waziri wa viwanda, biashara na masoko mh. basil mramba akiwabrifu paparazi juu ya ujio wa shaikh saud bin saqr al qasimi ambaye ni naibu mtawala wa ras al khaiman ambayo ni mojawapo ya nchi saba zinazounda imarati. mgeni huyu atatembelea sehemu mbalimbali ambazo nchi yake imeonesha nia ya kuwekeza ikiwa ni pamoja na fukwe za dar pamoja na daraja la kigamboni. atatembelea zenj na kwenda kuangalia wanyama huko grumet

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Serikali pado tu kuuza watu wake......ambayo iko matayarishoni. Sasa hivi uatasikia .

    ReplyDelete
  2. Michuzi umekosea maelezo ya picha (caption). Maelezo sahihi ni kuwa: Chifu Mangungo wa Msowero akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa Waarabu kutoka Imarati kwa ajili ya mazungumzo ya mauzo ya fukwe za Bahari ya Hindi eneo la Dar pamoja na kila chenye thamani ambacho Waarabu hao watapenda kuvinunua kwa bei ya chee. Buriani Watanzania, tuuzwe kwa amani, na tulazwe mahali pabaya umaskinini. Amen!!

    ReplyDelete
  3. Kama kuna DALALI NAMBARI wani serikalini basi atakuwa ni huyu Mramba.

    huyu mtu hafai, alitaka kuiza hivi hivi Eapoti ya Mwanza. kwa kigezo cha kuiokodisha lakini kumbe mpango ndio ulikuwa wa kuisukum jumla jumla.

    ReplyDelete
  4. Labda alimalizia kwa kusema `Sheik usiogope Watanzania heri wale nyasi kuliko kuona daraja la Kigamboni halijengwi au wewe unakosa fukwe za kupumzisha familia yako tukufu`.

    ReplyDelete
  5. Wziri Mramba alisema week chache zilizopita kwamba nyaya mbovu zilizo chini ya kiwango ndizo zinaunguza nyumba dar(sio miujiza!!!)na wananchi wajihadhari nazo. Je, amefanya juhudi gani kuhakikisha HAZIENDELEI kuingizwa nchini? Je, amefanya juhudi gani kukamata wanaoingiza nyaya mbovu na kuwauliza wanaouza rejareja zilikotoka?. Mramba, Mtanzania wa kawaida anajisikia halindwi, anaona hakuna mamlaka nchini, kwasababu anaona bidhaa mbovu(nyaya, n.k)zinatamba na anaunguliwa na nyumba!!. Mwananchi wa kawaida anakuuliza mbona humlindi?

    ReplyDelete
  6. MHESHIMIWA rais;

    Leo naendelea na wajibu wangu kwako na nchi yangu, nikiwa katika hali ya kuchanganyikiwa. Yananichanganya mengi, lakini niruhusu leo nichepuke kidogo nje ya hotuba yako ya Desemba 30, 2005 nizungumzie japo kwa ufupi mawili yaliyojiri hivi karibuni.


    Kama kuna kikwazo kikubwa kwa taifa letu, basi haya mawili ni sehemu muhimu isiyohitaji kufumbiwa macho kwa njia yoyote. Naam, mambo haya ni uhuru na wajibu wa Bunge na hatma ya elimu ya juu nchini mwetu.


    Namwomba Mwenyezi Mungu aendelee kuniwezesha kuwa mtii kwa nchi yangu. Anipe ujasiri wa kuheshimu viongozi wanaojali watu wao. Kama sehemu ya utii huu, kila siku nikijadili jambo linalohusu taifa letu, kila inapobidi, sitaacha kukukumbusha ulichokisema. Taifa hili likifanya masihara, likabweteka na kughilibiwa na kauli zako zisizotafsiriwa kwa matendo, hakika litageuka taifa la “kondoo” ambalo nalikataa kwa unyonge wangu wote! Sitazua! Nitajadili ulichosema! Ndiyo msingi na nguzo ya tafakuri zangu.


    Nitakusaidia kwa kukumbusha kila kauli uliyoitoa, bila kuchoka hadi hapo utakapoamua kunifunga mdomo; ama kwa mamlaka yako ama kwa kutekeleza kauli zako kwa vitendo.

