Home
Unlabelled
kitabu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Naomba kufahamu maudhui japo kwa ufupi tu kuwa "Simu ya kifo" kinaeleza juu ya nini.
ReplyDeleteUmenikumbusha mbali sana. Nilisoma hiki kitabu nikiwa 1st or 2nd grade. Uivyosema simu ya kifo hata sikukikumbuka lakini hii picha imenikubusha mbali sana. Nilikua silali usiku.
ReplyDeleteVitabu zamani tulikuwa tunavisoma sana lakini sasa hivi usomaji wa vitabu umekufa.Umeuawa na TELEVISION,DVD,CD za miziki.Kizazi kipya kinachotakiwa kusoma vitabu hakisomi. Kutwa wanasikiliza CD NA MIZIKI wakiwa na earphones wawe kwenye magari au njiani.Muda wowote huru walionao kama hawako darasani wanasikiliza miziki hawataki kusoma vitabu kabisa.
ReplyDeleteZamani kijana ukimkuta ana muda wa ziada utamkuta anasoma novel ikiwemo hiyo ya Simu ya Kifo.Utamaduni wa kusoma vitabu Tanzania umeuawa na miziki utafiti wa wakenya walioufanya kuhusu soko la vitabu vya riwaya Tanzania unavyoonyesha.
Soko la hicho kitabu ni halipo.Mchapishaji ajiandae kuula wa chuya.Hasara iko njiani.Nadhani hakutaka kufanya utafiti kabla kukichapisha.
Watanzania hasa wafanyabiashara ni vizuri waende shule na wasome na waelewe wanachosoma na kutumia wanachosoma vinginevyo kila kuchapo watakuwa wanaanza miradi ya hasara kama huu wa Simu ya Kifo ambao simu yake ya kifo cha faida ya huu mradi imeshalia kwa mchapishaji.
Ni kweli inabidi wazazi tuwe na mda wa kuwasisitizia watoto kusoma. Japo nusu saa tu kwa siku inatosha sana.
ReplyDeleteZamani tulikua tunasoma sana vitabu na magazeti. Na katika darasa ilikua kama ni mwanafunzi asiyejua kusoma kwa level ya darasa lake ni mmoja au wawili tu kulinganisha na sasa hivi utakuta ni wanafunzi wawili tu kwenye darasa wanaosoma vizuri kulinganisha na level yao na wengine wote wanasoma below grade level.
Either tumekua na hamu ya kutafuta hela na kusahau kuwa maanani na kujua kinachoendelea kwa watoto wetu au tumezidi kuwanunulia watoto vitu ambavyo haviwasaaidii katika elimu ila ni kwa starehe tu.
Na hata watu wasiokuwa shuleni ni vizuri kuwa na tabia ya kusoma kila siku. Pamoja na kuwa ukisoma utajifunza jipya lakini ukweli ni kuwa watu wanaosoma mara kwa mara hata wakizeeka ugonjwa wa kusahau hauwashiki kama wale wasio na mazoea ya kusoma sana.
Michuzi umenikumbusha mbali sana, enzi hizo kama hujamsoma Willy Gamba au Ray Sibanda basi wewe si mtoto wa mjini. Mambo ya Kamlete akibisha mlipue, Kikosi cha kisasi, njama na kadhalika...Achana na hawa kina Shigongo ambao wana-copy novels au movies za kizungu na kuzibadilisha ktk kiswahili ati wanaita Novels, so retarded. Aminia Hammie Rajab
ReplyDelete