WARAKA KWA WAFANYAKAZI WA POSTA TANZANIA

Mimi nikiwa ni Mtanzania niishiye marekani kwa kweli ninakereka mno na tabia ya kampuni ya POSTA hapo nyumbani.
Nitaanzaia kwenye barua tu za kawaida, yaani it takes sometimes up to a month kwa barua kutoka huku kumfikia mlengwa hapo nyumbani,and mind you here am talking about huyo mlengwa aishie DAR, it is hard to imagine how long will it take for a latter to get to KAMACHUMU huko BUKOBA kagera au say LINDI kwa kweli inasikitisha saaana hali hiii?
Nikitoa mfano wa hili la barua nakumbuka mwanzoni mwa januari nilituma documentation Fulani za mamboya uhamiaji huko nyumbani nah ii ilikuwa ni kwa EMS na hapa nilielezwa it will take the most three day,na nataka ukumbuke hiyo EMS ndio service ya post ya haraka lakini wapi ,ilichukua almosta month kufika huko {DAR} yaani ilibidi nitume tena kwa DHL same documents kiasi kwamba the fist documents zinafika Dar huyo mtu tayari alikuwa ameisha ondoka nyumbani Tanzania!!
Now the main reason of me writing here ni kuhusu kutuma vifurushi huko nyumbani,duhhh!! Hata sijui nianzie wapi kwa kweli it is a shame.
Nilituma zawadi huko nyumbani toka tarehe 21 mwezi wa pili mwaka huu,na kwa kujua tuu what kind of people I am dealing with nikaweka na insurance kwenye huo mzigo kwani ulikuwana atleast na thamani ya $300 hivi na huku ukituma mzigo basi unaandika what is in the box na thamani yake.
Mpaka leo hii ninaandika waraka huu huo mzigo haujafika na pia nilitumia huduma ya haraka kwani ilikuwa ni zawadi kwa wakati maalum na nilitaka ifike kwa wakati muafaka{birthday presents},nilipopiga simu kwenye posta ya huku wao walinambia mzigo umeishafikatarehe 28 february kule nyumbani ,na wakati huo ilikuwa ni mwanzoni mwa mwezi wa tatu .
Na kwa kweli mpaka sasa huo mzigo haujafika {mimi ninafahamu fika ya kuwa hawa watu wanaiba mizigo pale posta nyumbani}, na nimefungua claim na watu wa posta hapa na wanasema wanawasiliana na watu wa posta nyumbani wacheki may be the did hold the parcel in immigrationand custom offices for reasons they know best,lakini bado hatujapata majiu yeyote kutoka huko mpaka usawa huu,hawa jamaa wao wana policy ya kusubiri kwa siku sitini before they do anything ,sasatokea nipate hiyo claim number bado hizo siku hazijafika.
Swali langu kwa hawa wakuu wa posta na kwa watanzania wote kwa ujumla je kwa namna hii kweli tutafika,au ndio hiyo ARI MPYA ,NGUVU MPYA NA KASI MPYA katika wizi huu wa kimachomacho
Ndimi mdau toka USA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2007

    Posta ya Tanzania ni wezi wakubwa. Nilituma picha za mtoto wangu toka U.S. hazikuwahi kufika. Tatizo wakiona bahasha ina stempu ya U.S. wapumbavu wa posta wanafikiri kuna hela ndani. Na hao EMS ndio mafirauni kabisa. Wanakula rushwa wakisingizia hela ya tax. Washenzi kabisa. Inabidi posta na EMS Dar isafishwe kabisa. Wafukuze wote, na waajiri upya watu wapya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2007

    Mie nilituma kifurushi mwezi wa 9 2006, kimefika baada ya mezi sita na nusu-mwaka huu mwezi wa tano. Sikuweka insurance, lakini nilituma kwa njia ya kawaida. sasa sijui tatizo ni njia niliyotumia au ni pale posta wanachelewa ku-sort vifurushi. Nilikuwa nimeshakata tamaa!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2007

    Posta hapa hawajui kuwa biashara ya posta inahusika na vitu viwili tu.

    1.uaminfu
    2.Uharaka

    ndio maana siku hizi watu wanaacha kufuata huduma za posta wanakimbilia mashirika binafsi ya usafirishaji barua na vifurushi na mabasi na malori ya watu binafsi.

