kwa msiofahamu ni kwamba uwanja wa kumbukumbu ya karume stedium umekuwa kituo cha mazoezi ya kabumbu kwa timu za taifa za wakubwa na vijana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2007

    is that a calender? what is that thing?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2007

    Safi sana....
    Haya ni Matunda ya Mbrazil Marcio Maximo.
    hilo ni goli la kufundishia wachezaji target/shabaha ili wasiwe watu wa butua-butua

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2007

    Mbona mnapenda kudanganyana. Hilo sio goli huo ubao wanatumia kuwafundishia tuition ya hesabu wachezaji wetu.Nasikia mpira wa siku hizi ni mahesabu matupu,ila sijui sasa hesabu hizo zinatumikaje.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2007

    Mimi ni kijana sana kuweza kukumbuka lakini naambiwa Gibson Sembuli na wengine baada yake walikuwa wanawekewa matairi ya magari golini katika level tofauti na kocha Tambwe Leya (kama sikosei - si nimesema mie kijana sana kukumbuka?) ili walenge shabaha.

    Sasa nini kilitokea waTanzania hatufanyi tena vile mpaka Maximo kaja kufufua?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2007

    UCHAMBUZI WA GAZETI LA MWANANCHI KUHUSU MAANDALIZI YA TAIFA STARS

    Taifa Stars inatakiwa marekebisho kabla ya kuivaa Senegal


    *Mechi ya Uganda Cranes imeonyesha sura ya timu

    Na Frank Sanga

    TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakuwa na kibarua cha aina yake, Jumamosi itakapojitupa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kurudiana na Senegal.

    Huo ni mfululizo wa mechi za kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Ghana, Januari mwakani.

    Kwa sasa timu hiyo iko katika mazoezi makali kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

    Stars, Jumamosi wiki iliyopita ilikuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Uganda Cranes na kutoka nayo sare ya 1-1, huku ikitangulia kujifunga.

    Lakini ili Stars kushinda mchezo huo itatakiwa kufanya marekebisho mengi ya haraka na hasa kutokana na jinsi walivyocheza mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Uganda, Jumamosi iliyopita.

    Bila shaka wachezaji wa Stars walioanza dhidi ya Uganda, wengi wao ndio watakaoanza dhidi ya Senegal na kama yatakuwapo mabadiliko hayatazidi ya wachezaji wawili.

    Ukiondoa nafasi ya kipa, Ivo Mapunda ambaye alicheza vizuri pengine kuliko mechi zozote, katika nafasi nyingine kulikuwa na makosa ambayo inabidi kocha, Marcio Maximo ayafanyie kazi kwa siku nne hizi zilizobaki kabla ya mechi ya Senegal.

    Katika mchezo dhidi ya Uganda, Maximo aliwapanga wachezaji wake wacheze mchezo wa kushambulia kwa kushtukiza 'counter attack', lakini itakuwa ni hatari kubwa iwapo ndio amepanga kucheza hivyo dhidi ya Senegal.

    Tatizo kubwa la kushambulia kwa kushtukiza kwa timu kama Stars ambayo haina wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi ni hatari kwa sababu huwa unafanya timu ishambuliwe zaidi na kufungwa magoli ya kizembe.

    Mchezo wa kushambulia kwa kushtukiza dhidi ya Uganda, uliwashinda wachezaji wa Stars, badala yake wakajikuta wakiruhusu kushambuliwa wao muda mwingi wa mchezo na bahati nzuri, Ivo Mapunda alikuwa makini langoni.

    Uganda ambao watacheza na Nigeria Jumamosi, walionekana kumiliki zaidi mpira na kupanga mashambulizi, huku Stars ikionekana kujihami zaidi na kuruhusu lango lao kuwa katika wakati mgumu zaidi.

    Wakitumia mfumo wa 4-4-2, Stars walikuwa wamejazana zaidi katika nafasi ya kiungo, huku mabeki wa pembeni wakiachiwa uhuru wa pande zao kutokana na mawinga kuingia kati kucheza kama viungo.

    Shadrack Nsajigwa ambaye alicheza kama beki wa kulia, aliachiwa nafasi ya kutawala upande wake wote wa kulia kutokana na winga wake wa kulia, Shaaban Nditi kuingia katikati kucheza kama kiungo, hivyo hivyo ilikuwa kwa beki wa kushoto, Mecky Maxime ambaye aliachiwa upande wote wa kushoto huku Abdi Kassim ambaye alikuwao akiingia zaidi katikati.

