mlimani site komplex usiku. humu mna maduka ya vitu mbali mbali kama 200, shoprite kapata mpinzani anayeitwa gemu toka sauzi na vitu kibao na bei poa. photo point nayo ndani!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Nimekubali sasa hiyo siyo mchezo nafikiri savey sasa wajiandae yale makolokolo eti ni nyumba nafikiri sasa zitabomolewa.

    Michuzi hapo hakuna night club kweli? Make naona kumekucha. Afadhali nami sasa nitakuwa mjini.

    ReplyDelete
  2. Kutokana na Plan iliyokuwa ikionyeshwa na management ya UDSM kwenye banda lao la sabasaba mwaka 2003 na 2004 ilikuwa ina nafasi ya Five Star hotel + Conference hall, lakini kulikuwa hakuna students hostel kabisa. Hivyo mimi sikuifurahia wala kuishabikia hiyo plan, kwani najaribu kufikiria hali ya wanafunzi wa UDSM hasa ukizingatia kuwa hivi sasa tu pale hall 5 na 2 watu wanalala zaidi ya 4 kwenye chumba cha watu wawili. Sasa sioni sababu ya University kukodisha eneo kwaajili ya kuinvest shoping center, badala ya kufanya kama walivyofanya NSSF kujenga zile Mabibo Hostel! Anyway hayo ni mawazo yangu ya Kihandisi na wala si ya Kiuchumi. NATOA HOJA.

    ReplyDelete
  3. Kila kitu Sauzi mweee, tutapona kweli siye?

    ReplyDelete
  4. Mambo hayo!
    Jambo zuri ni kwa hizi kompleksi kujengwa kando ya jiji. Itasaidia kupunguza msongamano wa magari. Lakini, bidhaa zinazouzwa humo ndani zitatusaidia kutengeneza ajira kwa vijana; kuanzia kwa mkulima hadi mwenye kiwanda kidogo cha usindikaji? Maana hawa Wasauzi wana hulka ya kuagiza hata machungwa na ma-apples kutoka kwao wakati yetu yanaozea Lushoto na Njombe kwa kukosa soko.

    ReplyDelete
  5. YOTE TISA KUMI UMEME UPO HAPO AMA MAMBO YA MGAO? NA HAYO MAJI SIJUI KAMA YANATOKA VYOO VITANUKA BAADA YA WIKI TU. BONGO NI BONGO TU BWANA.

    ReplyDelete
  6. mbona wanajenga Dar mikoa mingine itajengwa lini hayo maduka mikoani kunazidi kuchoka tu Dar inapendeza manaake picha tuzionazo ni za Dar tu

    ReplyDelete
  7. Aah mbona uwekezaji jambo la kawaida chakubanga... kuku sauz, machungwa sauzi, toilet paper sauz.. sasa bado nini tena...!!! Ajira kasheshe manake utashangaa hata wafagiaji wanaletwa kinamna wakati wabongo tupo kibao na tunajua kufagia fresh..... mameneja toka sauz nk wakati tuna vijana wabichiii hapa bongo na elimu zao na wanajua kazi lakini wataachwa wanashangaa kama sio kuwekwa kwenye till kupokea hela toka kwa wateja.. JK aruhusu uwekezaji lakini swala la ajira liachiwe wazawa basi walao kama nanasi si la lushoto basi mfanyakazi awe wa lushoto kuliuza hilo la sauz.....

    ReplyDelete
  8. Nakuunga mkono, ewe Mzawa = Tuesday, November 14, 2006 11:45:41 PM!

    Katika kipindi cha miaka sita ijayo, kuna haja ya kuendeleza miji yetu mingine ijengeke, kama Dar!

    Kila mwaka tuwe na jiji moja la kuendeleza! JK akifanya hivyo atabakiza legasi safi yenye mwelekeo wa kuleta hali nzuri ya maisha kwa wote si wa Dar tu!

    Dar ibakie makao makuu ya Serikali kwa sababu "wazee" hawataki kuhamia Doma - mpaka sasa nyumba nyingi za Mawaziri wa kabineti ya JK zinajengwa Dar! Dar iunganishe Mikoa ya Dar, Kibaha na sehemu za Morogoro ya Kasikazini.

