wachezaji wa yanga wakienda kupanda boti kuelekea zenj kwenye michuano ya klabu bingwa bongo januari 3, 1975 walipokuwa mabingwa wa bara. mie namkumbuka kipa muhidin (mbele) na mzee mangara tabu (mwenye baraghashia akiongea na gibson sembuli). wadau kazi kwenu..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. mtu zilikuwa zimeshiba kisawa sawa!

    ReplyDelete
  2. Micuzi naoma nikuweke sawa hapo ni uwanja wa ndege wa zamani wa Dar na sio pahala pa kupandia boti.Boti zilianza kwenda Zanzibar mwanzoni mwa mwaka 1990 na boti ya kwanza ikiwa Virgin Butterfly.
    Halafu mwaka 1975 kwenda Zaznibar hakukua na boti ila Meli nazo ni MV Jamhuri,MV Afrika na baadae ikaletwa meli kubwa MV Mapinduzi.

    ReplyDelete
  3. Vipande! Sijui vilikuwa vimeridhika nini? Hebu vingunge tupeni siri! Wengine tulikuwa hatujazaliwa. Namuona Mayaula Mayoni kwa mbaaali!

    ReplyDelete
  4. Huyo mwenye miwani meusi ni Omar Kapera

    ReplyDelete
  5. ...huyo mwenye fulana ya mistari mistari kushooto kabisa ni nyanda Patrick Nyaga, nyuma ya mwenye mawani kushoto ni Juma Matokeo na kulia aliyezibwa kidogo ni Muhaji Mukhi,hapo katikati huyo mfupi ni winga Ahmad Omar na nyuma yake yupo Jellah Mtagwa. annoy aliyesema anamuona mayaula mayoni atakuwa amekosea. Kwenye kikosi cha Yanga kilichochukua ubingwa wa E&CA mwaka 1975 huko Zbar Mayaula alikuwa hayupo kwani aliishaondoka Yanga mwaka mmoja kabla ya hapo....

    ReplyDelete
  6. michuzi enzi hizo watu walikuwa wanapanda ndege za forker(F28)EAA tarehe umeipatia kwa sababu januari 13-1975 ilikuwa fainali ya kombe hilo yanga wakaifunga simba ambao walikuwa wanatetea ubingwa huo wa E&CA club championship. simba walinyang'anywa ubingwa wa bara kule nyamagana stadium august 10-1974. yanga walikuwa wamechoka walipata msaada sana siku hiyo kupitia marefa manyoto ndimbo na zuberi, ramadhan kaabuka alikuwa neutral,wachezaji walikuwa wazee, baada ya hapo wakapata wachezaji wapya kama vile jella mtagwa,leodgar tenga,juma shabani,juma matokeo,patrick nyaga,muhaji muki, ahmad omar timu nzima ilibadilshwa au sivyo hawaifungi simba mara mbili. kinachofurahisha timu mbili toka bara zilikuwa fainali siku hiyo that says alot for the state of soccer in TZ at that time.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...