    Mheshimiwa rais;

    Wakati unafungua jengo jipya la Bunge kule Dodoma, Juni 12, 2006, kama kawaida yako ulitoa hotuba yenye sura mbili. Sura ya kwanza, ilikuwa ni hotuba iliyoonekana kujaa nia njema na kutoa matumaini kuwa serikali yako itaheshimu uhuru na nafasi ya Bunge katika kujenga taifa letu.


    Sura ya pili, inayojengeka kutokana na ushahidi wa kimazingira, inahoji ni nini kinasababisha kauli zako zisishabihiane na nia unayojaribu kuijenga kwetu wananchi wako.


    Hapa chini nanukuu sentensi chache kwenye hotuba yako.


    “Mheshimiwa Spika; Ukumbi huu utawawezesha waheshimiwa wabunge wetu kupata huduma bora na hivyo kufanya shughuli za uwakilishi kwa ufanisi wa kiwango cha juu. Ni ukumbi wenye hadhi ya kimataifa unaowapa wabunge vionjo vya Bunge katika karne ya 21.


    “… Sina shaka akilini mwangu kuwa, kwa hakika jengo hili litabadilisha namna tunavyofanya kazi ikiwa ni pamoja na mienendo na mitazamo yetu kuhusu vikao na maamuzi ya Bunge.


    “… Bila ya shaka kwa kuutumia kwa ukamilifu ukumbi huu wa Bunge… sauti za Watanzania zitasikika bila mikwaruzo. Aidha, matakwa na matarajio yao yatawasilishwa, kujadiliwa, kufanyiwa kazi na kupatiwa majibu kwa ufanisi zaidi sasa.


    “Mheshimiwa Spika; Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Bunge, kama mhimili huru wa utawala wa nchi yetu. …Nawaahidi ushirikiano wangu binafsi na wa wenzangu wote serikalini.”

    Mheshimiwa rais;

    Hilo ni wakati huo. Lipo hili la majuzi. Wakati ukiwahutubia wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali siku ya Februari 3 katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Ulisema maneno yafuatayo:


    “Tupeni muda suala hili tunalishughulikia haraka na kwa muda mfupi mtapewa majibu, lengo ni wale wote waliofaulu waweze kujiunga na masomo na si kuacha kwa vile wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia ada.” Mwisho wa kunukuu.

    Mheshimiwa rais;

    Si siri, serikali yako inadharau Bunge. Serikali yako inadhalilisha Bunge. Serikali yako, inatumia kila mbinu kulificha Bunge ukweli wa ufisadi ndani ya serikali yako na zile zilizokutangulia. Wasaidizi wako - nina hakika kwa baraka zako - wanawafunga wabunge midomo. Wanazuia mijadala.


    Kama mnaamini Watanzania watasahau, mnajidanganya. Tunazidi kukusanya takwimu na muda unavyokwenda bila majibu, ndivyo mshindo utakavyokuwa mkuu. Kwa mema yote mnayoyafanya tunawapongeza, lakini hayatatufunga midomo kusema na kuhoji mpaka kieleweke!


    Ahadi yako kuwa jengo jipya litabadilisha utendaji wa Bunge ni dhahiri kuwa haikuwa ahadi ya kweli. Kwa kuzingatia mengi mnayowazuia wabunge kujadili, ni dhahiri ahadi yako kuwa, utawasaidia wabunge kutekeleza wajibu wao kwa kulifanya Bunge kuwa huru, haikuwa ya kweli.

    Mheshimiwa rais;

    Kero kubwa za wananchi bado zinaendelea kuwa siri ndani ya serikali yako. Waziri mkuu wako anaendelea kwa kasi kulidhibiti Bunge na kukingia kifua ubadhirifu ndani ya serikali yako. Unayaona, unayajua, unakaa kimya, unayabariki. Ni wewe unayemtuma? Kwa nini tusiamini wewe ni sehemu ya ufisadi huu?


    Chuo kikuu leo kimefungwa. Ahadi zako hazijatekelezwa. Hakuna maelezo yeyote ya mtu mwingine yeyote yataeleweka. Tunasubiri kauli yako. Pengine fikra zako umeelekeza kwenye chuo kipya Dodoma! Cha nini kama kilichopo tumeshindwa kukiendesha?


    Wanafunzi leo wamefukuzwa chuoni! Nani kasema kufukuza kila kukicha ndiyo ufumbuzi wa elimu ya juu nchini? Haya ni majibu ya sera mbovu za elimu ya juu. Ninyi mtumbue, mfuje matrilioni halafu mfukuze maelfu ya watoto masikini. Nikisema rais alidanganya watoto masikini na wazazi wao nitakosea?


