
Safari Investment wamiliki wa ukumbi wa sherehe uitwao Safari Party Hall mjini Houston Texas wanafuraha ya kuwatangazia wabongowa ndani na nje ya Marekani kuwa kutakuwa na bonge la onesho la music live na Bongo Flava Queen RAY-C "binti mauno" jumamosi hii tarehe 30/12/06 music mpaka saa 12 asubuhi kwenye ukumbi wa: Safari Party Hall zamani "Hustonian"
9651 Bissonnet st
105 Houston
TX 77036
ukikosa usilalamike....
Jamani kuna tofauti ya kukodi ukumbi na kumiliki.Acheni,ujinga wa kipumbavu na ubabaishaji watanzania.Tujifunze walau kusema ukweli kwa kukaa ughaibuni.This makes me sick!!!
ReplyDeleteHuo ukumbi unamilikiwa na wa-TZ fulani hapo Houston , kipi cha ajabu kwa m-TZ kumiliki ukumbi ughaibuni? Stop being a hater!
ReplyDeleteWewe binti hapo juu, mbona una chuki binafsi?. Wako wabongo wenye mambo makubwa sana ughaibuni zaidi ya hall. usidhalilishe wabongo kama hawana uwezo wa kuwa na vitu kama hall. njoo ughaibuni ujihakikishie mwenyewe.
ReplyDeletejamani hivi sisi wabongo tunamatatizo gani? kwa nini hatupendani? mara tu jamaa hapo juu keshaanza kuandika upumbavu badara ya kufurahiya kwani wewe baada ya kusoma huo ujumbe umeshafanya uchunguzi kujua kama huo ukumbi umekodishwa kwa ajiri ya RAY-C tu? inamaana umeishaonakwamba wabongo waishio ughaibuni hawawezi kumili ukumbi kama wewe huwezi basi usijaji wabongo wote hawana akiri au uwezo wa kuweza kufanya vitu furani huwo tunauita upumbavu na chuki binafsi kwa mbongo mwenzio hebu tujaribu kupendana ili tuendelee kwa taarifa yako hawa jamaa wanafahamika huo ukumbi wanaumiliki, tafuta jengine.
ReplyDeleteAcha ushamba na chuki wewe anony wa kwanza furahiya wabongo wenzio wakifanya kitu cha kugenga maisha usitafute kuwafanya wajinga wengine kupondaponda vitu msivyovijua, jitahidini wana HOUSTON ndiyo inavyotakiwa.
ReplyDeletekwani kumiliki kuna maana gani wewe anony wa kwanza hebu wafafanulie wabongo labda kiswahili pia kinakubabaisha kwa kujifanya mjanja na kuwatukana watanzania wote maana umeandika "Acheni, ujinga wa kipumbavu na ubabaishaji watanzania." hivi watanzania wote tumekosa nini mpaka ututukane?
ReplyDeleteMwanadada Ray C anatesa!! Wabongo wa Houston, na wengine wote tum-support msanii wetu... this is our Beyonce!!!
ReplyDeleteAnony hapo Juu,wacha jazba mimi nimeelewa kuwa labda wame lease kwa muda fulani kama nyumba za kuishi zinavyo kuwa huku ughaibuni, ukisema hivyo inamaana asilimia kubwa ya watu hawamiliki nyumba zao.Labda tungeuliza kuwa ukumbi huo wame rent kwa siku moja ama wame lease kwa muda maalum?
ReplyDeleteAnany wa kwanza anaonekana ni mtu wa wivu sana, halafu ni mshamba fulani, anaongea bila kufanya uchunguzi na anaona watu wengine ni wababaishaji. Mimi binafsi namwona kama aidha amejaribu sana kutafuta alipoona amekosa akaona wengine waliopata ni wanga kwake, au akili zake zio nzuri kwa vile anatumia lugha ambayo ina generalise mambo. Ushauri wa bure kwake, hata kama ukumbi sio wao, yeye kinamuuma nini, si aache, RAY C ndo anajua na ndo mwalikwa, alaaah, hembu nyamaza hukoooo.
ReplyDeleteTatizo la wanamuziki wa Kibongo ni Mapozi yaani wanajiona Ma-Star wakati bado hawajafika popote na ni Chokambaya tu. Huyu Ray C alishakuja zamani akaharibu hadi show zake nyingine watu wakagoma kwenda. Akaja Mr. Nice akaleta vituko vya ajabu na kujifanya Diva la Kiume na hadi watu wakaboreka. Na sasa huyu Ray C anarudi tena, aje akijua asilete mapozi kwa sababu atajikuta pake yake na waandaji wake tu kwenye Hall.
ReplyDeleteTATIZO KUBWA LA WATANZANIA WALIO WACHACHE NI KUSUBUBIRI WENZAO WAJARIBU HALAFU KUANZA KUWAPONDA HUYO ANONY HAPO JUU ANA ULE UJINGA KUWAFANYA WATU WOTE WASHAMBA HASA WALE WALIO HUKU BONGO. JAMANI TUPENDANE TUSAIDIANE NA KUPEANA MOYO TUIGE WENZETU KTK COMMUNITIES NYINGINE AMBAO WAPO TAYARI KUSAIDIANA KWA KILA HALI SISI TUMEJAA MAJUNGU CHUKI UWONGO NA UZANDIKIILHALI HATUENDELEI MAJORITY YA WALIO HUKO UGHAIBUNI WANAISHI IL MRADI WAONEKANE WAPO HUKO INGAWA WANNYANYASIKA NA HAWANA MBELE WALA NYUMA SABABU YA TABIA ZETU CHAFU ZA CHUKI UWONGO NA UJUAJI MWINGI KUMBE HAKUNA LOLOTE.
