
aliekuwa mkuu wa mkoa wa tabora athumani ukiwaona ditopile mzuzuri akiwa mahakamani kisutu leo ambako alifikishwa na shtaka lake la mauaji kusomwa kwa mara ya tano. litasomwa tena katikati ya mwezi huu ambapo waendesha mashataka wanatarajia kuwa jalada la kesi hiyo litakuwa limeshafika kwa mwanasheria mkuu kwa maelekezo zaidi. kesi za mauaji husomwa mahakama kuu pekee, ila ni baada ya faili la kesi husika kupitia ngazi zote na kuridhisha kwamba kuna kesi ya mauaji ya kujibu.
ILANI: WADAU! HII NI HABARI ILOTOKANA NA TUKIO LILITOKEA MAHAKAMANI LEO, NA NI HAHALI KURIPOTIWA KAMA HIVI. NI KINYUME CHA SHERIA KWA MTU YEYOTE KUJADILI AMA KUHUKUMU KESI HII KWA NAMNA YOYOTE ILE. NI VYEMA UKAE KIMYA KULIKO KUTAKA KUJIFANYA JAJI/HAKIMU.
Michuzi umenichekesha sana na hiyo warning yako in Capital letters. Comment ni comment tu haiwezi kuwa hukuma may friend.
ReplyDeleteanatia huruma maskini lakini ndio muuaji tena kama saaadam tu alinitia huruma walivyomtia kitanzi jamaa anaongea tu mpaka dakika ya mwisho wanaachia mlango aning'nie mhhh ama kweli dunia hiii ina mambo pole dito lakini uliyofanya ni yale yale ambayo kila mtu siku zote anaishia kusema Ningej............
ReplyDeletemichuzi acha unafiki bwana sababu ni dito? angekuwa mtu mwingine yeyote usingemweka usimuogope huyo kashaapewa uraia wa wakawaida kama mimi angalau hata wewe unaogopesha teh teh...sasa basi acha tumwage maoni yetu after all hukumu yoyote dhidi yake iwapo itakuwa nje ya mbili (kunyongwa au kifungo cha maisha) basi nashauri serikali iliyopo iachie madaraka naomba utoe maoni yangu pliiiiiiiiiz michuzi
ReplyDeleteMbona una shout namna hiyo Michuzi. Unatisha watu sio?
ReplyDeleteduh michuzi sasa na wewe umeanza kuwa mwanasiasa huyu mtu kauwa tena kwa makusudi sasa wewe unatuletea habari alafu unasema tusizungumze kama kweli ameuwa unafikiri kweli utatufunga midomo wakati wewe ndiyeuliyeweka hii habari wacha turushe nyuki usitujime raha bwana tunanajinafasi kwa kuwa hatumsingizii kiukweli amemuhuwa mtoto wa watu mwache na yeye akanyongwe au kifungo cha maisha
ReplyDeleteMichuzi achakufanya kitu kwa kujiami Brother.Ungetaka tunyamaze kimya usingemuweka uyu Mh,Ww unamuweka thn Unatoa onyo tukuelewaje?Ata mungu apendi icho kitu bwana.Usirudie tena kuweka kitu thn useme NO COMM WEEEE!!. UTATUTIA HASIRA UMESIKIA HAYA TUMEKUSAMEHE.AU SIO WANA BLOG?REEN APA.
ReplyDeleteissa unakava engo zako najua. lakini dito muuaji, na kama ilivyo sheria lazima aning'inizwe.
ReplyDeletemichuzi unachekesha sana na hasira zako nahisi ungekuwa na uwezo wa kutuona ungetudito pia.
ReplyDeleteUnajua Michuzi wakati mwingine inabidi tukuelewe kutokana na system inayokupa mkate wako waki la siku ila hili la warning umechemsha vibaya. Hata hao wanasheria wanaojidai kusema ati tusiongelee kesi hii hawatupi kifungu cha sheria kinachozuia kufanya hivyo. Dito alijihukumu mwenyewe baada ya kuamua kumshindilia mtu risasi mbele ya kadamnasi watu wa comment wasicomment ukweli unasimama pale pale. Aliua mtu in cold blood.
ReplyDeleteKama kesi itakuwa ya haki, na Dutopile akipata lawyer mzuri, hiyo ni second degree murder, ambayo ni kuua bila kuwa mpango wa wali, au plan ya awali kabla ya tukio. Kwenye Criminal Justice tunaiita, killing out of passion without premeditation, ambapo mtu anaweza kuua kutokana na(kwa mfano) mabishano makali, au mtu katukanwa akakasirika akampiga aliyemtukana akafa. Kwa hapa U.S. kesi kama hiyo mtu hupewa 25 to life, kutegemea na state ilipotokea tukio. Lakini prosecution inaweza kusema kuwa Dito hakuwa na haki ya kumtaka dereva ashuke kwenye dala dala kwa kuwa hiyo ingekuwa kazi ya polisi wa barabarani kupata taarifa za ajali. Na pia prosecution inaweza kusema kuwa Dito alitumia extra force/deadly weapon mahali ambapo angeweza kutumia kitu kingine kama ngumi, au kipande cha mbao, badala ya bunduki. Kwa mtazamo wangu, kwa kuwa ni second degree homicide, anaweza kupew miaka kadhaa ndani.