    Posta Tanzania mjue kifo chenu cha vibarua kiko njiani msipojali hivyo vitu viwili.Inaonekana kazi inawashinda lakini tatizo ninaloliona posta ni hasa

    1.Wana wafanyakazi wazee wasiosoma wengi sana.Posta imejaa form failures wengi sana ambao hawataki kujiendeleza na wagumu kubadilika.

    Kiwango cha elimu kazini kwenye utandawazi hakitegemei aina ya kazi bali aina ya watu unaowahudumia.Ndio maana hata mahoteli makubwa huhitaji wasomi wa vyuo vikuu si kwa sababu ya Kazi ya aina ya kazi bali aina ya watu unaowahudumia.

    Ushauri wa bure kwa posta ni kuwa Kitengo cha barua na virushi vya nje ya nchi wawekeni wasomi.Hoteli za kitalii wanatakiwa wasomi,Ikulu wasomi,N.k Iwe dereva,Mpishi etc unatakiwa uangalie aina ya watu anaohudumia siyo kazi kuwa oh! kazi hii hata aliyefeli aweza fanya siyo hivyo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2007

    SAWA HAWA JAMAA WANATABIA YAKUCHOMOA VIFURUSHI TOKA NG'AMBO.
    ILA NAWEWE HIYO ENGLISH YAKO NI YA KIMA BOX BOX TU.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 10, 2007

    Best Mdau wa USA, acha kumpigia mbuzi kinanda. Pumzisha vidole vyako bwana. Tumia DHL. Mi niko Dar DHL parcel yangu ikifika wananipigia simu kisha wananiletea parcel hadi mlangoni, nasign receipt then narudi ndani kuendelea na shughuli zangu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 10, 2007

    Mzee/Bibi hiyo ndiyo inahitwa bongo, suala hilo linaeleweka barabara na vibosile wa posta. Pole sana.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 10, 2007

    Hila mzigo kutoka Tanzania unafika muda mfipi sana. Mpaka marekani inatumia siku kama saba.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 10, 2007

    Hello, Pole sana kwa yaliyokupata. Nilishawahi kuwa kukumbwa na haya pia. Kumbuka miezi michache iliyopita nilitoa malalamiko yangu kwa kupitia blog ya michuzi na watau wakachangia sana.

    Vitu nilivyo mtumia rafiki yangu havikufika kabisa hadi leo ingawa niliweka bima na kila kitu. Kampuni ya huku UK wameishia kunilipa pesa yangu na wakaniambia kuwa mizigo yangu imepotelea TZ.

    Ni jambo la aibu sana. Nilipo lalamika, nilishangaa watu wengine kuniambia kuwa mimi si mzalendo, au kwamba naikandia nchi yangu kwa kuwa niko ulaya. Raha yao ni kwamba tusiseme kitu ili tuonekane wazalendo hata kama kuna uchafu unatendeka. Dawa yao ni kutuma mizigo kwa mashirika ya kigeni ambao ni waaminifu, wasipoingiza pesa watabinafsisha na huduma zitakuwa nzuri zaidi. Pole sana!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 10, 2007

    Sir, I symphathise with your problem but you fail miserably to make your point. You have got to be articulate man, rambling and bragging will not makes your complaint inffectual.

    Tatizo Watanzania wengi mnaishi Marekani lakini shule hamjaenda. All you do is nitpick about how the country should be run, blah blah. Imitating to talk like African Americans is the only thing most of you do, hiyo haitawafikisha popote ndugu. Someni ili mje mshiriki kwenye ujenzi wa taifa. The private sector is booming in Tanzania. Ila watu kama wewe mkirudi Bongo mtabakia kusema...hey yo...hey yo..what's up wichuu...Bongo siyo SE, Washington.

