nipo nangurukuru mkoani lindi katika harakati za janta. pana mahindi matamu sana ya kuchoma hapo - samaki nchanga sikuwaona...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Michuzi Barabara Mkeka kama za Dar? Nakumbuka hapo na NJINJO ni maarufu sana kwa samaki wa kukaanga.....hahahahhahahaha barabara yote ilikuwa imejaa Mchanga

    ReplyDelete
  2. Nadhani serikali na wahusika wataupata huu ujumbe toka kwenu wanafunzi mliopo Ukraine ambao ni madaktari/wafamasia watarajiwa, ili muweze kumaliza masomo yenu na kwenda kutumikia wananchi Tanzania. Juzi tulimsoma katika mtandao Mh. Raisi JK akitoa ahadi za kuwajali wanafunzi ili waweze kusoma vyuoni bila matatizo ya karo na fedha za kujikimu, nadhani kauli yake haibagui kama ni mwanafunzi nyumbani Tanzania au wale wadhaminiao na serikali nje ya nchi.

    ReplyDelete
  3. Bw. Michuzi umenikumbusha mbali saaaaaana!!!

    hahahahahahaahahhahah!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Sasa Bro Michuzi nasikia eti siku hizi lami hadi Mtwara. Mbona hapo bado naona dongo jekundu? Nakumbuka hapo kulikuwa na songombingo sana enzi zile je bado zipo. Kulikuwa na tope la kufa mtu. Usisahau samaki wa hapo watamu sana. Haya bwana we nikumbushe tu!

    ReplyDelete
  5. Mambo ya Nangu hayo mwanangu.Hilo ni Akida bus (la waarabu wa Ikwiriri,Rufiji).Linawakomboa sana watu wa Lindi,Masasi,Newala,Mtwara na Tandahimba.Lakini hii picha ni ya zaidi ya miaka miwili iliyopita.Eneo hilo sasa hivi lina kituo cha mizani ya kupimia uzito wa magari.Toka Nangurukulu kuna lami hadi kijiji cha Mandawa.Kampuni ya CICCO ya Uchina ndiyo inashughulikia eneo hilo na wamejenga madaraja mazuri na makubwa mto Mavuji na mto Mbwemkuru.Kama wataendelea kwa kasi waliyonayo basi lami itafika Mbwemkuru (95 km from Nangurukulu) mwezi wa kumi hivi.Kutoka Mingoyo (Mnazi Mmoja),Lindi hadi Mbwemkuru ujenzi unafanywa na kampuni ya M.A.Kharafi&Sons.Wamejenga madaraja imara ktk maeneo korofi kama Ngongo,Mtange,Mmongo,Mchinga,Kilangala,n.k na pia earthwork yao imefika karibu na Mbwemkuru.Wameanza kuweka lami toka Mingoyo kuelekea Lindi mjini na wako maeneo ya Machole sasa ila hadi mwezi wa saba au wa nane watakuwa wamemaliza km 95 zao.Kwa mliotoka zamani kusini ni kwamba kuna lami pia toka Somanga-Njia Nne-Matandu-Nangurukulu. Lami ya Dar-Mkuranga-Kibiti sasa hivi ipo maeneno ya Kibiti Sekondari na itaungana na lami ya Ikwiriri pale Kibiti mjini miezi michache ijayo.Hii inamaanisha kwamba hadi mwisho wa mwaka huu (2007) ni km 60 tu toka Nundu (mwisho wa daraja la Mkapa)-Muhoro hadi Somanga ndio zitakuwa hazijakamilika kwa kiwango cha lami kati km 508 za barabara hiyo ya Dar-Kibiti-Lindi-Mingoyo.Pia umeme wa gesi unaingia Lindi mjini mwezi ujao mwishoni toka Mtwara.Wadau mliotoka huku zamani au mliowahi kupita huku rudini muone utofauti na miaka hiyo na pia muwekeze;hili ni kwa watanzania wengine pia.Nayazimika sana maembe dodo ya kusini,korosho,karanga,samaki,matikiti,nazi,machungwa na mabo kibao.Michudhi aminia mdhee kwa picha hii,leta dhingine bathi!

    ReplyDelete
  6. nimekumbuka enzi zileeeeeeeee wow!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...