Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Kama wenzake wamegoma kuingia darasani naye agome kwa kutokwenda kununua dawa famasi mpaka kieleweke. by Mropokaji

    ReplyDelete
  2. Agome kurudi nyumbani... mpaka FFU waje kumtoa.

    ReplyDelete
  3. niliposema kuwa hawa wanafunzi wana ufupi wa mawazo kuna watu walidhani nakurupuka na wengine walisema naongea pumba.mwenye muda asome habari hii kuthibitisha nilichokisema.rais wa serikali ya wanafunzi anasema ameshindwa kwenda Dodoma kuonana na waziri mkuu kwa sababu uongozi wa chuo haujampa pesa!hivi kama kweli rais huyo anaamini kuwa alichotaka kufanya ni utatuzi sahihi wa matatizo ya wanafunzi chuoni ameshindwaje kupata mchango wa sh elfu 30(toka kwa wanafunzi) za kwenda Dodoma lakini ana nguvu na uwezo wa kuhamasisha watu kugoma.kwenye habari hii pia kuna maoni ya kiongozi wa serikali iliyopita.nashauri tuisome ili tuelewe vizuri kule taifa letu linakoelekea.zemarcopolo http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/04/21/88867.html

    ReplyDelete
  4. Michuzi chukua 5 hayo ndio mambo mazee kaza buti hatutaki uwe muoga sisi pouwa sana hapo..

    ReplyDelete
  5. we kweli mropokaji,hautumii akili kama wenzako wa chuo kikuu,sasa akigoma kununua dawa anamgomea nani?unadhani kikwete anajali?sanasana atapanga mikakati ya kwenda kupumzika ukerewe kwa ajili ya kuepuka kelele za wananchi.
    MANYUNYU

    ReplyDelete
  6. We Zemakopolo, acha ujinga. Kwa nini wamchangie nauli ili-hali ni wajibu wa chuo kumpatia hiyo nauli?

    Nakushangaa kama unatoa sapoti kwa uongozi wa DARUSHWA ULIOPITA. Huu uliopo ndio uongozi wa DARUSO. Lkn uliopita walikuwa wezi na wala rushwa wakubwa na kwa maana hiyo wanatafuta kujipamba kwa kuropoka. Otherwise una uhusiano nao ktk ubadhirifu.

    ReplyDelete
  7. WEEE ANNON HAPO JUU HEBU ACHA KUMUANDAMA ZERMACOPOLO,WEWE NDO JINGA KABISA,SASA WANASHINDWA KUPATA HIYO TSHS 30,000 YA NAULI TU BASI MADAI YAO HAWAYAPI UZITO.KWANZA HIVYO VITOTO KUTWA VIKO KWENYE VILABU VINAKUNYWA BIA LIKIJA SUALA LA FEES NA FARES NDO VINAONA GHALI.NA WADANGANYIKA WENGI TUKO HIVYO KWA MICHANGO YA HARUSI,NGOMA YA UNYAGO,KITCHEN PARTY N.K PESA TUNATOA,LINAPOFIKA SUALA LA ELIMU TUNAJIDAI MASKINI.WAACHE WA UDSM WATAKOMA KURINGA,J.K BABA UZI NDO HUO HUO LAZIMA WAJUE SERIKALI NI KUBWA KULIKO WAO.

    ReplyDelete
  8. Jamani maoni ambayo yametolewa na lile jinga linalo jiita listaafu la Daruso msiyaweke maana kwanza ni lipuuzi yaani lisomi lisubutu kusema kuwa serikali ililionga kweli mtu mwenye akili timamu anaweza akasema maneno kama haya. Kwanza sijui linasoma nini ningekuwa, Linaonekana ni jilevi lilikuwa nilishinda pale kwenye mgahawa wa DARUSO LINAKUNYWA POMBE kwa kutumia hela za wanafunzi, sasa uongozi wake umeisha linaanza kupayuka na halijui hela ya kununulia pombe litazipata wapi.