    In short, nyinyi Watanzania mlioko Marekani mnapenda ku-criticize halafu tatizo ni kwamba hamjui constructive criticism!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 10, 2007

    Kaa chini uandike kwa makini unachotaka kueleza. Mambo ya kiswaenglish hamna atakaye kusikiliza. Hata kama uko marekani kama umeelimika tumia kiswahili sanifu au kiingereza basi.
    naomba kwakilisha

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 10, 2007

    Bad lucky mimi vitu vyako vinachelewa kufika. Mimi nimetuma mwezi uliopita kwa kutumia EMS niliambiwa 7 days lakini ilitumia 10 days. Kila kitu kilichotumwa kilifika salama

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 10, 2007

    Bwana wee mi nimetuma percel imagine ni printed materials toka Malaysia Wallah nimetuma mwezi wa pili tarehe 17 hadi leo havijafika na huku waki track wanasema wali handover the 5th day baada ya kupokea toka kwangu lakini huko Tz bwana sijui kuna mdudu gani yaillah toba!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 10, 2007

    Mi nakuunga mkono kabisa. hii ni wizi, hapo posta karibia 99% ya wafanyakazi wadokozi na wanadhani kila kitokacho abroad ni deal. Mimi nilituma barua nyumbani kwa express kutoka UK waliniambia ni 2days itakuwa TZ ikachukua mwezi na nusu na ikawa imefumuliwa na kusomwa na kufungwa niliweka seal wakakata hawa jamaa ni wizi pase. Nafikiri kuna haja ya kuliuza shirika kwa watu wa nje ambao wanajua maana ya business ni nini. Huweza tajirika kwa wizi wa vifurushi sana sana utaganga njaa tu. Uongozi wa Posta inaonekana unahusika na wizi huu ndio maana hawachukui hatua madhubuti.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 10, 2007

    ndugu habari yako,
    mimi naona umekuwa na bahati tu kwako,kwa kweli posta ya tanzania siku hizi wanafanya kazi kwa ufanisi,hata mimi niko nje ya nchi kama miaka 10,sijawahi kupoteza mzigo wowote,na inafika kwa muda mzuri.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 10, 2007

    Hiyo siyo ari mpya na kasi mpya bali ni wizi mpya, udhurumaji mpya na ujanja mpya. Pole sana ndugu wa huko USA, inatakiwa ujue hii ndiyo bongo, kitu cha msingi nakushauri hivyo vifurushi uwe unatuma kwa njia ya DHL.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 10, 2007

    aahhh, we umetuma hapa juzijuzi tu? bado sana muda kwa posta ya bongo.subiria miezi 10 ipite u-claim insurance ndo utashangaa mzigo unakurudia undeliverable, sasa hivi kuna mtu huko posta bongo kauficha mzigo wako sehemu anasubiria tu usipo claim unakuwa wake. ilinitokea nikawapa ndugu zangu number za mzigo kila siku wanaenda posta mzigo haupo, ikapita miezi 10 ku-file insurance after a month eti mzigo umerudi undeliverable. Bongo hata barua sasa hivi situpi, labda sana post card ndo natuma angalau nauhakika inaweza kufika, ila na post card usichague yenye picha nzuri la sivyo haifiki

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 10, 2007

    Ndugu,
    hayo yaliwahi kunipata mie miaka ya zamani kidogo, lakini niligundua dawa ya kudeal na hawa ndugu zetu - ukituma mzigo ama barua yoyote ile itume kwa njia ya REGISTERED MAIL! wakishaona iko registered hakuna atakaethubutu kuubania huo mzigo ama barua kwani wanajua kuna namba ya kuwafuatilia. Usilipie Insurance maana inakuwa gharama sana bali fanya REGISTERED.

    Goodluck!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 10, 2007

    Una hoja hapo lakini matumizi yako ya Kiswa-ngilish yamenitolea hamu kabisa ya kuendelea kusoma. Kama unafahamu Kiingereza si afadhali ungetumia lugha hiyo tu? Mnakera na lugha yenu hiyo.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 10, 2007

    DHL ndo jibu mzee...... i can see steam coming through ya ears duh......

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 10, 2007

    Mdau nakuunga mkono kuna tatizo kubwa na posta Tanzania. Hivi ninavyoandika mail yangu ya muhimu inasiku ya kumi na moja haijafika nimetuma na Royal Mail(UK post)special delivery tangu 27/04 nimei-track online ilifika Dar mapema lakini mlengwa haijamfikia. Nimetuma barua pepe kwa customer service posta Dar hakuna jibu, simu yao waliyoweka kwenye website haipatikani.

    Hii yote tisa, nilituma mobile phone mbili moja mpya nyingine nzee wameiba mpya wamekabidhi ya zamani. Na huwezi kutrack parcel yako online ikishawafikia Posta Tanzania.