    Mwanza liwe jiji kubwa kwa Mikoa yote ya Ziwa Victoria na senta ya madini ya dhahabu na almasi (kwa ajili ya Mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga na Mara), ikiwani pamoja na kudumisha biashara, michezo na utamaduni na nchi za jirani za Uganda na Kenya.

    Arusha kwa Mikoa yote ya Kasikazini -Arusha iwe makao makuu ya Korti Kuu na senta ya madini ya tanzanite - licha ya Makao Makuu ya Muungano utakaozaliwa. Mikoa yote ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga inufaike ikiwa ni pamoja na kukaribisha biashara, michezo na utamaduni kutoka sehemu za jirani za Kenya.

    Dodoma kwa Mikoa yote ya Kati - Dodoma ibakie Makao Makuu ya Bunge tu.

    Mtwara kwa Mikoa ya Kusini - ili kuvutia biashara na michezo na utamaduni karibu na Msumbiji. Mikoa ta Lindi, Mtwara na Songea inufaike na kuunganuishwa kwa reli!

    Mbeya kwa Mikoa yote ya Milima ya Kusini - ili kuvutia biashara na michezo na utamaduni karibu na Zambia na Malawi na senta ya makaaa ya mawe na chuma. Mikoa ya Iringa, Mbeya na sehemu za mkoa wa Morogoro ya Kusini zinufaike.


    Kigoma kwa Mikoa yote ya Magharibi (Tabora, Rukwa na Kigoma) - ili kuvutia biashara na michezo na utamaduni karibu na Burundi, Rwanda na Kongo (K).

    ReplyDelete
  9. Mimi nadhani Serikali ifanye kazi ya kuwekeza kwenye miundo mbinu na watu binafsi na mashirika ndio wawekeze kwenye biashara kutokana na nguvu za soko. Mfumo wa kugawa viwanda kwa zamu ndio uliotumika wakati Tanzania tuko kwenye ujamaa matokeo yake viwanda vingi vilijengwa mahali pasipostahili kama Tanganyika Packers ikajengwa Dar ng'ombe wanatoka Shinyanga wapi na wapi?. Pia tukumbuke uwekezaji kama huo uliofanyike hapo Mlimani wawekezaji wamechukua mikopo benki inayohitaji kulipwa na riba, kwa common sense ya biashara huyu mwekezaji hata kwa bunduki hawezi kuwekeza biashara hii Singida au Tabora.

    ReplyDelete
  10. Nakuunga mkono kabisa katika hihlo Mzee Mjengwa! Naona tatizo ni kwamba Tanzania bado haiingii mikataba kiakili kama nchi nyingine. Angalia China!Ukienda lazima ujue watakudaka sehemu. Lazima utoe teknolojia kwa wachina , au ujenge kiwanda na mambo ya hivyo. Nchi nyingi ziko makini sana katika mikataba lakini sijui kwanini Tanzania kosa hili tunarudia kila wakati. Haya maduka lazima yangewekewa asilimia fulani ya bidhaa zao ziwe kutoka Tanzania. Nchi nyingine mpaka Televisheni kuna asilimia fulani lazima iwe ni local production . Sasa tusipoangalia tutaua kabisa soko la bidhaa za wakulima wa bongo . Halafu tutaendelea kulalamika kuwa vijana wanakimbia vijijini na kuwa vibaka mjini.

    ReplyDelete
  11. michuzi tunaomba picha ya amina chifupa mbunge wa viti maalum ccm nasikia kafanya mambo bungeni kuhusu wabwia unga.tunaomba habari kamili na picha yake pls.

    ReplyDelete
  12. Hawa wamezoea kutuuzia bidhaa zilizo-expire.Si mnakumbuka Shoprite yale makuku na minofu ya mbuzi na kondoo iliyo-expire?Muwe makini, nunueni bidhaa zingine lakini sio vyakula mtalishwa yaliyoexpire!!