    Mimi serikali ya Wanafunzi pale mlimani nilikuwa naifahamu vizuri sana, kipindi chote nilichosoma pale sijawahi kuona viongozi wanakabiziana Madaraka kwa amani. Na yote haya ni kwa sababu kuna hela nyingi sana huwa wanakula

    Nilivyo soma maoni ya lile jilevi nimegundua kuwa kuwa uongozi wa sasa ni mzuri sana na wanajua kupigania haki za wanafunzi na sio kama uongozi uliopita.

    Hii serikali ya Kishikaji (Nguvu Mpya) inabidi iwape wanafunzi mkopo wasome wamalize kama wenyewe walivyosemeshwa, sababu wakimaliza wanarusha na sio kuwa wanapewa bure.

    ReplyDelete
  9. kama hiyo serikali ya wanafunzi ina pesa nyingi ambazo viongozi wake wanatumia kunywea pombe tu kwa nini wasitumie pesa hizo kama nauli ya kwenda Dodoma kuonana na waziri mkuu?zemarcopolo

    ReplyDelete
  10. Agome tu jamani....maana siku hizi fashion ni kugoma tu.Matokea tutajua mbele kwa mbele.

    Ama la kweli kipanya una akili.Maana kugoma kununua dawa ni sawa na kugoma kuingia darasani.

    Watu wangapi wanakufa hospitalini hakuna madawa.Mbona hawagomi hawa wagonjwa kuja hospitalini??

    Wagonjwa gomeni na nyie huduma ya afya iwe 100% free.

    ReplyDelete
  11. Hivi hawa wanafunzi wanaomba mkopo wa kusoma,kununua magari,kununua vitu ambavyo si muhimu na kwa uwezo wao/watanzania wengi hawawezi kununua?????

    Kweli JK fuatilia suala hili,huu mkopo watu wana nia nao tofauti.

    Kama kukopa jamani si hata Bank zinakopesha si mkakope?

    Kusema sirikali inawaaibia wananchi,na hawa waliosemameshwa na sirikali na kisha kubaki nje na wewe si wezi tu??????

    Huu wizi tuangalie ngazi zote.Mwanafunzi unaposomeshwa na serikali kisha ukazamia manchi ya watu huko na kutorudi kulitumikia taifa na kulipa deni na wewe mwezi.

    Kila mtu anaiba anapoweza.Tukitaka tuache wote kuiba.

    ReplyDelete
  12. watu wanataka mkopo hadi dawa ya mswaki.Kwani ukiwa kwenu hampigi mswaki na dawa.Sasa ni kiasi cha kuchangia hiyo 40% maana hata ungekaa kwenu hizo mzazi wako ingemtoka kwa kukulisha,kukupa nauli,dawa ya mswaki,maji unayotumia nyumbani


    Kwa kweli serikali sawa sawa 40% walipe mmewasaidia zaidi ya nusu.Na kwa wasiojiweza kabisa ndio muwasaidie,na kama mnatoa mkopo basi kila mtu apewe hata kama itafikia kila mtu anapata 20%,ila kwa kweli kila mzazi analipa kodi.

    JK na EL hebu tumieni hivyo vichwa kufikiria hili.

    ReplyDelete
  13. Hili suala la kugoma kila mara tena kwa sababu zisizo na mantiki tumechoshwa nalo kabisa. Watu wenye matatizo Tanzania ni wengi tu, sio wanafunzi peke yao. Pesa zinazotolewa za huduma za jamii zinapaswa ziwafaidishe wote, si wanafunzi peke yao. Kwa nini wang'ang'anie 100% sponsorship bila kuwafikiria watanzania wengine wanaohitaji fedha hizohizo? Mbona wagonjwa mahospitalini wanachangia gharama za huduma za afya, wao nani atawasaidia kugoma ili watibiwe bure 100%? Kuna matatizo ya njaa, barabara, nishati, makazi, usalama, n.k, yote yanahitaji fedha. Mbona hawa vijana wanakosa uzalendo? Na hata hivyo serikali ilikwisha waahidi wawe na subira, hatua zinapangwa kuboresha hali iliyopo.