    Afisa habari wa Posta aje hapa michuzi blog atuambie kwa nini na wale wote waliopatwa na tatizo kama hili la kupoteza vitu wajitokeze hapa na kutoa maoni ili wajue ukubwa wa jambo hili.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 10, 2007

    Nakubaliana kwa 100% na mtumaji wa ujumbe huu. Mimi binafsi nilikwisha acha hata kutuma picha tu kwani kila ukituma hazifiki zilikokusudiwa. Vifurushi vyenye thamani ndo kabisa usithubutu. MDAU-CANADA.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 10, 2007

    na nyie wahaya hua mna matatizo sana unataka kulinganisha U.S na bongo?Bongo jamani miundo mbinu,kuna usafiri gani kutoka DAR kwenda KWAMACHUMU whatever tha fuck is?Bukoba mjini penyewe ni mpaka uweke kifurushi kwenye basi la njia ya kati kupitia singida amabyo hua hayajulikani destination yanafika lini.Kwanza linaweza kuharibika singida vifurushi vyote vikaibiwa.
    Posta yes ina magari machache ambapo ingeweza kufanya kama UPS ambayo kwenye big hub iko na ndege zake binafsi lakini sasa kupeleka gari kwamachumu barua yenyewe iko moja and that one barua is once a year,does it make any sence ma friend.Arusha na Dar UPS ipo same day delivery ila hiyo ni miji ya kibiashara,kua mvumilivu dogo we will get there someday though it is a snail speed.
    Babau wa kimeru.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 11, 2007

    ni kweli kabisa hawa posta wa kwetu shida tupu,mimi mwenyewe nilituma some documents tangu february hadi leo hazijafika imebidi niscan nitumie by emeil.
    mimi nawashangaa wanalalamika shirika linataka kufa halina fedha wakati wenyewe ndio wanaliua, kenge kabisa hawa

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 11, 2007

    POLE SANA. UJUMBE NI WA KWELI KABISA, LAKINI TAFADHALI USICHANGANYE LUGHA. KAMA NI KISWAHILI AU KIINGEREZA, SIO UNACHANGANYA-CHANGANYA. WEWE VIPI?

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 11, 2007

    Unajua we ndugu nadhani bado ni limbukeni sana. Hivi kama kweli ni mTanzania na waTanzania wote tuna lugha yetu ya Taifa, mbona unashindwa kuandika kwa kiswahili ? Hivi kweli umekosa ustaarabu kabisa wa kuwasialina na watanzania katika lugha yao husika. mambo ya kuchanganya kimombo na kiswahili yamepitwa na wakati. Pevuka Ndugu !!!samahani kama kauli yangu hii imekuudhi, lakini haya ndio maisha.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 11, 2007

    Ndg yangu unapaswa kuwa mvumilivu kabisa katika hili."First in, first served" sisi wewe tu unayetuma virushi huko Tanzania wapo watu wengi sana wanaotuma vifurushi hata sisi tuliopo ulaya hutuma na tunajaribu kuvumilia.


    Pia kumbuka miundo mbinu ya nyumbani na usafiri wetu huko.

    Huko wanaotuma mizigi pia wanaweza wasitume siku hiyi hiyo maana pia wanamizigo mingi si rahis kuibeba kwa wakati mmoja.Jingine ni swla la usalama wa vifurushi vyenyewe (Ukaguzi)ikiwa huwezi kuwa mwana usalama huwezi kulifahamu hili.lazima vikaguliwe kwa kiasi cha kutosha.

