ni mwaka 1975 wakati nahodha wa simba sc haidari abeid muchcaho alipopokea kombe la ubingwa wa soka kwa nchi za afrika mashariki toka kwa mh. joseph mungai

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Asante sana Michuzi,
    Hii picha naikumbuka, kaka yangu aliikata na kuiweka kwenye albamu yake. Nazikumbuka pia enzi za Haidari namba 8 na Aluu Ally namba 6. Ah! Simba tulikuwa "Taifa Kubwa" kweli!

    ReplyDelete
  2. Duh mjengwa UMECHEMKA nini,sidhani kama Haidar kacheza na Aluu Ally,navyokumbuka mimi enzi ya Haidar Abeid Muchacho namba sita alikuwa Khalid Abeid na hao wote waarabu wa Shinyanga mjini,nakumbuka hoteli ya akina Haidar ilikuwa ikiitwa ZAmzam Hotel pale Shinyanga.Na wakati Haidar anacheza Aluu alikuwa kinda bado,kwani alitokea Mseto ya mjini kasoro bahari wakati huo kipindi Muchacho yupo umangani.Michu hebu nikumbushe kama niko right bruv.

    ReplyDelete
  3. Aaaaah naona kwa chini vikombe vidogo vingi, naona kwa ajili ya kila mchezaji na viongozi kweli zamani tulikuwa mbali. Hivi siku hizi zipo hizi kweli!??Au ndio Ndolanga alikuwa anapeleka nyumbani kwake akapandie maua. Katurostisha kweli yule fala, tungekuwa mbali kinoma kama Tenga angekuja enzi zake!!

    ReplyDelete
  4. Mi mnanichanganya. Hivi kuna tofauti gani kati ya Aloo Ally na Aloo Mwitu??

    ReplyDelete
  5. michuzi, naomba ucheki kumbukumbu zako tena hapo. mi nakumbuka hii ilikuwa ni mwaka 1974 ambapo simba ilitwaa kombe hilo ambalo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kushindaniwa. Simba iliwakilisha kutokana na kutwaa ubingwa mwaka wa Tz mwaka 1973. Kisha mwaka 1975 ndipo yanga ikawakilisha kutokana na kutwaa ubingwa wa Tz mwaka 1974 pale Nyamagana.

    huko Zbar Yanga ikafaulu kutwaa ubingwa wa E&CAkwa kuifunga Simba bao 2-0 na Sunday Manara na Sembuli ambao pia ndio waliifunga Simba pale Nyamagana miezi kama mitano kabla.....!

    ReplyDelete
  6. annoy wa 2:43, kwa kumbukumbu zangu hawa ni wachezaji wawili tofauti. Aloo Mwitu alikuwa back four wa Simba na alijiunga nayo kama sikosei mwaka 1973 kutoka Lake Star ya Kigoma timu ambayo ilikuwa imeingia fainali ya klabu bingwa ya Tz mwaka huo na kufungwa na Simba.
    huyu Aluu Ally kama sikosei alitokea Mseto na alijiunga na simba mwaka 1976.....

    ReplyDelete
  7. Anony 2:43.00PM tofauti kati ya Aloo Ally na Aloo Mwitu ni kama Ben Kisaka na Ben Mkapa!!Una swali lingine?

    ReplyDelete
  8. usichanganyikiwe ndugu yangu Alluu Ally katokea mseto Morogoro na Aloo Mwitu katokea Kigoma

    ReplyDelete
  9. Usichanganyikiwe Aluu Ally katokea Mseto Morogoro na Aloo Mwitu Kigoma

    ReplyDelete
  10. Kwa ufafanuzi zaidi wote walikuwa wachezaji wa Simba,Aloo Mwitu alikuwa anacheza beki namba 4 na alijiunga na Simba akitokea Kigoma pamoja na Khamis Askari.Huyu Aluu Mohamed Alli"Spoiler" alikuwa midfielder mahiri wa kikosi cha Msimbazi,yeye alitokea Mseto FC ya Morogoro alicheza Simba then akakimbilia umangani.Alikuwa bonge la midfield kwa sasa unaweza kumcompare na Steven Gerrard only kwa maana midfield anayefunga magoli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...