    Mbinu ya Maximo ilikuwa ni kuwataka mabeki wake wa pembeni, Nsajigwa na Maxime wapande kwa uhuru na kumimina krosi langoni mwa Uganda, lakini hatari yake ilikuwa kubwa kuliko faida.

    Kuwaruhusu Nsajigwa na Maxime kupanda muda mwingi kuliwafanya wachoke mapema na kuwapa nafasi mawinga wa Uganda, Danny Wagaluka na Massa Geofrey kuleta hatari nyingi katika lango la Stars.

    Kuanza kwa mchezo tu, Wagaluka alianza kufanya vitu vyake na kumtoka Maxime na krosi yake ndio ilimfanya Nsajigwa ajifunge kwa kumrudishia mpira kipa, Ivo Mapunda akiwa hatua tatu hivi kutoka katika mstari wa lango.

    Nsajigwa alifanya hivyo akimzuia Massa Geofrey asiuwahi mpira huo uliokuwa umetoka winga ya kulia.

    Mpira huo wa dakika ya pili haukuwa wa hatari sana kama Nsajigwa angetulia, lakini kwa sababu ya utelezi kidogo, alijikuta kama kukosa 'balance' na kupiga shuti ambalo lilitinga wavuni na kumuacha Mapunda akishangaa.

    Kwa muda mwingi sana, Stars ilishambuliwa kupitia upande wa mawinga wa Uganda na jambo ambalo kubwa ni kwamba Nsajigwa na Maxime hawakuwa katika kiwango cha kuwakaba Wagaluka na Massa.

    Ikumbukwe kuwa Uganda ilicheza mchezo huo bila wachezaji 12 wanaocheza soka nje ya nchi. Miongoni mwao ni Dennis Onyango, David Obua, Timothy Batabaire, Hassan Mubiru na Nestory Kizito.

    Kuna mambo mawili ambayo unaweza kuwatetea, Nsajigwa na Maxime: Kwanza mawinga wao; Nditi na Abdi walikuwa hawakabi ipasavyo na hivyo kuwafanya mabeki hao wa pembeni kujikuta wakilemewa na mzigo mzito kutoka kwa mabeki wenzao wa pembeni wa Uganda waliokuwa wakisaidiwa na mawinga wao.

    Lakini jambo la pili ni kwamba, ilionekana Nsajigwa na Maxime walitaka kila mpira wanaoupata wapande nao mbele jambo ambalo wakati mwingine lilikuwa gumu kwani mipira iliponaswa ilipigwa upande huohuo ambako beki alikuwa ameondoka na kuleta kizaazaa kwenye lango la Stars.

    Kupanda sana pia kuliwafanya mabeki hao wa pembeni kuchoka kiasi kwamba ilibidi wakati mwingine kujisahau mbele huku wakiacha 'nyumba' ikitaka kuungua langoni mwa Stars.

    Makosa kama hayo yalifanyika pia katika mchezo wa kwanza dhidi ya Senegal mjini Dakar ndio maana karibu magoli yote yalipitia upande wa mabeki wetu wa pembeni.

    Kama hali hiyo haitarekebishiwa kabla ya mchezo wa Jumamosi, itakuwa ni kazi rahisi kwa Mamadou Niang na Diomansy Kamara kufanya vitu vyao na kuleta madhara kwa Stars.

    Maximo anatakiwa kuwaelekeza vizuri mawinga wake jinsi ya kucheza kama viungo huku wakikumbuka wajibu wao wa kukaba upande wao wa winga na si kuwaachia mabeki wa pembeni tu.

    Ukiondoa makosa hayo ya mabeki wa pembeni, kulikuwa pia na makosa madogo kwa mabeki wa kati, Salum Sued na Victor Costa ambao walitakiwa kuacha kucheza kama inavyotakiwa na kujikuta wakienda kusaidia mabeki wa pembeni na hivyo kufanya wakati mwingine lango kuwa wazi bila ulinzi.

    Hilo halikuwa tatizo sana kwani viungo, Henry Joseph na Shaaban Nditi walikuwa wakirudi kuziba nafasi, lakini Costa na Sued watatakiwa kuacha kutegeana kwani kuna wakati walionekana kutaka kuachiana mpira jambo ambalo lilitaka kuleta madhara katika mchezo huo.

    Kosa kama hilo lilifanyika katika mchezo dhidi ya Senegal wakati Stars ilipofungwa bao la pili la kizembe kutokana na mabeki kutegeana.