    Michu,tunakutuma nenda DHL wakupe sababu ,nilizoandika ni baadhi tu

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 11, 2007

    ndugu mdau kutoka usa pole sana. hawa wafanyakazi wa posta sijui wanamatatizo gani.. hata sisi tulioko nyumbani tunaipata fresh. licha ya majibu mabaya waliyonayo pia taratibu zao za utendaji ni kama wako enzi za kale za mawe. ni niko mza. ukitumiwa mfano pesa. kujua tu pesa zako zimekuja upange foleni its ok. tellar ana rundo la vitabu counter books sina uhahika kila mkoa la tabu lake, pia ana rundo la makaratasi ya fax na majidubwana mengine yamemzunguka. ukifika unataja jina, no. tarehe na zilikotoka,afu anaanza kupekuwa majitabu, anapekuwa weeeeeeeee, anakosa, anachukua rundo la makaratasi, anaperuzi weeeeee, anakosa, anarudia tena yaani takribani nusu saa anapekuwa, hapo umepanga foleni masaa mawili. msongamano chumba kdg hakuna ac. usafi chini ya kiwango, pakuka padogo pamejaa. hapo umefuata mali ya ofisi huwezi kususa ujiondokee, basi yaaaani uhwii!!! kichekesho ni kwamba mbele yake kuna licomputa, sasa mwana wane unajiuliza kwanini wasingekuwa wanagandamiza hizo data humo???? ivi wale watu ni profeshono au niaje. na kwanini . WANABOA. au urongwe umwandikie mwandikie mwanafunzi barua utumbukize kaelfu tano. utaona matokeo ya kipimabaridi.
    pole ndugu tena ila ndo ivyo posta yetu

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 11, 2007

    ndugu michuzi,
    najua hii si kazi yako-je inawezekana haya malalamiko yakafikishwa sehemu inayohusika??Tusibakie kupiga domo bila vitendo.
    Mfano: inawezekana kumtumia barua pepe yenye haya maoni meneja wa posta ili ashughulikie hili swala??

    Hao wadau wanaotaka kila mtu atumie DHL nafikiri wana-upungufu wa akili. Mie nafikiri tujitahidi kutatua matatizo sio kukimbia matatizo.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 11, 2007

    posta huwa wanachana barua au kadi ili kuona kama kuna hela hasa kama barua inatoka nje ya nchi!!!!
    hata tanesco wanasumbua mno ktk kuunganisha umeme. hela imelipwa lakini wanakuzungusha mara gari ya kubeba nguzo haipo, surveyor atakuja sijui lini... n.k.
    usumbufu sana huko home kwetu - umangimeza na urasimu usio na maana!!!!

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 11, 2007

    JAMANI KAMA UNAJUA KISWAHILI BASI ANDIKA KISWAHILI. NA KAMA HUJUI KINGREREZA BASI USIJARIBU CHA KUBABAISHA.

    KUISHI USA SIO KUJUA KINGREREZA KAMA HUENDI SHULE SANA SANA UNAJUA CHA KUONGEA MITAANI TU LAKINI CHA KUANDIKA HUWEZI.

    MNATUONYESHA KUWA HAMJIFUNZI CHOCHOTE HUKO. UNATAKIWA KUELEWA KUWA WASOMI WENGI WANAWEZA KUJUA LUGHA ZAIDI YA NNE KUU ULIMWENGUNI LAKINI AKIONGEA KIFARANSA HACHANGANYI KABISA NA KIINGEREZA, KUGERUMANI AU KISWAHILI.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 11, 2007

    Mkereketwa,
    Labda kama Michuzi itauhariri huo ujumbe kabla hajaupeleka huko posta. Inatia kichefuchefu jinsi lugha ilivyochanganywa humo. Mwandishi wake inaonekana kichwani ni zero kabisa. Samhani kwa lugha kali lakini sina namna nyingine ya kumwelezea mwandishi kama huyo.

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 11, 2007

    MKEREKETWA mi nadhani akili yako ndo inakereketwa. hii ni dunia ya soko huria unachagua huduma unayoitaka au inayokufaa na ni jukumu la mtoa huduma kupandisha viwango vya huduma ili kupambana na ushindani, pumbafu wewe eti tung'ang'anie posta tu wakati wanatuibia mizigo yetu kila siku sababu tu ni shirika la wazawa? ibinafsishwe basi kama ndo hivyo

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 12, 2007

    Jamni posta ya bongo kujuana....... Ukiona mizigo yako haifiki. Next time mtumie postmaster shati na ka-tshirt halafu weka kamzigo kako huko ndani,you'll see kama hiyo parcel haijafika in 10days. Mimi nimejaribu na since then barua na mizigo inafika bila wasi as long as kuna kajizawadi ka postmaster your set. Good luck!!!!