ReplyDeleteHakuna Jaji wa kumnyonga Ditopile tanzania labda waajiri wale majaji kutoka Nigeria ,Zitapasuliwa nazi mpaka kieleweke Wameuwa watu wengi tuu nongwa kwa kuwa yeye ni Uncle Dito mtoto wa mjini wameuwa ma IGP enzi za utawala JKN na kuishia ubalozini sembuse yeye na kipindi hicho ndo tunasema kilikuwa na utawala wa sheria chini ya pilato mkakamavu haya kuna familia mmoja ambayo sasa hivi iko kidedea na ari mpya na kasi mpya ambayo mdogo wao alimrusha mtu gorofani pale Upanga jee mmesahau hilo na sasa hivi kaka yake ndo kibosile wa madanta na aliyekuja na swala la shut to kill ,hebu hamkeni kidogo huenda kuna vijana wengi humu ndani hivyo kuna ufinyu wa historia mambo ya enzi zile za Uhuru ,Mzalendo ,Mfanyakazi na kiongozi.
ReplyDeleteSina hukumu lakini sitashangazwa na lolote lile litakalotokea
Najua Ditopile anajua that he really messed up, lakini bado anategemea wenzake wamsave. Kigumu zaidi ni kwamba hii imetokea wakati wa kikwete, siyo mkapa. Mkapa angemwambia ebwana mkondo wa sheria utachukua mkono wake, utajiju! Lakini kikwete ni mtoto wa mjini kama yeye, ni mwenzake huyo sheikh!
ReplyDeleteItakuwa very interesting kuona jinsi kesi hii itakavyokwisha, I hope vyombo vya habari, ingawa sivitegemei sana, kama mr. michuzi is any indication, vitatupa full coverage jinsi inavyoendelea.
Nilianza kuona dalili kwamba kesi hii itapindishwa toka siku ya kwanza, matter of fact, mara tu niliposikia habari ya tukio. Then nikaja kusikia kikwete anampa pole wakati yupo korea, halafu viongozi wakubwa wa serikali na ikulu wakaitembelea familia ya marehemu na kutoa 'ubani', nikajua this is going to be interesting.
Mimi sina cha kutabiri au kuhukumu, lakini sina mategemeo mengi kwa justice system yetu. I don't like to be dissapointed, but, I'm watching!
MZEE MICHUZI KWELI UNAFURAHISHA SANA KATIKA BULOGU HII MAANA UNARIPOTI KILA KITU VILE KINAPOTOKEA NA KAMA KILIVYO, BILA YA CHOYO, WALA KUPENDELEA WOTE UNATUPA HAKI SAWA.
ReplyDeleteHII KESI WANANCHI WOTE TUNASUBIRI HAKI ITENDEKE, JUSTICE TO BE DONE. KIKWETE HAPA ANA KAZI NA NDIO TUTAONA NI MUUNGWANA KWELI AU VIPI, MAANA DITO NI MSHKAJI WAKE, LAKINI AWE FAIR NA HAKI KWA WATANZANIA WOTE.
ASANTE MZEE MICHUZI.
Dito ni mlemavu wa mikono, in case una define mkono kama kitu chenye uwezo wa kupiga ngumi. Hii tunaita miwa sio mikono. Tumia hilo kujustify adhabu uliyotoa Dito. Au sema, ulikuwa ndotoni. halafu ita madokta toka nje waje ku-confirm kuwa kuna watu wanaota huku wakiwa wanatembea mtaani utadhani wako macho, dreaming while awake. Ukishinda kesi hiyo, nami ntagushi hela halafu niseme nilikuwa naota, ntarefer kesi yako, nisafishie njia bro Dito.
ReplyDeletekaka issa tunajua alikua rafiki yako,lakini mh!hapo inabidi uache ukali tu maana hata sadam hussein kelele haikumsaidia .
ReplyDeletesasa tuone kama kweli we na kikwete huyo jamaa mtamsaidiaje.bora mtutolee kocha na babayake.
Hivi wanangoja nini kum-dito kwa kamba shingoni?
ReplyDeleteebu nielimisheni, kupiga picha mahakamani ni ruksa?
ReplyDeleteKupiga picha mahakamani. Sijui kama ni ruksa, ila hiyo picha inaonekana kama imepigwa wakiwa kwenye lobby ya mahakama wakati wanasubiri kuingia kwenye court room. Ila wakati court is in session, hapo ndio nadhani kamera huwa zinakatazwa. Ila kwa U.S. hiyo hutegemea na jaji kama ataamua kuruhusu kamera au la.
ReplyDeleteunaye sema kikwete ana kazi, kwa JK ndo atakuwa hakimu au wakili? ...waupande gani !?
ReplyDelete