ReplyDeleteWewe Anony wa kwanza umekosa cha kusema? kama umepigika na life kivyako sio kuponda usivyovijua acha wabongo Houston wakamue.
ReplyDeleteYou are sick from your own mental problems sio kusingizia ati watu hawasemi kweli huna adabu.
nyie anon wote hapo juu mnamponda huyo anony wa juu amekosa nini? huo ukumbi mmeununua au mmeujenga? kama ndio basi mnamiliki kama vinginevyo ni kwamba management yenu ndio inaendesha ukumbi huo kwa sasa kwa maana ya kwamba anytime mkivuruga mnatimuliwa kwa kuzingatia mkataba sasa basi ni kweli wa juu anaweza kuwa ameandika kwa chuki lakini neno miliki maana yake mna hati na kila kielelezo cha huo ukumbi lakini kama mnaendesha ukumbi basi si wamiliki pamoja na hayo yote ningependa kusema kwamba inaonyesha jinsi gani watz bado tuna safari ndefu sana sana michuzi katupa taarifa ya ray c kuja lakini comments kama 10 zinaonyesha jinsi gani watz tulivyo nyuma kimawazo,uungwana,heshima na adabu hebu tuamke sasa na kuwa mawazo endelevu.
ReplyDeleteray c kesho sio kutuvalia kama ulivyovaa hapo juuu ohooo(gauni la kuziba namna hiyo na mkanda juu)kama unaimba kwaya ya TOT!! hayo mavazi wavalie wabongo huko huko tanzania sisi tunataka kiuno nyororooo kionekane kabisa ukatike tuone hicho kiuno bila mfupa,nshasema hivyo kama mmoja wa wahudhuriaji naomba sana nakwambia mapemaaa ujue
ReplyDeleteSio kitu cha ajabu kwa mtanzania kumiliki nyumba ughaibuni,ukumbi na chochote ukijuacho wewe...sio ajabu hata kidogo.Kama nyumba ni yako,ni wazi una haki miliki na documents zote zinazothibitisha umiliki wa nyumba/jengo hilo.Kulipia jengo kila mwezi(rent)bila kuwa na hati za umiliki,ni wazi haikupi sifa ya umili.Huwezi ukawa unamlipa mama Kidawa pale Mwananyamala kodi ya nyumba yake kila mwezi,leo ukawatangazia watu hadharani unamiliki nyumba hiyo.Muulize mama Kidawa atakwambia....utakuwa na bahati kama hatakushtaki.You just can't do things like that guys!!!!Na mtu anaposema hivi huwezi ukaita chuki!!!!
ReplyDeleteSioni kwanini kunakuwa na ugumu kusema hali halisi.Sioni kwanini maoni hayo ya kwanza yanaonekana chuki ama roho ya korosho kama wachangiaji karibu wote walivyohitimisha.Kuna ubaya gani kukosoa mahali ambako uongo unapopewa nafasi ya ukweli?Wachangiaji waliopita wanajuaje mwandishi wa kwanza kama hakufanya utafiti kabla ya kuandika?Why are we getting so personal?Kwanini tunafanya judgments za haraka haraka bila kujiuliza maswali mawili,matatu.Ukweli ni kwamba ukumbi huo haumilikiwi na watanzania hao kama walivyodai.
Nakubali tuna budi ya kupongezana na kutakiana heri sisi watanzania,pindi mwenzetu anapofanya zuri.Kuendelea kukumbatia uzushi,uongo na unafiki hakutusaidii.Kwenye ngoma tuseme ngoma si TB wala kisukari.Ni lazima tujifunze kukosoana bila kudhani anyekukosoa anakuonea kijicho.Wenzetu wamefika hapo walipo kwa kupitia hatua hizi ambazo sisi bado tunajikongoja kuondokana nazo.
Naomba ieleweke wazi kuwa hakuna yoyote mwenye tatizo na Ray C kufanya concert yake kwenye ukumbi wa kukodi ama unaomilikiwa na mtanzania....hakuna.Imenisikitisha jinsi watu walivyorukia kuchangia negatively bila kusoma vizuri between the lines comments za mwandishi wa awali.We still have a very looong way to go.
I love u all.See you at the concert.
anony hapa juu yangu nakupongeza kwa kiswahili kizuri chenye sentensi za kunyooka kweli kweli, nimesoma viswahili vingi tuu lakini hiki chako kimenifurahisha kwa mtiririko wa uandishi nimeelewa ulichosema lakini kikubwa ni jinsi ulivyopanga maneno nimekuwa nasoma mpaka nasikia raha,kwenye kupongezana lazima tupongezane hongera sana.
ReplyDeleteWewe anony hapo juu uliyemjibu anony pale juu ambaye alimjibu anony yule juu, nadhani hukumuelewa anony alivyosema kuhusu maoni ya anony, na ukifuatilia aliyosema anony chini yake utaona kuwa anony huyo yuko sawa.
ReplyDeleteHonest speeking the owner are Tanzanian. The concent was worse, however the laidy gatta the voice. Things that she need to learn is, first the power of being on time. second, singing is business and business has the rules that need to be followed in order to succeed. Third, audience are customers and they deserve customers service, she real need to learn on this sector, for instance i left Tanzania long time when there is no Ray C word on no body mouth, so i know her music through Kajumulo DVDs, so when we asked to hear the song that we know even thrice we mean it, dont ever turn a customer off.
ReplyDelete