    ReplyDelete
  13. Natofautina na wote wanaoogopa/wanaopinga uwekezaji. Sasa hizo nyanya na machungwa yenu machafu yasiyo na kiwanngo nani akubali kuyakuta ktk jengo hilo bomba? Boresheni bidhaa zenu zifikie kiwango cha kimataifa kiulaji zitawekwa tu hapo. Huu mradi ni bomba cha muhimu mkataba wake uwe na manufaa kwa TZ/UDSM kwani kuna uwezekano wa kuwafaidisha tu waliosaini makubaliano. Serikali isimamie kwa AKILI miradi ya uwekezaji kama huu ili tusilishwe vyakula vibovu na ajira tusiporwe. Serikali yapaswa kutathmini kwa kina mikataba ya uwekezaji KABLA badala ya kuwaacha akina Mangungo wa Msovero wakituumiza kwa maslahi yao.

    Nitapiga mtu sipendi wanaoipeleka TZ pabaya hasa wenye dhamana za umma walio mafisadi!

    ReplyDelete
  14. Ninyi kaburu Tunataka maduka ya bei rahisi humo kama JET, Mr. Price, Woolworth...... na parking yenye kivuli kama ya Nelspruit ebo! Jengeni kama kwenu! Msituletee mabo ya East Gate hapa!

    ReplyDelete
  15. Jamani hii ni private sector kazi ya kuweka miundo mbinu (infrastructure) ni ya serikali na sekta binafsi inawekeza kule ambako inafikiria kuna faida (ROI). Wawekezaji wameona kwamba kwa kujenga Dar kuna nafasi ya wao kurudisha mtaji waliowekeza. Hii ni kwa nchi mbali mbali. USA ukiwa New York ni tofauti kabisa na ukienda down south Missisippi. Tuwe tunafikiria kabla ya kukosoa kila kitu. Vitu kama hivi ni vya kuungwa mkono maana vitaleta ajira nyingi indirectly.

    ReplyDelete
  16. Du born again ilibidi tukupe urais wa nchi... hivi wahishimiwa wanatembelea hii blog Michuzi au kuna namna ya kuwafikishia mawazo ya wazawa kama hawa... kwani saa ingine mambo mengi wanapitiwa na great ideas kama hizi....

    ReplyDelete
  17. MIMI SIKATAI,HAYA NI MAENDELEO KATIKA NCHI YANGU,LAKINI NI WATANZANIA WANGAPI WANAUWEZO WAKUNUNUA BIDHAA KATIKA DUKA HILO?

    ReplyDelete
  18. Ewe Anonymous Mtoa Maoni, Wednesday, November 15, 2006 4:19:10 PM, asante sana.

    Naendeleza kuhusu kukua kwa Jiji la Mwanza:

    Mwanza imejengwa karibu na ziwa na milima, milima. Lakini sehemu ya Barabra ya Makongoro na Ziwa...toka daraja karibu na Hospitali hadi Barabara ya Kirumba Stadium kwenda Mlimani na Mwaloni... inaweza kabisa kuendelezwa kujenga upya ikiwa ni pamoja na kutengeneza sehemu hiyo ya kandokando ya ziwa kuwa Park na hoteli za kisasa.

    Endapo sehemu hii haitakidhi upanuzi wa Jiji, basi, Jiji lipanuke around sehemu za mkondo wa ziwa(lake bay) za Bwiru, Pansiansi kuelekea kcha ndege, ikiwa ni pamoja na kuwa na Marine itakayoshughulikia utalii wa Ziwa Victoria.

    Mwanza ina Kiwanja cha ndege. Kiwanja kipanuliwe kwa ndege kubwa za abiria ili watalii wanaopenda kuja kutembelea mbuga za wanyama za Serengeti watue hapo Mwanza kuliko kutua Kilimanjaro na kusafiri kwa magari au ndege ndogo hadi Serengeti na kurudia humo humo. Watalii wanataka sana ku-maximize vya kuona si kwenda na kurudi kwa barabara hiyo hiyo!

    Najua kuna projekti ya kujenga Kiwanja cha ndehe huko Mugumu, Wilaya ya Serengeti. Lakini hii itategemea kama mwekezaji huyo Mwamerika anayemiliki the private Grumeti Game Reserve atapendelea projekti yenyewe; anasitasita!

