wekundu wa msimbazi wangemtafuta mnyama kama huyu wamweke pale klabuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Pamoja na watani wetu kutufanyia "hujuma" kocha wetu kuondoka, kunyang'anywa ponti lakini jana bado tumefanya makubwa. Soma Mwanaspoti ya leo!

    ReplyDelete
  2. Huyo wa bei ghali sana, akina Kaduguda na Dalali hawawezi kumnunua. Labda we mnazi wao unaweza kujitolea, kisha ukasema kuwa hutalipia ada ya uanachama ya miaka miwili. Waionaje hiyo Misupu!!!

    ReplyDelete
  3. Michuzi umeona simba walivyoharibiwa na watalii huko kwa Da Chemi? http://swahilitime.blogspot.com/

    ReplyDelete
  4. Duh! Mzee Umependeza!Lakini mbona sikuoni kwangu!

    ReplyDelete
  5. YAANI WEWE MICHUZI NA MOURINHO MNATOFAUTIANA RANGI TU..KAZI KUROPOKAROPOKEA YA WENZENU YENU YANAWASHINDA.WEWE SIKU ZOTE CHUKI NA SIMBA LEO IMEKUWAJE UMEWAONEA HURUMA HIVYO.KISA KWA KUWA SIMBA LAZIMA WAMUWEKE HUYO SIMBA.!!AU UNATAKA AWEKWE LEO KESHO WATU WA YANGA MUMUNG'OE?YANGA MTAWEKA NINI!KWANZA NAKUSIKILIZIA SANA LEO SIJUI LEO UTAONGEA NINI KUHUSU MANCHESTER SIJUI WAMEBAHATISHA TENA AU WAMEPENDELEWA KAMA KAWAIDA YAKO.NA UKUMBUKE JUMANNE SIO MBALI HIYO HASIRA YA BOLTON INAAMIA KWENU.

    ReplyDelete
  6. Kaka hizo nondo zako si mchezo!

    ReplyDelete
  7. vipi misupu,bwawa la maini naona linayoyoma au nyie ndio wasindikizaji, au bado mnaota doto ya chealse

    ReplyDelete
  8. Swali kwa michuzi, wewe kama mpiga picha (photo journalist) inakuaje picha nyingi hivo ni wewe au wewe ni modo? Badala ya kupiga picha wewe ndio unapigwa picha?

    ReplyDelete
  9. Misupu tafadhali tuwekee ule mkwara wa serikali kwa vyombo vya habari tuujadili.

    ReplyDelete
  10. MHESHIMIWA MICHUZI, WATU WANAIBIWA BONGO HIVIHIVI. NAOMBA TULIJADILI HILI: KWANINI WABONGO WANAIBIWA KIRAHISI HIVI? NA HATA WASOMI WETU WA CHUO KIKUU AMBAO TUNAWATARAJIA NDIO WAONGOZE JAMII INAKUWAJE NAO WANAINGIA KWENYE MTEGO WA KIJINGA HIVI? JE HAO WANAOFUNGUA OFISI NA KUKUSANYA PESA KUTOKA KWA WATU INAKUWAJE WANARUHUSIWA KANA KWAMBA NYUMBA(TANZANIA) HAKUNA WENYEWE?

    INAKUWAJE MGENI ANAKUJA ANAFUNGUA DUKA NA ANANZA KUIBIA WATU TUNAMKODOEA MACHO TU?

    Upatu: Dar waibiwa

    2007-04-25 17:37:55
    Na Mwandishi Wetu, Jijini


    Ule mchezo maarufu wa kupeana pesa kwa staili ya mzunguko almaarufu kama upatu, umerejea Jijini Dar es Salaam kwa kishindo na tayari Wabongo kibao wameripotiwa kulizwa fedha zao.

    Taarifa zinadai hadi sasa, mamia ya watu wamelizwa baada ya kudunduliza senti zao kwenye vibubu na kuzipeleka kwenye upatu huo unaodaiwa kuendeshwa na kampuni moja ya Wakenya kwa matarajio ya kuzoa mamilioni.

    Na cha kusikitisha zaidi, chanzo kinadai, miongoni mwa wengi waliopigwa changa la macho ni wasomi wa vyuo vikuu, baadhi wakiwa ni miongoni mwa wale waliosimamaishwa sasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kugomea asilimia arobaini ya ada na gharama za `ield`.

    Tarifa zinadai wapo wanafunzi kibao wa vyuo vikuu Jijini waliojinyima pesa za kujikimu walizopewa na Bodi ya Mikopo na kuzipeleka kwenye upatu huo ili wazoe mamilioni, lakini hadi sasa hakijaeleweka.

    ReplyDelete
  11. Michizi naona nondo unazo hapo Hiyo Canon EOS babu kubwa....

    ReplyDelete
  12. kaka michuzi kuna hawa wabongo wawali wenye hizi blog mbili moja ni mikundu.blogspot.com na videozamatusi.blogspot.com naomba uanzishe mjadala tuwadiscuss maana wanatutia aibu vitu gani vya kijinga vya kudiscuss tunataka watu wenye kufanya mambo ya maana kama wewe sio hawa wanatuwekea ujinga,pliz ikiwezekana tuwasake na tubandike mipicha yao hapa.

    ReplyDelete
  13. Michuuuuuuu!!!!!!Simba wa Ikulu huyoooooo

    ReplyDelete
  14. michuzi hawa wabongo wa blog za matusi tuwavalie njuga bwana

    ReplyDelete
  15. Issa umependeza lakini angalia huyo simba asikumalize bado tunakuhitaji.

    Iam back! waridi

    ReplyDelete
  16. kesi ya ngedere unampelekea nyani, bofya HAPA USOME MAONI

    ReplyDelete
  17. Duh michuzi kaka huzeeki wewe! mzee nilianza kukusikia tokea mdogo nasoma shule ya msingi na mpaka sasa nimeshamaliza chuo kikuu, lakini unaonekana sawa na kijana anaenza maisha sasa hivi. Je unaweza kutuambia siri ya ujana wako? Hongera sana.

    ReplyDelete
  18. Sir Issa..vipi mzee naona UME MECHISHA....ANGALIA ANAUMA HUYO....PICHA KAMA HIZI AGHALABU..

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 02, 2007

    michu kumbe zinga la hb(handsome boy)wewe.naona naanza kukupenda sasa itakuwaje nieleze tafadhali si lali juu yako mawazo kibao mpenzi.

    ReplyDelete
  20. Anon May 02 usijifunge mwendee daily news uso kwa uso, face to face, lakini ndoo ujue kufunga kibwebwe maana atakufa mtu.

    Candidates kibao lol!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...