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 12, 2007

    pole sana mie yalinikuta pia kutoka hapa marekani,inatakiwa siku wakisema utafika unanza kuwahs moto nyumbani ukiona haujafika basi wewe simu kama kichaa hapo dar na mkwara sana kwamba ukirudi utawsha moto hapo ofisini kwao alllaaah mzigo utatoka nilituma parcel arusha wakataka kuiba waliutoa baada ya siku 2 tu ,wezi sana dawa yao jikoni sana toka miaka hiyo posta tanzania weziiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 12, 2007

    Watu wengine wapumbavu sana eti wamekomalia lugha kuchanganywa wakati wao wenyewe hawajioni wanapochanganya lugha wakati huo huo.

    Mfano fala mmoja hapo juu analalamikia lugha wakati mwenyewe kachanganya, hivi neno "zero" ni Kiswahili?! Jinga kabisa unashindwa hata kusimamia unachodai kutetea!

    Cha msingi ni kwamba ujumbe umefika acheni hizo ala! Huyo mkereketwa aliyeko Marekani awe anasoma au la hayawahusu sana sana mnadhihirisha jinsi mlivyo na roho za kwanini!

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 13, 2007

    Nimefanya kazi posta kwa muda wa miaka miwili hadi nilipokuja UK kwa masomo. Ningeweza kutoa maoni ambayo wadau wengi wametoa kama ningekua sina knowledge yoyote ya postal industry. Lakini kwa kuwa nimefanya kazi huko na sasa ninaishi ughaibuni kama ambavyo majority ya watoa hoja kuhusu suala hili, naamini maoni yangu yatakua na uzito kidogo.

    Watanzania wengi walioko ughaibuni wanakuwa wepesi kujump into conclusion kila mara mizigo yao inapopotea na kusema kuwa imeibiwa posta za nyumbani. Unaona wazi kuwa kuna fikra kuwa parcels/barua haziwezi kuibiwa katika posta za ‘wazungu’, kama kuna wizi wowote wanaona ni lazima utafanyika nyumbani. Hii si sahihi hata kidogo, kama kuna wizi posta zetu za nyumbani ni wa scale ndogo sana. Sio chini ya mara tatu nimeona kwenye news wafanya Wafanyakazi wa posta za ulaya na America nao pia huiba, tena kwa kiwango kikubwa tu. Nimeona kwenye news (TV and papers) sio chini ya mara moja wafanyakazi wa posta za UK wakiwa matatani kwa wizi.

    Kingine ambacho wengi hawaelewi ni kwamba mashirika ya posta duniani husafirisha mizigo yao kwa kutumia vyombo mbalimbali vya usafiri, ndege in particular kama ni international mails/parcels. Kinachofanyika hapa ni kwamba wafanyakazi wa Posta watakwenda na furushi lao la barua na parcels na kuliacha mikononi mwa shirika la ndege ambalo nalo litaiacha mizigo hiyo mikononi mwa Laguage handling companies zinazo operate kwenye airports- naomba ieleweke pia kwamba kuna mianya ya wizi au upotevu katika mtiririko huu. Mwezi uliopita kuna video ilionekana nchi nzima hapa UK, kuliwekwa kamera ya siri kwenye changing room ya posta moja hapa UK baada ya tatizo la wizi kukithiri na wahusika walikamatwa.

    Kunakuwa na matatizo mengi ya upotevu na wizi wa mizigo pale ambapo mzigo wenye barua na parcels unapita in transit, nikimaanisha mzigo huo unapandishwa ndege zaidi ya moja. Kama ni US utatoka huko uliko, utashushwa na kupandishwa New York, kama ndege ni Emirates zoezi hilo litafanyika tena Dubai then ndo unapandishwa ndege ya mwisho. Ni jambo la kawaida sana, kwa mfano, wafanyakazi wa language handling companies kufanya makosa na kuupeleka mzigo wa Tanzania Taiwan na utakapofika huko itategemea umefikia mikononi mwa nani.

