nimepokea ujumbe huu toka tokyo, japan, kwa wadau wenzetu...
NDUGU WANACHAMA WA UMOJA WA WATANZANIA WAISHIO JAPAN NA WATANZANIA WOTE NA MARAFIKI ZETU WOTE, WIKI YA "MISUKO X 2" (GOLDEN WEEK) UMOJA UNAWALETEA MAMBO YA KUPENDEZA YATAKAYOKUFANYA KUPUNGUZA UCHOVU WA PILIKAPILIKA ZA JAPAN NA KUJISIKIA UPO BONGOLAND.
MAMBO YAKOJE TEGA SIKIO:MSANII MAARUFU TANZANIA MWANADADA, JUDITH WAMBURA AU LADY JD AU JIDE UKIPENDA MUITE KOMANDO ANATUA NDANI YA JAPAN TAREHE MBILI (2/5/2007) NA SIKU YA TAREHE TATU(3/5/2007) ATAFANYA MAHOJIANO NA NHK IDHAA YA KISWAHILI, SIKU YA TAREHE 4/05/2007) IJUMAA KUANZIA SAA 1.30 JIONI HADI 3.30 USIKU ATAANZA KUFUNIKA NDANI YA NIPON AMBAPO JIONI ATAKUWA ROPPONGI PALE KATIKA CLUB YA MAARUFU "BRONZE PALACE" ILIYOPO GHOROFA YA PILI KATIKA JENGO LA TSK, 7-15-2 MINATO KU, 106-0032 ROPPONGI TOKYO, KWA MAELEZO ZAIDI AU UKIKWAMA PIGA SIMU # 0357755707 WASILIANA NA EDWARD.
NJOO UONE LADY JD ANAVYOFANYA VITU, KIINGILIO HAPO NI YEN 4000 (ELFU NNE).HIYO ITAKUWA NI MWANZO TU WA MAKAMUZI, KWANI SIKU YA TAREHE 05/05/2007 HAPO NDIO PATAKUWA HAPATOSHI KABISA KWANI, KATIKA UKUMBI WETU WA NYUMBANI HON ATSUGI MWANADADA HUYO PIA ATAJUMUIKA NA WATANZANIA KATIKA SHEREHE NYINGINE KABAMBE, YA KUKATA NA SHOKA AMBAYO INAONGOZWA NA JOPO LA MA DJ, WAKIONGOZWA NA DJ MAARUFU DJ PEMBE, MZEE WA MAMBO MAZURI NA WAZIRI WA STAREHE BILA KUMSAHAU MKONGWE DJ EDDY TO THE S., VIONJO VYOTE VYA KUKUFANYA UJISIKIE UKO KILA NCHI VITAKUWEPO, TAARIFA KAMILI YA USIKU HUO WA KUFURAHISHA NA KUSTAREHESHA ZITALETWA KWENU PUNDE SI PUNDE, "KAA MKAO WA KULA MWANANGU"KAMA KAWAIDA, UKISIKIA USIWE MCHOYO WASHTUE WASHIKAJI WA MASKANI ZOTE, ILI WAONDOE STRESS NA WAO.MAMBO YAHO !!! NI BANDIKA BANDUA!! HADI LUKWILI!!

WAKO,
KITUGOD

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. jamani yeni moja ni shilingi ngapi, na jd atapewa ngapi katika hizo, au ndo kutumika tu wajanja wafaidi?

    ReplyDelete
  2. nakuaminia mdogo wangu jd wachengue hao,ila angalia wasikulalie kwenye mapesa ukaishia kuomba nauli ya kurudi, maana.......

    ReplyDelete
  3. Hiyo inakaribia Tshs 43,000 kazi kwenu watu wa MINATO KU..

    ReplyDelete
  4. Hii yen 4000 ni ndogo sana kwa huku, tatizo linakuja kama unakaa mbali na Tokyo, itakugharimu zaidi.

    ReplyDelete
  5. Jamani wakati wa kuandika ujumbe kwa jamii inatupasa kuwa makini sana na lugha tunazotumia manake kwa kitu kidogo tu ni rahisi kwa watu kupuuzia kile ulichokusudia kwao. Mfano ndugu yangu hapo juu ameandika neno Misuko x 2 sijui anachokusudia hapo. Naomba ikiwezekana nipewe ufafanuzi juu ya hilo, kivipi limetumika na lilikusudiwa kumaanisha nini hapo?

    Natoa Hoja.

    Salaam.

    Mti Mkavu.

    ReplyDelete
  6. Jay dee una kitako now days loh!! hongera mama

    ReplyDelete
  7. Sir Issa vipi Kaka..Lady Jay dee..sauti yake si haba..KOO LIMEUMBWA..LIKAUMBIKA...ILA MWILI HALALI YAKE MWENYEWE..NAONA KAKA PICHA MPAKA UPEPEPO UPULIZE...NDIO MAANA ISSA AL-MAARUFU...DIZAINA WAKE MBUNIFU KAKA...

    ReplyDelete
  8. Kitako cha jide kimetuna sijui kavaa pampasi au nepi au ni upepo ndo umefanya mambo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...