wadau kunradhi. niko katikati ya kuandika novo ya kiswahili na nimefikia sehemu ambayo inanikwaza. yaani hapo nilipo kuna mama ambaye hajajaaliwa kupata mwana japo kaolewa miaka 23 ilopita. sasa ombi langu kwenu ni kutaka kujua je huyu mama nimwite tasa ama mgumba? chonde chonde wataalamu wa lugha ya kiswahili naomba msaada wenu jamani... yaani nikivuka hapo tu novo imekamilika na huenda mkaiona mitaani hivi punde.
asanteni kwa uelewa na kunradhi kwa usumbufu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Sorry but Kiswahili fasaha is not reachable.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Michuzi!
    Tunasubiri kwa hamu kitabu chako. Mimi si mtaalam wa lugha, lakini kwa ufahamu wangu, mwanammke asiyezaa ni mgumba na kwa mwanaume asiyeweza kurutubisha yai la mwananmke ni tasa. Wataalam wengine huenda wana uchambuzi wa kina juu ya hili.

    ReplyDelete
  3. kulingana na maana ya maneno haya mawili inategemea na jinsi story yenyewe ilivyoanza.iwapo katika story haujaonyesha kithibisho chochote kuwa sababu ya kutokupata mtoto kwa wanandoa hao wawili iko kwa mama huyo basi mgumba ndio litakuwa jina sahihi,iwapo kuna kithibisho cha mama huyo kuwa ndio sababu ya kutokupatikana kwa mtoto basi mgumba au tasa yote ni sahihi.kama lengo ni kuonyesha stigma iliyozunguka wanawake wasio na uwezo wa kuzaa basi neno tasa litavuta hisia zaidi,lakini iwapo litatokea kwenye hadithi kama vile linatumiwa na wanajamii sio na wewe mwandishi.mgumba ni more polite than tasa.zemarcopolo

    ReplyDelete
  4. Huyo sio tasa wala sio mgumba tu, hadi hapo daktari atakavyothibitisha. Yawezekana mume ndo tatizo

    ReplyDelete
  5. Japo sina hakika sana lakini nadhani mwanamke huwa TASA na mwanaume huwa MGUMBA.Hata hivyo, gender si muhimu sana katika nomino za kiswahili.

    ReplyDelete
  6. Michu,
    nadhani tumia neno "mgumba", ndio linatoa lugha ya kiungwana (tasfida )kuliko neno tasa ambalo ni kali sana (tabaini)

    ReplyDelete
  7. Sema "ambaye hajafanikiwa/ hawajafanikiwa kupata mtoto kwa miaka 23" au toka waoane maana hakuna utafiti uliofanyika kuonyesha kama ni mgumba au tasa, inawezekana mumewe ndio mwenye tatizo.

    ReplyDelete
  8. Michu hapo hujafafanua vizuri, kama kaolewa miaka 23 na mumewe ni huyo huyo itabidi mumewe akapime kama anauwezo wa kuzaa nae, kama ni mume yupo fiti huyo mama akapime nae kama hana uwezo wa kuzaa basi ni TASA, ila kama mumewe ndio hawezi kutoa mbegu zenye rutuba basi mama huyu atakuwa MGUMBA yaani hajaaliwa mtoto ila akipata mtu stahili atapata mtoto. Sasa cheki novo yake imezungumzia hayo?

    ReplyDelete
  9. Mgumba,tasa huitwa mwanaume

    ReplyDelete
  10. Mr Michuzi,
    we are supportive in whatever you do. TASA NI MWANAUME, NA MGUMBA NI MWANAMKE.

    ReplyDelete
  11. Anaitwa mjane

    ReplyDelete
  12. anaitwa MJANE

    ReplyDelete
  13. Sir.. Issa vipi kaka..naona leo umemwaga lugha tupu..itawachanganya wengi..UNAONGELEA NDOA ANU TENDO LANDOA KAKA...ADO..ADO..

