la mate machungu likajilazimisha kudidimia tumboni. "Kileo cha Kipemba". Na hakika na wenzangu walikunywa kileo hicho.
Yule jamaa aliyekuwa mbele aligeuka nyuma kwa uchungu mdomo wazi. Najua tuliekeana sawa sawa lakini sidhani kama alikuwa akiniona. Dakika tano zilipita (sikuwa na saa) katika hali ile. Machozi yalikuwa yakimchuruzika. Oh maskini bahati yake hakuwa amesimama.
Filimbi ikaanza, foleni ikaanza kusogea haraka haraka utadhani sio wale waandishi wa jana. Leo kama wote mabingwa wa malaria (madaktari wakikutazama wanakujua kama unaumwa malaria). "Nenda dirishani". Oh maskini. Mtanzania nchi yako ndio maskini ya kutupwa, pamoja na utajiri wa amani. Hayo namwachia Lipumba labda naye amekunywa "ulevi wa Kipemba".
Basi wasikia sana. Ilipofika saa tano. Mtu mmoja alitoka ndani pamoja na "Mahita" akatwambia "wazee itabidi tusubiri "stika" kwani zimetuishia. Lisilo budi hutendwa, tufanyeje na walipindua ili watu..." watukomboe. Hayaa.
Basi baba tukasubiri, tukasubiri, tukasubiri.... Hadi adhana ya laasiri tukaambiwa sasa "stika" tayari. Tume bwana haina mchezo kwa kazi! Haya foleni ikasogea na mimi sikuwa mbali nikapata nafasi ya kuingia ndani.
Kabla ya kukaa kitako Sheha (wakala wa Tume, nasikia) akamaka "huyo hana kura huyo". "Mimi, mimi" nikajibu kwa kigugumizi. "Mimi nimemaliza F II mwaka jana hapa". Nikajitetea. Nasema hakai hapa huyo, kashahama. Kuona hivyo wakala wa CUF akanitetea, "lakini sheria ndivyo isemavyo. Vijana wanaosoma nje ya majimbo yao wajiandikishe kwao. "Wee! Utakwenda ndani sasa hivi usifanye fujo hapa", "Mahita" alimng'akia wakala wa CUF baada ya kuona "ulevi wa Kipemba" unaanza kumpanda mwana ngangari.
Kuona vile nikaona sina budi nikimbie kulala jela. Machozi huku yakinibubujika. Ni lazima nipige kura kwa maisha yangu... CCM imetandika mfumo wa kibaguzi... Mimi Mpemba sina langu, sina haki, katika nchi hii... Loh! Aliyeninyima kupiga kura ... Siendi mazikoni kwake... simpi maji hata akiwa na kiu ya kufa... kiwanda kizima cha matusi kilikuwa kimejenga kwenye ulimi wangu. yaliyonitoka kimoyomoyo, yakinitoka njiani, yakinitoka ninapokula, yakinitoka usingizini Loh! Maskini ulevi wa Kipemba".
Baada ya kuona sina jimbo. Labda Msomalia au Mhutu au sijui... Nikaamua kupanda meli kurejea Unguja. Nikabaki kuulizia Nani kapigwa... Nani katiwa pingu... Nani yuko rumande.
Mara Radio One, mara radio Kifua alimradi nimo mashakani, roho yangu imekuwa kiwanda cha matusi. Na chuki kwa nini lakini nisichukie?
Hadi ilipokuwa siku ya mwisho ya kupiga kura. Kaka yangu alikuwa amekataliwa kupiga kura. Kwa sababu eti sio mkazi wa pale. Bwana Sheha, hamjui, hayumo ndan ya madaftari yake. Sikushangaa kuona hana raha, nafsi yake imekuwa nzito sana kwake. Hana hamu ya kufanya kazi. Amebaki kukuna kichwa. Mwaka wa kumi sasa anaishi hapa. Kazini alifukuzwa kwa vile tajiri wake anaogopa kumwajiri kwa vile yeye ni Mpemba. Angepoteza haiba mbele ya wenzake. Sasa anaishi kwa kubabaisha tu.
Usiku kuamkia siku ile tulikaa nyumbani kutafakari hali halisi. Mtu mmoja alitwambia kwamba askari kutoka bara walikuwa wakiandikishwa kupiga kura. Wengine hawajawa raia wa Zanzibar. Wengine hawajatimiza sharia za ukaazi... Katika maongezi mtu mmoja alitudokeza kwamba wengi wa askari hupewa kadi ya kumchagua Rais wa Muungano tu. Tulipofika hapo mawazo yakatujia, kama ni hivyo basi sisi tuna haki zaidi ya kupewa kumchagua Rais wa Muungano na wa Zanzibar pia. Tukaazimia kesho yake kwenda kubahatisha.
Siku ya mwisho ya uandikishaji kulikuwa na watu wengi kituoni, kama kawaida. Ni dhahiri watu wasingemalizika. Tume iliamua watu wapewe risiti badala ya kutumia muda mrefu kuwapa kadi. Ili baadae watambulikane wote waliojitokeza wapewe kadi zao za kupigia kura. Uandikishaji ulikwenda vizuri zaidi alipowasili kiongozi mmoja mkubwa wa serikali. Kila mtu alikuwa na tamaa ya kuwahi ingawa wengine tulitegemea pingamizi.
Ilipofika saa tano mchana, mara tu baada ya kuondoka yule mkuu hali ilibadilika. Makundi ya askari wa kuzuia fujo, FFU yalivivamia vituo karibu vyote ya ng'ambo mjini. Watu waliokuwa foleni wakapigwa marungu ili waondoke. Watu wengi waliumia. Gari la polisi lililetwa kuwasomba majerhi. Mimi nilikuwa miongoni mwa watu tuliopata virungu ingawa nilikuwa nimeumia sana lakini nilifaulu kukimbia hadi uchochoroni. Kaka yangu yeye hakujeruhiwa. Tulikimbia pamoja kwa hatua chache. Nilianza kunyong'onyea. Kugundua hali hiyo, kaka yangu akanibeba. Kulikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Watu waliopigwa bila kosa lolote baadaye kupelekwa hospitali, bali walipelekwa rumande bila matibabu wakisubiri kubambikizwa mashitaka ya kufanya fujo kituoni. Mungu tuhurumie waja wako.
Baada ya muda mfupi nilipoteza fahamu nimeletwa hapa ili kupata matababu. Bali hapa nisalama zaidi kuliko hospitali. Kwanza nisingetibiwa kwa vile singepata fomu ya polisi PF 3. Ndivyo tunavyotakiwa. Tunaambiwa tumelewa, tumepagawa kwa kutaka ukubwa na uroho wa madaraka Akutukanae hakuchagulii tusi.
Baadaye kituo 'wana maskani'. Wakaendelea kuandikana tena na tena. Ole wako ufunue domo lako, utakung'utwa virungu ushike adabu yako.Nani kakuambia ulete
Ulevi wako wa Kipemba. Ulevi huu mbaya jamani.Lakini wanywaji watakosekanaaje
Wakati wagema wapo?.