
jk na jaji mkuu mh. barnabas samatta wakipozi na majaji wa mahakama ya rufaa aliowaapisha leo ikulu. majai hao (wenye majoho) toka kushoto ni mh. vicent lyimo na mh. mbaruku salim mbaruku na mh. laurian kalegeya. sio mbaya ukapata mapya ya bongo kwa kubofya hapa
Hivi majaji wa nchi hii kazi yao ni kusubiri kesi ije kwao ndio waamue? Hawawezi mshauri Raisi hata kwa siri wakiona bomu liko njiani kumlipukia?
ReplyDeleteKuna hoja ya kadhi iliyojaa harufu ya dini ambayo inapoteza mamilioni ya pesa za watanzania na majaji mmekaa kimya na wabunge wako kimya.Shauri yenu.
Ni lazima mjue kuwa nchi hii si ya Raisi,Wabunge au majaji peke yenu ni ya watanzania wote.Si vizuri hiyo mihimili mitatu ya dola mkajifanya mna genge la kuendesha nchi peke yenu na kuchezea fedha mpendavyo kwa hoja zenye harufu ya dini kama ya kadhi.Mjue kuna watanzania ambao nchi hii ni yao pia na wana uchungu wa nguvu na hawatawaacha muendelee kufanya mtakavyo.Nchi hii si kama ile ya wakati wa Nyerere,Mwinyi au Mkapa.Kikwete kama ulivyowashangaza wenzio kuwa raisi na wewe ujiandae kushangazwa.Kama husikilizi washauri wako au umewanyamazisha kwa makusudi utajuana mbele kwa mbele na wananchi ila usije ukashangaa na majaji na wabunge msije mkashangaa!
Ninawahakikishia nyie mihimili mitatu ya dola hoja hii ya kadhi mnayoendekeza itawatokea puani wote nyie kwa mpigo.
Sir Issa naona WAHESHIMIWA WAKO MGUU SAWA...KANZU ZINAPENDEZA NASUTI ZAO POA WAZEE WETU HAWA...NINAUHAKIKA JK KESHAFANYA BOOKING NA TIKETI ANAYO ANASUBIRI TIME TU...
ReplyDeleteNchi nyingi ambako watu hupigana hutokea hivyo pale mihimili mitatu ya dola yaani Serikali,Bunge na Mahakama wanapoungana na kuwa kitu kimoja kwenye kuvunja katiba.
ReplyDeleteKwa ufupi suala la kadhi ni uvunjaji wa katiba na kama Raisi au bunge likivunja katiba inabidi wote watimuliwe maana wamevunja katiba waliyoapa kuilinda hivyo inabidi watimuliwe uchaguzi uitishwe upya.Nadhani serikali, wabunge na majai wa Sasa wanataka serikali itimuliwe ndiyo maana hawataki kumshauri Raisi hatari inayomkabili.Serikali inachezea moto.Kuna watu wanataka Kikwete asimalize hata miaka mitano ya utawala na wamejichomeka kwenye hoja ya kadhi ili wahakikishe anaondoka kwa Kuvunja katiba.
Kikwete kaa mbali na hoja ya kadhi moto uko njiani.Kama huwa unaziba masikio kwa mengine hili usithubutu kuziba masikio.Sio siri utaondoka wewe na serikali yako,wabunge na majaji wako wote sababu nchi haiwezi endelea kuwa na majaji na wabunge wasiojua nini la kufanya wanapoona hatari mbele.