    ReplyDelete
  14. Hello Issa,

    nenda pale kwenye swahili sio kwenye makabila kwenye url hii http://www.websters-online-dictionary.org/translation/swahili/mgumba

    ReplyDelete
  15. Mimi nafikiri utumie Mgumba maana hili jina lenye hali ya ubinadamu (utu).Sasa Tasa ni neno lililokuwa likitumika sana hapo nyuma mpaka sasa,lakini katika kiswahili fasaha hili jina linafaa kuitwa vifaa na viumbe hai wengine lakini si binadamu.Kila binadamu anatambulika kwa kuanzia M...yaani mgumba,mlemavu,mjane,mbahili na mengineyo.
    Sasa hilo Tasa labda samaki au ng'ombe asiyezaa.aahah ahah.Kwenye kiswahili fasaha,tunalipiga vita sana kama neno Kiwete,Kilema na Kipofu.Tunasema mlemavu, asiyeona na mengine mengi yenye kubeba hadgi ya utu.
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  16. Kwa uelewa wangu wa Kiswahili ni kwamba kama mwanamke hana uwezo wa kuzaa wa kurutubisha yao na imethibitishwa na daktari basi huyo ni TASA, na kama tatizo nimwanaume basi huyo mwanamke hana jina rasmi anaweza kuitwa hajaaliwa kupata kupata mtoto. Kwa sababu NGUMBA linatumika kwa mwanaume ambaye mbegu zake hazina uwezo wa kurutubusha yai (Barren man).

    Zumba's

    ReplyDelete
  17. Hi Michu.....
    nafikiri haujatoa kielelezo je huyo mume wa huyo mama anawatoto kwa mtu mwingine au laaa.. maana unaweza kusema huyo mama ni Tasa au Mgumba kumbe mume ndio anamatatizo kwahiyo ni muhimu sana kuwa na maelezo ya kujitosheleza kabla ya kumtafutia huyo mama jina......

    br Kunta

    ReplyDelete
  18. Kama walivyosema hapo juu wengi tu. Tasa na mgumba vinatofautina sana. Kama Mume ana watoto wengine na wamepimwa ikaonekana mwanamke ni yeye ndio ana matatizo ya kuzaa basi ni tasa lakini hawajapima mwanaume hana watoto mahali pengine basi inawezekana ni mgumba tu huyo....Mgumba anaweza kuzaa kwa fujo tu na mtu mwingine hata mapacha wakatoka hapo.

    Sasa jina la kumwita ni jinsi novel yako inavyoelezea

    ReplyDelete
  19. JAMANI SIO wodow au widower,,,,,,kck

    ReplyDelete
  20. Kwa jinsi ulivyoweka mada yako. Si neno TASA, wala MGUMBA. Unaweza kujikuta unamdhalilisha mwanamke, nakutahadharisha. Ili uwe 'safe', toa mazingira ya kutopata mtoto au watoto kwa wazazi hao. Kama tuishio ugenini huku, watu tangu waoane miaka zaidi ya hiyo 23 hawajazaa watoto, si kwasababu hawawezi kuzaa, bali waliamua tu. Na baadhi yao wanarithi au ku-adapt watoto wa wengine. Wakati baadhi tena hukaa bila mtoto hata mmoja ili wasipate shida ya kufikiria mambo ya kuhudumia watoto na mashinikizo mengine.
    Sasa wewe ili kitabu chako kisilete utata, toa mazingira ya hawa wazazi kukosa watoto ni kwanini. Baada ya hapo, chagua neno linalokufaa kwa namna walivyokushauri wadau hapo juu. Ila uwe makini, maana baadhi hapo juu wanasema umwite mjane. Mjane ni mke aliyefiwa mme.
    Najua ni kwanini hukufikiria yote haya, sababu Bongo hamna sheria wala vigezo vingi vya kuangalia ili usijikute unamdhalilisha mwanamke.
    HOPE YOU GOT ME,
    IN THE STATES,
    Mlalahoi.

    ReplyDelete
  21. Mzee michu, kuna watu hawako sirias hata kidogo. minaona "Mgumba" imekaa kistaarabu zaidi.tasa inatumika kwa wanyama unajua. all the best

    ReplyDelete
  22. Even with all these comments still those vocabs are not reachable.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...