miss tz wa kwanza theresa shayo alipochukua taji hilo mwaka 1967. mashindano hayo yalipigwa stop mwaka huo huo na kuibuka tena mwaka 1994 na kuendelea hadi hii leo. hivi tunavyozungumza kuna warembo 25 kambini hoteli ya kunduchi ambao watashiriki kwenye mashindano ya kwanza ya miss universe siku ya jumamosi hoteli ya movenpiki ambapo mshindi ataiwakilisha bongo kwenye fainali za dunia huko mexico baadaye mwaka huu. miss universe ni jibu la marekani dhidi ya miss world yenye mizizi yake uingereza. wadau wa fani hii wanasema sasa bongo imefunua ukurasa mpya kwa kuwa na michuano miwili mikubwa ya ulimbwende. wadau mnasemaje kwa hilo???

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Asante kwa picha Michuzi. ni mrembo kwa kweli tena yupo natural. naomba utuletee picha yake ya sasa.

    ReplyDelete
  2. Michuzi mara ya mwisho ulipoweka picha ya huyu mama kuna baadhi ya wanaharamu walimtukana matusi ya nguoni japo hawamjui nina uhakika uliona na leo nashangaa imerudi tena, hayaa...

    ReplyDelete
  3. Naomba more updates, mdogo wangu anashiriki humo. kama kuna link ntashukuru au keep us inform si unajua tuko mbali

    ReplyDelete
  4. she is of my mum's age or less a bit if she won at age 20 or less,i need to see her recently look she was amazing with no make ups at all plus natural hair.

    ReplyDelete
  5. Michuzi hii picha umeiludia kuiweka nafikili hii mara ya saba sasa. Tafadhali naomba utuweke picha nyingine mpya this is now boring.

    ReplyDelete
  6. Sir Issa huyu Dada mambo yake natural, anavuutia kaka, aksante.

    ReplyDelete
  7. Michuzi mbona nilisoma kwenye gazeti moja hapa nchini sikumbuki ni gazeti gani siku za nyuma likisema huyu dada amefariki dunia huko ujerumani alikokuwa anaishi na mumewe, je ni habari hizi ni za kweli au uzushi? Na kama ni kweli kwa nini usiandike marehemu au hayati kama anastahili kuitwa hivyo kuliko unavyomwandika hivi as if yuko hai? Naomba utusaidie kuja ukweli wa dada au mama yetu huyu mlimbwende wa zamani .Thanx

    ReplyDelete
  8. Akina mama na baba wa umri wa huyo mama siku hizi wanajidai eti watoto wa siku hizi wameharibika wanavaa nusu uchi na hao je wa miaka ya 60? Wa umri wenu?

    Vizee fix kweli vya siku hizi nimevigundua ni viongo.Vinajifanya enzi hizo sisi tulikuwa sio kama ninyi.Uongo mtupu.

    Hongera michuzi kutupa picha ya miaka hiyo.Mamaangu nimemwonyesha.Kanywea kimya.Hanibwatukii tena.Alikuwa analeta za kuleta nikamwonyesha hiyo picha akanywea.

    ReplyDelete
  9. We anon wa april 12 kuwa na heshima kwa mama yako. Huyo hapo aligombea u miss na kati ya masharti ni kuonyesha uzuri wa miguu. Haina maana wamama wote walivaa hivyo wakati huo hii ni special moment. Mbona hiyo nguo sio fupi sana halafu huoni kwamba huyo mama ni very natural? Ona anavyo tembea kwa heshima yaani hapanui miguu ili kuhifadhi heshima sema tu wewe jeuri hutaki msikiliza mama yako shauri yako, mtoto akililia wembe mwache umkate.
    Kumbuka kuna UKIMWI!
    Waridi

    ReplyDelete
  10. We msemaji hapo juu kwanza huna adabu,pili inaelekea umekaa ulaya siku nyingi, na kuigaiga vitu vya kijinga, iga vitu vya maana,naomba kukujulisha ya kwamba nguo fupi ziko toka enzi na enzi, lakini ina tegemea unazivaa wapi, kwenye shoo, kama huyo dada, disco, au ufukweni mwa bahari,kama umezowea kuvaa tunguo tufupi na tuvitop mbele ya baba yako basi acha,maana kama ndio una mfiga ndugu yangu, baba yako uzalendo unamshinda,siku moja utamkuta yuko (TOP ON YOU)kwa hiyo bi mdogo vaa tuvitop twako kama upo sehemu muafaka na watu muafaka,kila mwanamke anavaa kanga moja na bila ya chupi, ni wakati gani na yuko na nani, akili kichwani mwako. Dumisha utamaduni,mila na desturi ya muafrika mwanangu eeeeeee!!!!.

    ReplyDelete
  11. Michuzi, si vibaya ukiweka habari kuhusu, "WHERE SHE IS NOW". Na picha. Of course by now ni Senior Citizen. Kama unaweza kum-contact umhoji kuhusu Ma Miss Tanzania Pageants wa siku hizi. Kweli tungependa kujua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...