    Wananchi, hatuna budi kujenga miji yetu...siyo Dar es Salaam tuuuuuuuuuuuuuuu!

    Miundombinu ya kisasa ipo kwa mfano umeme na Internet connection. Tuwe na viwanja vya ndege vya kisasa, na kuna uwezekano wa ajira kwa lundo la vijana watafuta kazi. Miji hii au majiji haya niliyoyataja yanawezekana!

    Rais, Waziri Mkuu, Waziri Madini na Maliasili, Wakuu wa Mikoa (Kagera, Shinyanga, Mwanza na Mara - na ma-Erea Komishina wake), kama wana uchungu na madini yaliyomo katika mikoa na wilaya zake, ni lazima wasimame imara kutetea projekti hii. Tumechoka kunyonywa na kuzawadiwa eti 3%!

    Hao wawekezaji katika madini yetu ni lazima wachangie kulifanya Jiji la Mwanza kung'aa!

    Huyu ni Born Again pagan, signing off for now.

    ReplyDelete
  19. HUUNI ULAGHAI NA MKATABA HUU INABIDI UCHUNGUZWE. HATA MTANZANIA MWENYE HELA ALIKUWA NA UWEZO WAKUJENGA HAYA MABANDA. ENEO NYETI NA ADIMU HALIKUSTAHILI KUJENGWA HAYA MABANDA. ILITAKIWA ANAYEPEWA HII NAFASI AJENGE SIO CHINI YA GHOROFA TANU KWENDA JUU. HAPA KUNA WATU WAMEKULA HELA. PLAN ILIYOKUWA INAONYESHWA NI TOFAUTI NA HII. KWANZA WALIOPEWA HILI ENEO HAWANA HELA WAMEISHIA KUKOPA HAPA HAPA KWETU KWENYE MABENKI YETU. TANZANIA JAMANI TUNALIZWA MNO. TOO MUCH.

    ReplyDelete
  20. Wewe mzawa na wengine,
    Mkumbuke kuwa mtu anayewekeza hapangiwi wapi pa kuwekeza ila anachagua sehemu ambazo kaelezwa au panahitajika mwekezaji,nyie mnalazimisha angewekeza Dodoma!!HAIWEZEKANI HII,ni kama kuchagulia mtu mke au mume wa kuoa!!

    FIKIRIENI KWANZA KABLA YA KUTOA MAONI!!

    ReplyDelete
  21. ANON FRIDA 4.46.45PM usinichekeshe.... MTU ANAYEWEKEZA HAPANGIWI UNAFIKIRIA KWELI WEWE??? KWA HIYO ANA MAAMUZI HATA YA KUWEKEZA NDANI YA IKULU???

    OFCOURSE LAZIMA APANGIWE SIO KUINGIA TUU NA KUJICHAGULIA KAMA NAZI... HIVYO NI SERIKALI INAPASWA KUKAA NA KUFIKIRIA KAMA TUNAMKUBALIA MWEKEZAJI TUMPE ENEO GANI HIVYO WANA UWEZO WAKUKWAMBIA UKAWEKEZE EVEN TANGA KWA KUWA KUWEKEZA SIO TUU KUWANUFAISHA WAWEKEZAJI BALI NA NCHI NA WAZAWA... SO MY DEAR SERIKALI INA MAMLAKA YOOTE YA KUWAAMBIA WAENDE WAPI WAKIKATAA WANATOSWA VILE VILE .....

    ReplyDelete
  22. Suala hapa kubwa ni kwamba itawachukua watanzania miaka lukuki kuweza kungamua kuwa huwezi kuendeleza tanzania nzima kwa kuishi dar es salaam.

    Na hii nafikiri ingeweza kutatuliwa na mbowe Initiative. hatuna budi kugawana nchi katika kanda mbali mbali na kila kanda ifikirie kufanya mipango yake.

    Lakini hili tunalofanya sasa itakuwa ni vigumu sana bahadhi ya mikoa kuendelea. Kuna siku nilipita mikoa kama kagera sasa hivi inabadilika na kuwa kama kijiji kikubwa badala ya mji.

    Hawa waeshimiwa wanafikiri kuendeleza tu karibu na nyumbani kwao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...