Home
Unlabelled
msuli
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Sir Issa..vipi ustaadh NAONA UMEPATA HII PICHA..UTAMADUNI SAFI HUO...MHESHIMIWA LOWASSA KAPENDEZA SAAANA...VAZI LA MWAMBAO LIMEMKUBALI HUYO..."..LAKINI MSULI HAUENDANI NA SURUALI MAALIM.."
ReplyDeleteMimi siandiki chochote kuhusu Lowasa.Huwa hapendi kukosolewa au kuandikwa vibaya au kuandika umbeya unaomhusu ambao ni wa kweli.
ReplyDeleteNamnyamazia Kimya yaje yamkute kama yaliyomkuta Sumaye,Waziri Mkuu aliyemtangulia maana naye alikuwa hapendi na hataki wakosoaji dakika ya mwisho akaanguko anguko la mende.
Hivi PM alikuwa hajatoa mchango wa nyama hadi Leo!!
ReplyDeletekwetu ukivaa msuli namna hii watu watakuuliza "kidonda hakijapona bado??".
huwa wanavaa watu wakitoka Jando.
sasa sijui hapo Primier nae ni hivyo hivyo au alikuwa kwenye boutique anachagua pamba!
Michuzi usiogope ku-post hii komenti yangu. Wamasai ni watani zangu. so is Lowasa.
RICHMONDuli...
ReplyDeleteJamaa siku likimpasukia sijui itakuwaje. Sema Kikwete ana mbeba mpaka wa anguke wote puuuu we subiri
Muheshimiwa Lowassa hapendi kukosolewa kwasababu anafahamu ukweli unauma. Angekuwa mkweli kwa watanzania angekuwa mnynyekevu na mwenye kusikia kilio cha wengi, na kufanya marekebisho pale yanapohitajika. With Richmond as his business he doen't want to hear any criticism.
ReplyDeleteKuna jambo moja huwa nashindwa kuelewaga Tanzania, hivi inakuwaje kiongozi apewe zawadi na watu wenye vipato kidogo maradufu yake pindi awapo ziarani?
ReplyDeleteHaoni aibu kupokea zawadi kwa watu ambao "hawapati umeme".....Richmonduli...
ReplyDeleteDC mstaafu awaonya viongozi dhidi ya zawadi
ReplyDelete(http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/5/10/habari32.php)
ALIYEWAHI kuwa mkuu wa wilaya (DC), mbunge na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni Lepilal ole Moleimet, amekosoa mtindo wa viongozi kupewa zawadi vijijini na kusema kuwa unawagawa wananchi.
Akizungumza na Tanzania Daima mjini hapa, Moleimet, ambaye pia ni ofisa mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), aliwata viongozi wa kitaifa kufahamu kuwa zawadi wanazopewa, zimepatikana baada ya wananchi kubinywa sana na viongozi wao.
Moleimet, aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya kwa zaidi ya miaka 14, katika wilaya mbalimbali na pia mbunge ambaye hivi sasa ni kada wa CCM, alisema wananchi wanalazimishwa kuchanga kwa ajili ya kupata zawadi za viongozi na kusababisha manung’uniko makubwa baadaye.
“Inasikitisha sana kuona viongozi wa ngazi za juu serikalini na chama kuridhia kuondoka na zawadi walizopewa na viongozi wa vijiji na kata bila kujiuliza zimetoka wapi wakati wananchi wa maeneo hayo ni masikini wa kutupa, ambao bado wanahitaji huduma muhimu ili kukidhi maisha yao,” alisema Moleimet.
Moleimet alisema kuwa aliyapata manung’uniko hayo kutoka vijiji kadhaa katika wilaya za Longido na Monduli, alivyovitembelea hivi karibuni.
Alisema viongozi kadhaa waliowahi kuyatembelea maeneo hayo hivi karibuni, walipewa zawadi nyingi na wao wenyewe hawana habari kuwa zawadi hizo zimetengeneza uhasama kati ya wananchi na viongozi wa vijiji.
“Wananchi wa maeneo haya ni wafugaji ambao wengi hawana elimu ya kutosha… wanatishiwa na viongozi wao na wanatoa ng’ombe na mifugo mingine, baadaye wanabaini kuwa walitishwa na uhasama unaanza,” aliongeza.
Alisema kwa sasa wananchi wengi wamekuwa wakinung’unika chinichini, lakini utafika wakati wataanza kuhoji dhana ya kuwataka kuchangia zawadi za viongozi ambao kwa msingi wanaishi kwa kodi zao.
“Mimi toka nimeanza kushika madaraka ya uongozi wa nchi hii wakati wa hayati Mwalimu Nyerere, sijawahi kuona hali kama inayojitokeza hivi sasa… watu kuingia madarakani kwa mwaka mmoja tu na kuanza kupewa zawadi lukuki ambazo hazijulikani ni za nini na wao kujichukulia bila kuhoji wanapewa kwa sababu ipi,” alisema.
Alisema wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere, pamoja na kutawala kwa muda mrefu, lakini alikuwa akifika mahali na kuanza kupewa zawadi, aliuliza ni za nini na akikabidhiwa huamua kuzitoa kusaidia shughuli za maendeleo katika eneo husika.