    Kuhusu uchelewesho, sina proof na hili ila nahisi pia wenzetu wa posta za nchi zilizoendelea wanazipa priority parcels/barua za kwao na zile zinazokwenda kwenye nchi zilizoendelea, wanadeal na za nchi maskini mwishoni. That is kama kuna ndege inakwenda Dubai toka New York na nafasi ni ndogo, mizigo ya UK , Germany, etc itapewa first priority na kama kuna kanafasi kadogo kakibaki baadhi ya mizigo inayokwenda Tanzania na Togo yaweza pakiwa. Hii inawezekana, lakini ni hisia zangu tu. Najua utakua unajiuliza- vipi kuhusu uchelewesho wa ndani? Ni wazi kwamba shirika la Posta bado halijawa na usafiri wa uhakika. Magari machahe ya posta yana operates katika routes za Dar- Iringa-Mbeya, Dar-Moshi- Arusha, Dar-Korogwe- Tanga, sina hakika kama kumekuwa na routes mpya tangu nimeondoka. Barua za route hizi huwa zinasafirishwa usiku wa siku zinapopokelewa. Kule ambako magari ya Posta hayafiki- usafiri wa ndege, mabasi na trains hutumika na vyombo vyoote hivyo vina matatizo yake na ukijumlisha matatizo ya mifumo yetu ya usafiri kwa ujumla-ni kawaida kusikia abiria wa traini au basi wamekwama njiani kwa siku tatu au zaidi, au majambazi wamepora abiria na mizigo ikiwemo ile ya posta kwenye basi Fulani.

    Naomba ieleweke kwamba wafanyakazi wa posta za nyumbani wanafanya kazi nzuri kwenye mazingira magumu na tunakuwa hatuwatendei haki kama kila mara tutakuwa tukiwalaumu kila kunapotokea wizi au upotevu wa vifurushi na naona its immoral kila mara kucompare na mazingira tunayoishi sasa huku ughaibuni, kwanini tunasahau tulikotoka? Tusiwe wepesi kumlaumu muhudumu kwenye restaurant chakula kinapokuwa kibaya wakati yeye kakileta mezani tu, mbona mpishi hatumgusi?

    Nawasilisha kwenu wadau- siwakilishi shirika la posta katika maoni yangu, nachangia tu kama wengine, akhsanteni.

    Former TPC employee.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 14, 2007

    Huyo anayesema wafanyakazi wa Uk na marekani wanaiba pia. Sijui juu ya UK lakini USA ukituma package wakakupa intenational custom parcel slip. Iwe umetumia njia ya kamaida au ems. Uwe umeweka insurance au la. Kuna number ambayo ipo pembeni hivi ukipiga simu utaona kabisa jinsi mzigo wako unavyoondoka kutoka nje ya nchi. Na pia ukiinsure ndio kabisa unaweza kuutrack kwenye internet pia mpaka unavyoingia TZ. Baada ya hapo hutauona tena umeenda wapi. Kwa vile tracking system ya TZ nadhani hawajalink na nchi za nje.

    Ila hata USa barua ndogo zinapoteaga. Ila hata miezi unaweza ukakuta unaletewa. Makosa yapo kila mahali lakini ratio ya hayo mambo ni kubwa sana kwa TZ. Na wamezidi kwa uizi na hongo. Kama humjui mtu posta utalipa sana tu

    ReplyDelete
  38. Watanzania wengi wanaoishi ng'ambo wanalalamika kwamba barua zao zinaibiwa na vifurushi vyao vinaibiwa na wafanyakazi wa posta nchini Tanzania. Mimi ni mmoja wao. Nimeishi USA zaidi ya miaka 20 na vifurushi nilivyotuma nyumbani viliibiwa. Hata barua pamoja na picha ziliibiwa.

    Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba ingawa viongozi wetu wanajua kuhusu tatizo hili, hawajafanya chochote kupambana na wezi.

    Acheni kutumia shirika la posta. Bila shaka hata Raisi Kikwete anajua kuna wizi sana katika shirika la posta kama ulivyo serikalini.

    Pia nakubaliana na wazalendo wanaosema tusichanganye lugha. Na ni kweli kwamba hata Watanzania wengi walioishi USA na UK kwa miaka mingi hawajui Kiingereza. Kimombo wanachoandika ni kibovu sana. Sijui wana elimu gani.

    Hata Kiswahili chao ni kibovu.

    ReplyDelete
  39. Samahani naombeni kuuliza hivi ukiwa mtu kutoka Abroad anataka kukutumia parcel utatakiwa kutumia address ya posta au address ya ( EMS) au ( DHL) kupokelea hiyo parcel ndugu zangu kwa anayejua naomba anieleweshe pindi atakapo soma ujumbe huu please

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...