balozi mwanaidi maajar akiwa na msaidizi maalum wa mzee kawawa kaka luanda wakati wa hafla ya muungano jijini landani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2007

    huyu mama kwa vipati mwe hajambo hakosi kipati chochote hapo london.mwee jk kweli ameula wa chuya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2007

    Hivi huyu anyeandika upuuzi huo kuhusu Balozi wetu anaelewa mambo au anajiandikia tu.
    Sherehe ya Muungano nayo unaiita ni vijipati vidogo na hebu nikueleze jema lipi Mabalozi waliopita walikuwa hawajichanganyi na Watanzania ikawa kero huyu mama wa watu amejitolea kuwa karibu na watu unapiga kelele za kipuuzi.
    Michuzi hebu maooni mengine yachuje bwana yanakera.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2007

    My dear brother Michuzi.

    Asante sana kwa kuendelea na hii blog ambayo wengi wetu tunaisoma.

    Nasikitika sana na maoni ya huyo annonymous no. 1 hapo juu. Kwanza, mimi ninaamini kabisa huyu ni mtu kutoka huko huko London aliyeandika hii comment. Halafu eti anaandika "hapo London". Angeandika "hapa London",angekuwa sahihi. watu wa huku nyumbani au nje ya London, watajuaje kuwa mama anahudhuria hizo party?

    Pili hiyo comment, mimi ninaamini kuwa si ya kweli kabisa. Huo ni utovu wa nidhamu. Anataka huyu mama ajifungie tu? Atawajuaje watu wake? Jamani tuwe na fair comment kwa viongozi wetu na tuwe na adabu pia.

    OMBI KWAKO KAKA MICHUZI:
    Kama inawezekana kaka yangu, ninaomba uiondoe hiyo comment ya hapo juu. Maana inaweza ikawafanya watu waamini na akili zao zikawa corrupted na kumchukulia vibaya huyu mama yetu. Wengi wetu tunamheshimu, kama baadhi ya watu hasa aliyeandika hamthamini, basi. Lakini mkumbuke kuwa, "Ukiwa nacho, hukithamini, kikikutoka ndipo hapo utakapoanza kujuta na kuona tofauti."

    Kaka Michuzi, naomba ulifanyie hisani ombi langu. ASANTE SANA.

    Mungu ibariki Afrika,
    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2007

    Balozi ni mtu kama watu wengine wowote ana marafiki,jamaa n.k na ni mwafrika.

    Yuko huru kuhudhuria hata ngoma akitaka au kisherehe chochote kiwe cha Ikulu au uchochoroni kwa ndugu au marafiki zake.

    Wewe unayesema anahudhuria vipati una maana gani.Kitu cha mwenzio kuita kipati si sahihi. Hicho uitacho kipati kwa aliyekiandaa ni bonge la pati.Ukome kuwa na mtizamo individualistic ambao kila unachokiona unalinganisha na vyako au vya mtizamo wako.Dunia haiko hivyo.

    Mnataka balozi ajifungie kama mwali ubalozini! Huyu ni balozi wa watu kule London siyo balozi wa kuta za ubalozi.Kukiwa na shughuli ya watu iwe private au public akiwa na nafasi yuko huru kwenda acheni kumnyanyasa.Angalieni mabalozi wa mataifa mengine kama India muone wanavyojichanganya na watu wa jamii zao hawajifungii ndani.Wao wakati wote huwa ni part and parcel of their society.Iwe msiba,sherehe n.k

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2007

    Freedom of speech. Nini maana ya demokrasia?

    Mungi ibarki Africa
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2007

    Jamani Watanzania hawakosi lakusema hata ufanyeje, ndio maana kamwe hatutoendelea, KAMWE. Mama wa watu anajitahidi kadri awezavyo kuwa karibu na watu so what is wrong with that? Angekuwa anajifungia ndani mngesema 'oh balozi mwenyewe hapendi watu'.... Acheni unafiki wenu na muacheni Mheshimiwa wetu she is doing just fine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...