    Kwa maoni yangu, vijana hawa wamekosa hekima na tena hawana adabu. Huwezi kumlazimisha anayekukopesha akukopeshe hela yote unayohitaji. Kopa kiasi kwake, nyingine jazia kutoka kwa mkopeshaji mwingine au kutoka vyanzo vyako vingine vya mapato. Na la zaidi, ni ukosefu wa nidhamu uliokithiri kumpa Rais wa Nchi ultimatum, ati atoe majibu ndani ya siku mbili! Wewe ni nani? Rais wetu yuko kushughulikia matatizo ya wanafunzi tu? Au hilo lilikuwa na dharura gani hadi likashindikana kusubiri?

    Huu ni ulevi wa madaraka ya kitoto, mtu anachaguliwa kuwa rais wa wanafunzi, nafasi ya mwaka 1 tu, basi anajiona naye ni Rais kama Mh Kikwete, anaweza kumtishia hata Rais wa Nchi! Anampa ultimatum! Uchuro kabisa huu! Rais wa wanafunzi ni mwanafunzi, na urais huo unakoma anapokoma uanafunzi. Waelewe hivyo. Waache kuyumbishana wanafunzi kwa kutumia vyeo feki hivyo na kudanganyana ati "solidarity", hakuna solidarity hapo wakati huna cheti! Subiri upate cheti (degree) ndipo utaweza kumsumbua mwajiri wako kwa masharti kwa sababu atakuwa anahitaji utaalam wako. Sasa hivi huna utaalamu wowote unabwabwaja ati "solidarity"! Utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua!

    Nashauri UDSM wachambue vizuri wale waliosababisha fracas hii wapewe adhabu ya kukomesha kabisa. Wakomolewe kabisa hao, wala siwatetei ng'o! Uongozi uwe tu makini wasije wakaumiza wale wasio na hatia.

    Kuhusu haya masharti mapya mie naona safi sana, kwanza wameyataka wenyewe hao wanafunzi. Nasema University ikaze uzi, masharti ndio hayo, naunga mkono kabisa na naomba serikali isimamie hilo. Hakuna jipya hapo, kwani hata wagonjwa hospitalini wanalipia gharama, sembuse hao wazima kabisa! Walipe hizo hela. Kama kweli yupo asiyeweza kulipa, abaki kwanza nyumbani tuone wangapi wanaweza tuendelee nao kwa kipindi hiki, tena itasaidia kupunguza fujo. Hao watakaoshindwa kabisa watafutiwe mpango wa kuwasaidia (mfano kama kampeni za michango mbalimbali n.k) na fedha zikishapatikana ndipo waitwe chuoni. Hata watoto wanaopelekwa kutibiwa India, ni fedha zinachangwa kwanza zikishatosha ndipo wanapelekwa. Tufanye hivyo kwenye elimu pia. Pesa mbele, hakuna huduma inayoweza kupatikana bila fedha.

    Nasema tu poleni sana lakini mmevuna mlichopanda.

    ReplyDelete
  14. Hapa ni ujinga mtupu unaochangiwa... SERIKALI itimize ahadi zake... Hatuhitaji ahadi hewa....mikataba Siri ya Serikali... mhhhh... nani serikali kama si hela ya walipa KODI... waanze kukata hela kwa viongozi wote waliosoma bure... Ebu angalieni Profile ya kila kiongozi kama si wakata nyasi tu toka walikokuwa.. Sasa wanatumia nafasi kula rushwa kwa mikata mibovu... na Kikwete atulie ofisini apange mikakati ya kuipeleka nchi mbele si kusafiri kila siku... sasa aanze kuonja chungu ya kuwa raisi mkimya kwenye masuala muhimu ya kitaifa kama ELIMU... Kilanja wake naye aangalie sifa si kigezo cha utendaji... VIJANA GOMENI TU WOTE HAO WAMESOMA BURE... KWANINI WASIANZE KUCHANGA WAO... ikiwa ni pamoja na mimi.. tuchangie sisi wenye kazi...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...