nchi zingine hurahisisha mambo kwa kuweka alama sahihi kuelekea maliwatoni. kwa sababu za kidiplomasia naomba nisitaje jina la nchi kwenye mambo haya. ila nakaribisha maoni kama hii ni sawa ama la. na je utamaduni huu sisi wa hapa bongo unafaa kuiga? toa sababu. mwenye maelezo bomba namba zawadi. msitari mfu ni jumamosi ijayo saa sita mchana...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. michuzi huna haja ya kuficha, hapa ni Sweden. Hawa jamaa jamii yao iko wazi sana. Nafikiri hizi alama ni ubunifu badala ya kuweka zile ndogo ndogo tulizozoea za mwanaume au mwanamke ambazo kama mtu umekata kilauri cha kutosha inakuwa taabu sana kuziona.

    ReplyDelete
  2. kuchora picha ya jinsia ya kike au ya kiume ikiwa imevaa nguo ni bora zaidi, ila inaonyesha kuwa matumizi ya washroom ni general(nafikiri nimeeleweka), ila kama matumizi ni specific kama vile ''haja ndogo'' au ''kubwa'' kwa bongo haifai kuweka picha halisi, ila unaweka maandishi tu inatosha kwani. ila kwa nchi yenye kuweka picha kuashiria nini hasa cha kufanya ukiingia humo si mbaya kulingana na utamaduni wao

    ReplyDelete
  3. michuzi mimi nikiwa km mtanzania napenda kutoa ushauri kuwa siyo kitu cha ajabu kuweka alama kama hii mlangoni siyo kitu cha kusema kuwa kinaaribu utamaduni wetu kwani ni njia moja wapo ya kurahisisha mtu kujuwa wapi anapaswa kuingia kwani kuna watu wengine wana matatizo ya kuona vizuri au kusoma lkn kukiwa na alama ya namna hii kunamasaidia mtu mara moja kuelewa wapi aingie vile vile tuna paswa kuwa na mawazo endelevu kwani hicho ni picha ya kikaragosi sio maumbile ya mtu wala picha ya mtu hivyo akuna umabya wowote ule thnx michuz

    ReplyDelete
  4. Huo ni utaratibu wa Sweden.
    Lengo ni kurahisisha uelewa kwa wageni.
    Bongo ukifanya hivyo watu hawatakuelewa. Nafikiri ni kutokana na utamaduni wetu wa kuheshimu privacy.

    ReplyDelete
  5. hiyo nchi ni ya watu wasio na uwezo wa akili period,maana hata mtoto wa miaka mitatu anatambua urahisi wake katika kujisaidia na mara anafata mkondo huo kigumu kwakwe chaweza kuwa maneno maana anahitaji kufundishwa kwamba women ni nini na men ni nini? hivyo basi hatuhitaji utaratibu huo hata kidogo hakuna cha ajabu lakini ni vitu ambavyo mtu analearn naturally.

    ReplyDelete
  6. Hii picha inaleta utatanishi kwa sababu inaweza kuwa ni mwanamume rasta anayekwenda haja kubwa!

    ReplyDelete
  7. Michuzi,
    Hiyo picha inapotosha! Ukiwa mwanamke huwezi kuelewa zaidi ya hayo maneno yaliyoandikwa kwa sababu mkojo wetu hautoki mbele zaidi ya mwili!..
    Huyu jamaa nilifikiria Rastaman anajisaidia!

    ReplyDelete
  8. Nimeshaingia vyoo vingi, sehemu mbalimbali za dunia, lakini ni mara ya kwanza kuona alama zinazoeleweka kama hizi!!
    Hizi alama za chooni-zimeweka kuweza kusaidia hata wale wasiojua kusoma na kuandika. Nafikiri hapa hakuna atakayeshindwa kuelewa.
    Swala la utamaduni sio muhimu kwa sababu ni kuhakikisha kuwa wanaume hawaingii kwenye vyoo vya wanawake bila kujua au wanawake kwenye vyoo vya wanaume. Hizo alama nafikiri zinatimiza hilo lengo.

    Napenda kuchukua hii nafasi kusisitiza jambo la muhimu zaidi ya maswala ya alama za vyooni. Hili ni swala la usafi wa vyoo. Kuna juhudi zinafanyika pale Dar za kuweka vyoo katika hali ya usafi, mfano kwa kufanya watu walipie huduma, na pesa zinazopatika kusaidia kuviweka vyoo katika hali ya usafi. Usafi wa vyoo ni muhimu sana, ukizingatia kuwa jiji la Dar limekuwa likikumbwa na ugonjwa wa kipindupindu mara kwa mara.

    ReplyDelete
  9. Mimi sioni hata cha kuiga hapo.Hayo ni mambo ya kawaida.
    Hatuwezi kuwa "innovative"kwa mambo yetu?!

    ReplyDelete
  10. Kaka michuzi mbona hujaonesha picha zote kwenye hiyo park? kwakweli mi sidhani kama kila kilicho nje ya nchi yetu ni kizuri kwetu , kwa hilo tu hatutakiwi kuiga... naamini viashiria vinavyotumika sasa vinatosha kabisa kutoa maelekezo ya eneo la kwenda kwa ajili ya shughuli hizi.
    Mwisho, utamaduni wa Kitanzania umegubikwa na staha na heshima pamoja na soni, kitu ambacho ni kizuri... nadhani tukiiga viashiria hivi sasa kwa wodi ya wazazi itatisha zaidi!

    ReplyDelete
  11. ningependa kujua ni nchi gani hiyo. labda wangependa ushauri. nadhani wamefanya hivyo kwa kuwa kalcha yao inaruhusu kitu kama hicho kionekane kama burudani ama refreshimenti ya kumpatia mtu angalau nusu-kicheko. kwetu wadau hii inacheza kwenye mpaka..

    -mdau wa chunya-

    ReplyDelete
  12. Nafikiri huu utaratibu huu wa kuweka alama ni mzuri kwa nchi yetu hasa ikizingatiwa kuna watu wa kila aina na lugha tofauti kwani unarahisisha watu wa lugha tofauti kutokuchanganyikiwa/kutokuelewa hasa watu wasiongea lugha ya Kiswahili au kiingereza.

    Kwa mfano nchi nyingi za ulaya hutumia neno WC (Water Closet). Ambayo inaweza kuleta mtu kuchanganyikiwa/kutokuelewa kwa watu ambao si wazungu. Vilevile Phillipines hutumia neon CR (Comfort Room) ambalo kwa watu ambao sio wenyeji wa sehemu hio inalete maana tofauti kabisa.

    Kwa hiyo mimi ninafikiri ni vizuri tukiiga mfano huu mzuri wa wenzetu wa Korea.

    ReplyDelete
  13. sasa rasta hizo ndizo zimechanganya zaidi.

    ReplyDelete
  14. Nyie mnaodai hapo sweden mna ushahidi? Mbona Michuzi kazipa majina hizi picha kuwa ni Korea ukizidownload?

    ReplyDelete
  15. Kiongezaji bora kutazama vituo vya Runinga kwenye LiveNet addon yako bure kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...