mwenyekiti wa kamati za harusi za deiliniuzi francis mushi akieleza kwamba kamati ya maandalizi inampatia chabi barasa na mkewe viki dola 800 wakanunue wenyewe zawadi waitakayo. wadau kunradhi siku mbili hizi mtandao wozi noti richebo ndo maana vitu havikushuka kwa wakti muafaka. hivi sasa mambo ni kama kawa na ili kuwashawishi mnisamehe kwa hilo naomba msikilizeni kylnn kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Safi sana kamati, hii style ya kutoa cash nimeipenda ni mfano wa kuigwa badala ya kuwanunulia chereni au used fridge.

    Ushauri: next time kamati ikusanye michango yote na kuwakabidhi maharusi badala ya kukodi ukumbi na kunywa. inaweza kuwasaidia wakanunua au hata kujenga kakibanda na kuepukana na adha ya kupanga.

    ReplyDelete
  2. KWELI HELA YA MADAFU SIKU HIZI HAINA THAMANI. KILA KONA DOLA. ADA YA SHULE KWA WATOTO, DOLA, MCHANGO WA HARUSI, DOLA. MWISHOE ITAINGIA NAULIA YA DALADALA HADI KWENYE VIDUKA MKOBA. SHILINGI INAPOTEA KIDOGO KIDOGO.TUNADHANI NDO UJANJA. jk sisimizi

    ReplyDelete
  3. Yani hii kamata ndio kwamba ilifikia etc (end of Thinking Capacity)?????

    Ni aibu kwa karne hii kwa kamati ya harusi kutoa pesa kama zawadi ya kamati!.
    ni ukosefu wa planning na creativity.

    Hivi hawa maharusi watakuwa na nini kama kumbukumbu ya harusi yao?.
    Hela sio zawadi muafaka kwani after a while mtu anazitumia kivyke na kupoteza kabisa maana.
    kwani zawadi ya harusi inabidi maharusi waikumbuke daima na milele ktk maisha yao.

    Inanisikitisha zaidi kuona kwamba Wanahabari wamekosa ubunifu kiasi hiki! Hii ni aibu kwa wanahabari wa Delenyuzi, kwani hawa maharusi wote wanafanya kazi hapo. Michuzi akiwa mmoja wao, tena bila aibu anaiweka hii hewani. kazi ipo!

    No wonder wanahabari wengi wanakuwa reporters, au story tellers. Ubunifu zero au umeenda likizo. na hali hii inaweza ikawa zaidi ktk vyombo vya habari vya serikali.

    Hela sio zawadi muafaka!, hapo kamati ilichemsha na maswahiba wa maharusi mmeonyesha udhaifu wakuishawishi kamati kubadilika.

    Mbona hujatuwekea picha za zawadi wa wafanyakazi wa delenyuzi? au mlikuwa mashehe ubwabwa, hwamkwnda na zawadi.
    kavu kavu - tigo kwa tigo... Noma washikaji, hivyo sivyo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2007

    USHAMBA!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2007

    Ndugu zangu kutoa hela sio ushamba,huu ni ujanja sababu mtu unaweza ukamnunulia kitu kwa mtazamo wako ukizani kizuri kumbe kwake ni takataka kwa hiyo ukimpa hela anaweza akafanya kitu ambacho kina manufaa kwake

    Pili siku hizi Bongo wanakuuliza wakununulie zawadi gani, sasa wewe mwenyewe ndo unaamua kitu gani kinunuliwe, kwa hiyo basi wewe unaweza ukawa unataka kitu fulani lakini ghalama ya hiyo kitu inazidi hela iliyopo,hapo kinachofanyika unapewa hela ili uongezee ununue kitu ukipendacho

    Kwa ujumla huu ni utaratibu mzuri sana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2007

    Mchango wa harusi ni sawa mkimpa mtu afanye anavyotaka harusi yake lakini zawadi ya harusi ni zawadi.

    Tukumbuke zawadi ni zawadi na sio kusaidiana maisha. Na wenye kamati hiyo wameharibu wangemuuliza nini anataka na kwa hela zao au uwezo wako wangemnunulia.

    Haka kamchezo kameanza hata nchi za nje watu wasiporegister kwenye duka lolote basi wanasema tunataka hela badala ya maua. Nani kakwambia analeteaga maua kwenye harusi? Kama sio njia ya kuomba hela tu. Siku hizi watu wengine wamefanya harusi ni mahali pa kutafuta mtaji au a house down payment money

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2007

    SIKU HIZI TANZANIA TUNATUMIA DOLLAR?JAMANI HII KAZI KWELI.INA MAANA MICHANGO YA HARUSI ILIKUWA NI $???TUACHE UBISHOO WA KIJINGA.

    TUWEKEE PICHA ZA MAANA ISSA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...