    Kama alivyofanya katika mechi nyingine nyingine karibu zote, Costa katika dakika ya 16 akiwa eneo la hatari alimgeuza mshambuliaji wa Uganda, Eugene Sepuya na ingawa alishangiliwa, lakini ilikuwa ni hatari sana kama mpira ungenaswa na mshambuliaji huyo.

    Upande wa viungo ambao ulikuwa chini ya Henry Joseph, Shaaban Nditi, Abdi Kassim na Nizar Khalfan ulishindwa kuipandisha timu mbele, badala yake wakaonekana kutaka kujihami zaidi na kuwaruhusu Waganda kumiliki mpira. Walipanda mara chache sana.

    Mipira ilipokuja walishindwa kuipeleka timu mbele, badala yake walitoa pasi ndefu ambazo ama zilidakwa na kipa wa Uganda, Muwonge Hamza au zilisababisha washambuliaji kuotea.

    Kuingia kwa Haruna Moshi na Amiri Maftah katika nafasi ya kiungo badala ya Nizar na Abdi hakukubadilisha sana, ila Haruna ambaye alitakuwa kucheza nafasi ya Nizar, naye akaonekana kucheza nafasi ya kiungo wa nyuma na kufanya timu kujihami zaidi.

    Kwa upande wa ushambuliaji walipoanza Joseph Kaniki na Danny Mrwanda, ilionekana mabeki wa Uganda kukosa raha kwani washambuliaji hao wa Stars walikuwa wanacheza kwa akili.

    Wakati Mrwanda alikuwa akirudi na kuchukua mpira na kuwapiga chenga mabeki, Kaniki alikuwa na kazi ya kupelekena puta katika mikikimikiki ya kuwania mpira na kumfanya Mrwanda kupata nafasi ya kuwatoka mabeki kuwa rahisi.

    Alipotoka Kaniki kwa kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Said Maulid kulileta mambo matatu; jambo la kwanza ni kasi ya mchezo upande wa ushambuliaji iliongezeka.

    Lakini ikumbukwe kuwa uchezaji wa Mrwanda na Maulid unalingana kwa kiwango kikubwa tofauti yao ni kwamba wakati Maulid hupiga mpira na kuanza kuufukuza, Mrwanda hukimbia na mpira ukiwa mguuni.

    Kutokana na washambuliaji hawa wawili wote kuwa na kasi, ilisababisha viungo kubadili mfumo wa kuanza kutoa pasi ndefu, lakini nyingi zilisababisha 'kuotea'.

    Wakati fulani mwamuzi, Ali Kalyango alionekana kujichanganya, kasi ya Mrwanda na Maulid ilimshinda na kudhani wameotea kumbe ni kasi yao ya kuuwahi mchezo.

    Wakirekebishwa na kucheza pamoja Jumamosi wanaweza kuwa na madhara, lakini kuna tatizo la wachezaji hawa wawili kuingiliana mara kwa mara katika nafasi zao.

    Mrwanda na Maulid walimchanganya hata kocha wao, Maximo ambaye alishangaa jinsi wachezaji hao wanavyoweza kucheza pamoja.

    Jambo la kujisifu ambalo ni mabadiliko makubwa ni kwamba, kila ulipokuwapo mpira nyuma yake ungewaona wachezaji wanne au watano wa Taifa Stars kuhakikisha haupiti.

    Hata hivyo tatizo lilikuwa ni pale mpira ulipopita kwani walikuwa hawajipangi vizuri na kuruhusu kupitwa kizembe wakati fulani.

    Stars inatakiwa kubadilika na hasa inapocheza mechi za kimataifa kama hizo, kipa akidaka mpira inabidi apige haraka mbele badala ya kuanza kusubiri kwa dakika nzima mpaka wapinzani wajipange.

    Wachezaji wetu wanapofanyiwa faulo waache kumtegemea mwamuzi apige filimbi, inapaswa waendelee na mchezo mpaka filimbi itakapopigwa.

    Mchezo wa Jumamosi dhidi ya Senegal ni mgumu na matumaini yasiwe makubwa sana kwani tujue kuwa tunacheza na timu yenye wachezaji wote wa Ulaya.

    Tukishinda ni furaha, lakini iwapo tutafungwa isiwe nongwa kwani bado kimpira huwezi ukatulinganisha na Senegal.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2007

    structure permanent kama hii ya nini hapo karume...yaani ni uchafu mtupu na hayo marangi rangi na machokaa...maendeleo bado sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...