masela wa kawe wakishangilia baada ya mtasha kutoa 'ubani' sh. 10,000. kila gari lililopita barabara ya old bagamoyo rodi lilisimamishwa kuombwa 'ubani' na waombolezaji wengi wao wakiwa madere, makonda na wapiga debe... .vinginevyo leo kwa ulikuwa hukatishi hivi hivi bila kutoa chochote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. NASIKIA DITO ALIKUWA BEST MAN WA JK SIKU ALIPOA, JE ATAMLINDA SWAHIBA WAKE WA SIKU NYINGI ?? TUONE KAMA SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE!!

    ReplyDelete
  2. Mi nafurahi kuona sheria inafanya kazi. kama Sadam Husseni kahukumiwa kunyongwa who is Ditopile?????????? Hata kama alikuwa best wa JK lazima atambue kwamba sheria haina nani wala nani. Naomba haki itendendeke na JK asiingilie kati.

    ReplyDelete
  3. Ulimwengu wa sasa si ule wa zamani watu wantambua haki zao hata kama hawana pesa. Huyo Ditopile na afungwe na apewa adhabu inayo stahili. Wakubwa wamezoea kukwepa kwepa mambo haya sasa tuone nini kitafuata. Na huko dar alienada kufanya nini? Badala akae ofisini anabakia kuzurua na kuletea watu balaa. So sad.

    ReplyDelete
  4. jamani jamani, sisi tunaodaiwa 'ubani' kwa kosa la kukaa tegeta tunakosa gani? huu si wizi wa wazi wazi kweli? Risasi itoke kwenye bastola ya Dito wengine woooote tunaopita hiyo barabara tunadaiwa 'ubani' hiyo haijakaa sawa

    ReplyDelete
  5. DITO AMEUA KWA KUKUSUDIA HILI HALINA MJDALA. HUKUMU YAKE INAELEWEKA NA HUKUMU HIYO ITAKUWA FUNDISHO KWA WATU KAMA HAWA NGULUME AMBAO INASHANGAZA, PAMOJA NA KUKIUKA MISINGI YA UTAWALA BORA, BAADO WANAKUMBATIWA NA JK

    ReplyDelete
  6. Samahani jamani, ni swali tu, Je, huu ubani unawafikia walengwa?(Wafiwa)

    ReplyDelete
  7. hii picha inaonyesha ile methali isemayo "kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi" watz lazima tubadilike la sivyo.....!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. mimi huwa kuna vitu vinanipa wasiwasi sana. Kwanza watanzania wengii mimi nikiwemo si proactive bali ni reactive.Ni sisisisi ambao tunawajenga hawa wapuuzi hadi kufikia sehemu ambapo wanaona kila kitu ni haki kwao, af likitokea tatizo kama hili tunareact kana kwamba tulikuwa tunategemea huu uozo kutokea(hindsite bias)wakati muda wote tulikuwa kimya na tunasifu kaka dito,kaka dito..tukiwaacha wanafanya wanavyotaka. Mbili,wasiwas wangu una zidi kuongezeka ninavyosikia kuwa huyu ni mtu wa karibu wa rais wetu na alkuwa bestman wake.uoga unazidi nikifikiria kuwa urafiki uwaga unaendana sana wakati mwingine na watu wanaoshahabiana muonekano, lakini nzuri, mbaya kwa hii case ni kwa wale pia wanaoshahabiana kimawazo na pia kiakili.Huwaga si mtu wa kupenda kuconclude mapema, lakini nikitumia huu mtazamo ninaanza kuingalia tena kesi ya babu seya kwa mtazamo mpya, kweli nimeamini lisemalwo lipo!. Tatu, najua kuna vingozi wengi tumewasifu, na tumewakashifu, lakini nimegundua uozo wa wale ambae wamekuwa wakikashfiwa kabla, haufikii ya wale ambao watu walikuwa kimya juu yao, hau ya wale baadhi ya wajuu wanaosifiwa sana( nafkiri mnanielewa!). Wasiwasi unataka kuniua ninapofkiri ipo siku watafanya zaidi ya haya na tutabaki tunashangaa na kusema tulijua wakati sio. Unajua sio siri mwanzoni nilikuwa naona watu wanaotoa maoni kukosoa wengine ni wazushi, lakini sasa nimeona umuhimu wa kukosoa watu hawa wanaotishia hali yeyote ya kijamii as ni njia ya kuwa proactive kwani wakijua watu hawapendi na wanajua watapunguza uozo wao. Hivyo napenda kutoa pongezi kwa watu wote waliokuwa wanakashifu upumbavu na uozo wa watu na naomba msamaha kwa mtazamo wangu wa kabla, kuanzia leo tuko pamoja. Kutokana na mwamko wangu huu mpya nadhani ingefaa hata kuanzisha blogu ya kuwaanika adharani na kuwapaka viongozi, watu, na vitukuu vyao ambavyo vinatishia value katika jamiii yetu. Hii nafkiri ni njia ya kuzuia uozo katika jamii( hata katika criminology kuna policy ya crime controll inayoitwa zero torelance ambayo inasema kuzuia uhalifu mdogomdogo ni njia nzuri ya kuzuia uhalifu mkubwa).kwa hiyo naomba mawazo yenu wanabogu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...