    Bado mnacheza na elimu ya juu. Serikali yako ni serikali ya anasa. Naam, ni serikali ombaomba. Mnaomba, mkipata mnatumia bila kuheshimu bajeti. Kila siku makusanyo ya kodi yanavyoongezeka, ndivyo matumizi ya uendeshaji serikali yanavyoongezeka.


    Taifa linakusubiri utoe kauli inayoeleweka kuhusu shilingi trilioni moja (bilioni 978) ambazo serikali yako imezifuja nje ya bajeti bila maelezo ya kutosha na bila yeyote kuchukuliwa hatua.

    Mheshimiwa rais;

    Kwani nani kawaambia wewe na mtandao wako mmemilikishwa nchi hii muichezee, muitumie na muiongoze mnavyojisikia? Nini maana ya wabunge kushinda miezi kadhaa bungeni wakitumia mabilioni ya fedha kujadili na kupitisha bajeti, kisha ninyi mtumie bila kujali?


    Sawa sheria ya rushwa imepitishwa. Ofisi yako (Ikulu) imeng’ang’ania usimamizi wake. Pamoja na kilio na hofu ya wadau, yaani wananchi, kwamba Ikulu ni kinara wa rushwa, hivyo asisimamie TAKURU, mmegoma. Nina hakika mmejadili na kuweka msimamo. Nia njema iko wapi? Unaogopa nini wewe na wenzio kama mko safi?


    Wewe kama rais, umetoa kauli nyingi tangu uchukue dhamana ya kuliongoza taifa letu. Kauli zako hizi, ulizozitoa maeneo mbalimbali na katika mazingira mbalimbali, kwetu wananchi wako zinawakilisha ahadi yako kwetu.


    Ni wajibu wetu kuzihuisha na hotuba yako ya kufungua Bunge. Ya ufunguzi ilikuwa dira yako kwa taifa na zinazofuatia zote, tunazitegemea si zitoe ahadi na dira tena, bali zijikite kwenye utekelezaji wa dira yako ya Dodoma ambayo kwetu ni ahadi.

    Mheshimiwa rais;

    Woga wangu ni kuwa, taifa hili linaanza kuamini kauli za rais ni usanii. Ni uzushi. Ni danganya toto. Ni funika kombe mwanaharamu apite. Ni ubabaishaji. Rais anazungumza asichoelewa, asichokijua, asichoamini!


    Kama sivyo, basi ni kuwa rais wetu ni dhaifu; na wasaidizi wake wanamwona hivyo. Na wao ni dhaifu, pengine zaidi. Ni kwamba rais ana ubia na watu katika utawala wake, na hana kauli ya mwisho.


    Sifa zote hizi si sifa nzuri. Sisi watiifu kwa nchi yetu na kwako tunakueleza, kwani tunajua hao unaojaribu kuwakingia kifua ndio hao hao wanaotumia fursa hiyo kuonyesha udhaifu wako. Nchi hii haijapata kupata kiongozi wa sifa mbaya kama hizi.


    Kiongozi mwongo, asiyeaminika hakika ni sifa mbaya isiyo na kifani. Ukimya wako si ushindi, ni uthibitisho wa hofu hiyo. Kataa sifa hiyo. Mtandao wako hauwezi kukusaidia kwenye hili. Onyesha kwa vitendo kuwa kweli huna ubia na wanamtandao, bali una ubia na wananchi wako.

    Mheshimiwa rais;

    Yako mengi yanafukuta. Kumbuka hakuna siri ya watu wawili. Punde yatawekwa hadharani. Watanzania wanajua Richmond tu! Mbona Richmond ni cha mtoto! Yako mengi, mazito! Kama huyajui, tutakusaidia kuyajua.

    Kupenda sana kusema maneno ya kufurahisha watu wako hata kama hukusudii kuyatekeleza, kutakuponza na kukuvunjia heshima. Kutaliangamiza taifa letu.


    Nakushukuru kwa kunisoma. Wiki ijayo nitaendeleza utii huu kwa kurejea hotuba yako ya dira yako kwa taifa!


    Mheshimiwa rais;

    Naomba kutoa hoja

    freeman@chadema.net

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...