“Hivi sasa viongozi wote walioratibu utoaji zawadi kwa viongozi wa kitaifa wamekuwa miungu watu vijijini kwani mtu akionekana kupingana na maamuzi yoyote ya viongozi hao, hutishiwa kushtakiwa ama kwa rais ama kwa waziri mkuu na hali hii imeondosha dhana ya utawala bora hapa nchini,” alisema.
Alisema hali hiyo pia imechangiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa juu wa serikali kuwa na sauti za maamuzi hata katika jambo dogo lililopo katika ngazi ya kata.
Hawa wadau mtaficha wapi sura zenu sasa? Richimonduli hiyooo
ReplyDeletePCB yaisafisha tuhuma za rushwa Richmond
Jonas Songora na James Magai
TAASISI ya Kuzuia Rushwa nchini (TAKURU) imeisafisha kampuni ya Richmod Development Company dhidi ya tuhuma za rushwa zilizokuwa zikiikabili katika uingiaji wa mkataba wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kwa TANESCO.
Akizugumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya Takuru , Upanga jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Takuru, Edward Hosea alisema kuwa hakuna ushahidi wowote uliopatikana kuthibitisha vitendo vya rushwa, uzembe, au upokeaji wa kamisheni kwa watendaji wa serikali.
Kusafishwa huko kwa tuhuma za rushwa dhidi ya kampuni hiyo, serikali na wadau wengine kunakuja baada ya kuwepo mingong'ono ndani ya jamii na hata serikali na bunge.
Alisema kuwa uchunguzi huo ulithibitisha kuwepo kwa mapungufu ya kawaida katika utendaji na ambayo hayakuhusisha rushwa au manufaa ya aina yoyote ile kwa upande wa watendaji na hakuna hasara iliyosababishwa na mapungufu hayo.
Katika ushahidi uliopatikana kufuatia uchunguzi huo, Hosea alisema kuwa kampuni ya Richmond Development Company, LCC ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited inayomilikiwa na Naeem Gire ambaye ana uraia wa Tanzania na Mohamed Gire ambaye ni raia wa Marekani, ilifanikiwa kushinda zabuni iliyotangazwa na TANESCO baada ya kuyashinda makampuni mengine manane yaliyojitokeza.
Aliongeza kuwa kampuni hiyo ilishinda zabuni hiyo baada ya Kamati ya tathmini yenye watu kumi na mbili, wakiwemo wajumbe wanane kutoka TANESCO, mjumbe mmoja mmoja kutoka Wizara za Fedha, Nishati na Madini, na wajumbe wawili kutoka Kampuni ya ushauri ya Laymeyer International ya Ujerumani ambayo ni kampuni ya ki- ufudi kwa TANESCO.
Hata hivyo kutokana na hali ya dharura na uharaka wa kutatua tatizo la umeme, alisema kuwa serikali iliamua kuingilia kati na Waziri Mkuu aliamua kuunda kamati ya watu watatu ilio kuharakisha zoezi hilo baada ya kuona kuwa utaratibu wa kutumia soko la kimataifa la wazabuni ungezidi kuchelewesha upatikanaji wa umeme.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Katibu Mkuu Hazina ilipewa jukumu la kuishauri serikali kwa uharaka zaidi, na kuweka vigezo ikiwemo mzabuni kuthibitisha uwezo wake kiufundi, uthibitisho wa bei kutoka kwa mzabuni, na kueleza muda atakaotumia hadi kuanza uzalishaji, ambapo kampuni ya Richmond ilithibitika kuwa na sifa zinazotakiwa.
Aliongeza kuwa Richmond ilithibitisha kuwa na sifa zinazotakiwa kwa kushirikiana na kampuni kubwa ya Pratt and Whitney yenye uzoefu mkubwa katika utengenezaji na uzalishaji wa umeme na pia kuthibitisha kuwa inaweza kuingiza umeme ndani ya wiki kumi na nne.
Akizungumzia kuhusu kushindwa kutekeleza kwa mkataba ambao Richmond iliingia na serikali, Hosea alisema kuwa baada ya kuthibitishwa Richmond kushindwa kutekeleza masharti ya mkataba, serikali haikuilipa kampuni hiyo hadi ilipouza kazi zake kwa kampuni ya Dowans Holding SA Disemba 21, 2006 ambayo ndiyo inastahili kupewa malipo ya usafirishaji mtambo.
Aliongeza kuwa Richmond ilipaswa kuilipa TANESCO fidia ya ucheleweshaji huo kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 kwa siku kuanzia Februari 20, 2007 kwa vile shughuli za Richmond ziliuzwa kwa Dowans, adhabu ambayo kwa sasa italipwa na kampuni hiyo.
Taarifa hiyo ya uchunguzi imekuja kufuatia malalamiko yaliyojitokeza kufuatia mchakato mzima wa utoaji zabuni ambapo serikali iliingia mkataba wa kukodi mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kufuatia kina cha maji kupungua katika mabwawa ya kuzalishia umeme ambapo serikali iliingia mkataba na Richmond kupitia TANESCO mwezi Juni 23, 2006.
Hata hivyo baadhi ya watendaji wa serikali walishutumiwa kuwa wamiliki wa kampuni hiyo ambayo ilishutumiwa sana kutokana na kuchelesha uletwaji wa majenereta hayo ya kuzalisha umeme wa dharura.