
WAKENYA WATAWALA MBIO ZA FLORA LONDON MARATHON
Na Saidi Yakubu, London, Uingereza.
Mashindano ya Flora London Marathon yamemalizika kwa wakenya kuibuka kidedea kwenye nafasi za mbio ndefu baada ya Martin Lel kumshinda mkenya mwenzie Felix Limo aliekuwa bingwa mwaka jana.
Mashindano hayo yalishirikisha wakimbiaji zaidi ya elfu thelathini ambao wengi wao ni watu wa kawaida kabisa ambao wamedhamini vyama visivyo vya kiserikali vinavyosaidia makundi ya kijamii yenye kuhitaji misaada, hufanyika kila mwaka na kudhaminiwa na kampuni ya siagi na vyakula ya Flora.
Bingwa wa mwaka huu, Martin Lel alimaliza mbio hizo za maili 26 baada ya kukimbia kwa masaa mawili, dakika saba na sekunde arobaini na moja ambapo aliwashinda kwa sekunde sita tu mshindi wa pili Ghoumri na mkenya Felix Limo. Hata hivyo mwanariadha mwingine maarufu Haile Gabresselassie wa Ethiopia alishindwa kumaliza mashindano hayo baada ya kuishiwa na pumzi akiwa amekimbia maili kumi na tisa tu.
Martin Lel alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa anaona ni fahari kwa Afrika nzima kwa Waafrika kushinda nafasi zote tatu za juu kwa upande wa wanaume, ''nachukulia ni fahari kwangu, kwa nchi yangu ya Kenya na pia Afrika nzima kuweza kushinda tena'' alisema.
Hata hivyo mwafrika pekee kushinda kwa upande wa wanawake alikuwa ni Gete Wami kutoka Ethiopia ambae alipata ushindi wa pili nyuma ya mchina Chunxiu Zhou aliemaliza kwa muda wa masaa mawili, dakika ishirini na moja na sekunde 45.
Hata hivyo mashindano hayo hayakuwa na mwanariadha hata mmoja kutoka Tanzania. Mbio za London Marathon ni moja ya mbio maarufu sana duniani ambazo zinaambatana na kitita cha dola laki moja kwa mshindi wa kwanza na mikataba kadhaa ya matangazo ya bidhaa za michezo. Hii inaashiria kuwa Tanzania inaelekea kupoteza sifa yake katika mchezo wa riadha ukilinganisha na miaka ya themanini enzi za kina Filbert Bayi na Juma Ikhangaa.
Saidi Yakubu London Correspondent BBC SWAHILI SERVICE Bush House London WC2B 4PH Tel: 0207 557 1620 Mobile: 07708407483 Fax:: 0207 240 4637


Said unatumia hili neno "Hata hivyo" Mara nyingi mno bro !
ReplyDeleteKwa nini Tanzania haikuwakilishwa? Kwa nini watanzania mnaobeba Mabox Uingereza msijitokeze kutuwakilisha kwa kukimbia hizo mbio?
ReplyDeleteHivi kipi rahisi kupata Kukimbia kwenye ghala ukiwa umejitwika box au kukimbia bila box kichwani kwenye hizo mbio za Marathon?
Hivi wameba mabox hamuoni kuwa hiyo ilikuwa nafasi yenu ya dhahabu hapo London?
Naamini kama watanzania wabeba mabox wangejitolea kukimbia tungeondokana na hii aibu ya kukosa mwakilishi wa Tanzania huko London marathon.
Tunashukuru kwa mchango wako hapo juu (ingawa ni pumba tupu). Hii inaonyesha upeo wako wa kuelewa.
ReplyDeleteLakini nashangaa umeshindwa kuelewa kuwa asilimia kubwa ya wabeba box wamejilipua na hivyo tayari walisha-ukana uraia wa Tanzania.
Ndugu uliyetoa wazo la kwa nini wabongo wanaoishi UK wasishiriki kwenye hizo marathon, kwa upande wangu nafikiri umekosea sababu mbio kama hizo siyo unaamka tuu na kwenda kushiriki kwanza inatakiwa uwe na kipaji na afya yako ni njema ndipo utumbukie katika hizo mbio. Kwa hiyo nafikiri ungepima hayo kabla ya kwenda na kuzungumzia watu kutoshiriki na kazi wanazofanya hazina uhusiano na hayo mashindano, jaribu kupima mawazo yako kabla ya kutuma hoja zako.Cha msingi ni kujiuuliza kwa nini nchi yetu imepungukiwa na washiriki wa hizo mbio, tufanye nini ili turudishe heshima yetu?? nchi kubwa katika A. Mashariki ikose mwakilishi???
ReplyDeleteYakubu kafanya uzuri ku-highlight kuwa hakukuwa na mbongo alieshiriki.
ReplyDeleteKulaumiana na watu wa mabox ama la ni ukosefu wa hoja lakini la msingi ni misupu kuwatafuta kina Bayi na kuwauliza kuna nini kimetokea mpaka hali ikawa hivi?
hapo ndio tutafika!
Kuna mheshimiwa amasema mambo ya afya kweli wabongo wengi UK wana ngoma kwa hiyo ni wazi kabisa wasingefaulu huo mtihani wa afya,kifua kikuu na mambo ya ukimwi wengi sana wanao.Hivyo vya marathon tumwachie John Yuda,mtu amabaye hatombi wala havuti fegi na ulabu.
ReplyDeleteWabeba mabox wanakuwa na miguu iliyokomaa sana na yenye stamina sababu ya kuzidiwa uzito na mabox wanayojitwika.
ReplyDeleteMbeba box kama aweza kimbia na box ukimwambia akimbie bila box ni hatari Michuzi!
Wangeshiriki hata bila mazoezi wangeweza kushinda hata kama wangekosa medali ya Dhahabu wangeambulia hata ya jiwe!
Watu wanakimbia na Mabox usiku kucha kwenye masupermarket na maghala itakuwa na hayo masaa mawili matatu ya kukimbia bila Box kwenye Marathion!
Michuzi acheni dharau